Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Nimeambiwa kwamba wanasiasa wetu wameanza utoto na kupoteza muda kwa mambo yasiyo na tija. Eti wanatushawishi tususie Vikao na Ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo. Kwanza tujiulize, Uzoefu wa kuongoza hata Vikao vya Mtaa tunao? Wengi tumetoka vijiwe vya Kahawa hata Halmashauri hatujui zinaendeshwaje! Si tutumie muda huu kujifunza na kufanya mambo waliyotutuma Wananchi? Au tunatafuta umaarufu ambao tulishaupoteza kitambo??