UKAWA tumuunge mkono Rais wetu Magufuli

UKAWA tumuunge mkono Rais wetu Magufuli

the reformer

Senior Member
Joined
Dec 15, 2014
Posts
195
Reaction score
68
Kiukweli Dr.Magufuli yuko vizuri. Jamaa ana determinasion na dhamira ya kweli ya kujenga nchi yetu.

Nawasihi wana UKAWA wenzangu tofauti zetu tuziweke kando.

Tumu encourage Rais wetu nchi yetu ifike mbali. Kama John Kerry na Obama wameweza why not us?
 
japokuwa kabebwa akifanya vizuri tutampongeza kwa kulitendea mema taifa letu..akifanya maigizo hatutasita kukosoa.
 
Huyo ni Rais wa ninyi wachache mliompa kura, kwa ajili ya maslahi yenu! Hiyo ndiyo hasara ya kulazimisha uongozi, kwa kuiba kura. Angalieni sasa jinsi mnavyotafuta support ya sisi tulio wengi! Waswahili waliona mbali, pale waliposema, "wengi wape"!
 
Kiukweli Dr.Magufuli yuko vizuri.Jamaa ana determinasion na dhamira ya kweli ya kujenga nchi yetu.Nawasihi wana Ukawa wenzangu tofauti zetu tuziweke kando.Tumu encourage Rais wetu nchi yetu ifike mbali.Kama John Kerry na Obama wameweza why not us?

Kama angepata urais kwa kura za uhalali UKAWA tungempa support. Ila kwa kuwa aliingia madarakani kwa kura za wizi, UKAWA hatuko tayari kumpa support. Tunajipanga kushinda uchaguzi ujao. Ninyi mliompa kura mpeni support
 
Huyo ni Rais wa ninyi wachache mliompa kura, kwa ajili ya maslahi yenu! Hiyo ndiyo hasara ya kulazimisha uongozi, kwa kuiba kura. Angalieni sasa jinsi mnavyotafuta support ya sisi tulio wengi! Waswahili waliona mbali, pale waliposema, "wengi wape"!
Wewe kweli gumegume. Zinakutosha mwenyewe!
 
Last edited by a moderator:
Kama angepata urais kwa kura za uhalali UKAWA tungempa support. Ila kwa kuwa aliingia madarakani kwa kura za wizi, UKAWA hatuko tayari kumpa support. Tunajipanga kushinda uchaguzi ujao. Ninyi mliompa kura mpeni support

Kamanda usikubali kubebwa na cheap politics
Uko wapi ushahidi wa yeye kuiba kura
 
Umenichefua Mkuu!!! Wewe sio ukawa!!! Nyamaza tu, hujui machungu tuliyonayo!! Anyway mapema Sana saivi,tuendelee na kazi.
 
Na yule Rais wenu mwengine mtafanya naye nini... (sorry I didn't mean this)
Uchaguzi umekwisha watanzania wameshinda tunasonga mbele wewe baki na jealous zako kwa Lowassa ambazo najua hazitokusaidia mwenzako ametimiza haki yake ya kugombea na anaendelea kula utajiri wake ambao hata ukusanye mali za ukoo wako haziwezi kufika hata robo yake,

wewe huyo rais wako Slaa amekusaidia nini hadi sasa.
 
Duh! Ok basi.time will tell
Vitu vingine havihitaji time Mkuu!!! Ushaambiwa sisiem ni ile ile!!!! Shida ni kwamba hicho chama kinawenyewe!!! Kuna Mkuu hapo juu kasema Jamaa aunde tume Huru na katiba mpya!! Baaasi.... Kinyume na hapo bado TUMEKALIA KUTI KAVU.
 
mkuu tumwache dk JPM afanye kazi ni kwa maslahi ya watanzania wote na pale atakapoharibu ni kwa wote pia
 
Huyo ni Rais wa ninyi wachache mliompa kura, kwa ajili ya maslahi yenu! Hiyo ndiyo hasara ya kulazimisha uongozi, kwa kuiba kura. Angalieni sasa jinsi mnavyotafuta support ya sisi tulio wengi! Waswahili waliona mbali, pale waliposema, "wengi wape"!

Majibu yako sawa na jina lako, Sasa kwa akili yako tunataka support ya nini???, ukisuport usisuport Magufuli mbele kwa mbele, hamzidishi wala hampunguzi, hamvuti wala hamkokoti, hamuwashi wala hamuzimi, labda hukumuelewa mtoa mada amemaanisha, muache kuponda hata kwa mazuri, penye baya mseme baya na penye uzuri toeni credit, CCM hawaitaji support yoyote toka kwenu.
 
Vitu vingine havihitaji time Mkuu!!! Ushaambiwa sisiem ni ile ile!!!! Shida ni kwamba hicho chama kinawenyewe!!! Kuna Mkuu hapo juu kasema Jamaa aunde tume Huru na katiba mpya!! Baaasi.... Kinyume na hapo bado TUMEKALIA KUTI KAVU.

Tume huru na katiba mpya.kwa masilahi yetu ukawa .?au kwa masilahi ya nchi? Naomba unielewe dhamira yangu ni nchi kwanza vyama baadae.
 
na pengine ukawa wangekuwa wana wabunge wengi zaidi ya ccm hata mimi ningekua na nnamashaka.sasa wabunge wa ccm ni wengi na wapiga kura haohao ndo ulikua mtaji wa pombe sasa kaiba kura kvp?

CCM sio wajinga kiasi hicho wachakachue za urais waache za wabunge! Si ingekuwa wazi sana? Nape kapata kura zisizofika 1000, lakini ushindi kapewa yeye, Mwakyembe kashinda kweli? Na wengine wengi tutapoteza muda kurudi huko.
Tatizo nyie mnapenda sana ukweli ugeuke uongo na uongo uwe ukweli. Problem kubwa ni tume isiyo huru na vyombo vya dola karibu vyote vilisimama kuhakikisha by crooks and hooks chama kilicho madarakani kinashinda
 
Majibu yako sawa na jina lako, Sasa kwa akili yako tunataka support ya nini???, ukisuport usisuport Magufuli mbele kwa mbele, hamzidishi wala hampunguzi, hamvuti wala hamkokoti, hamuwashi wala hamuzimi, labda hukumuelewa mtoa mada amemaanisha, muache kuponda hata kwa mazuri, penye baya mseme baya na penye uzuri toeni credit, CCM hawaitaji support yoyote toka kwenu.

Ungenyamaza pia ingekusaidia kumbe hujui wanasaidia nini kweli wewe ni bongo lala uwe unajitahidi kuangalia bongo kids utapata huko hata akili ya kuanzia
 
Ungenyamaza pia ingekusaidia kumbe hujui wanasaidia nini kweli wewe ni bongo lala uwe unajitahidi kuangalia bongo kids utapata huko hata akili ya kuanzia

Duh! yani wee ndo tahira kabsaa na nahisi umejibu ukiwa umelewa?? kwanza unajua kusoma?? au kuna mtu amekusomea? Fatilia hayo meneno yenye red labda utaelewa kidogo-: Msaada wao ni Kukosoa Serikali pale inapokosea, na mimi nimesema penye baya mseme baya na penye uzuri msifie....Na mleta mada alimaanisha support ya kusaidiana nae katika hayo mema ukiwa mpinzani sio lazima kila kitu unabisha tu, mwisho wa siku hata wananchi watawaona hamna ni njema, mana wao wanayaona ni mazuri kwao nyie mnapinga na kukosoa tu, mtajipoteza na kushusha hadhi ya upinzani japo tayari imeshashuka bado kuisahau.
 
Back
Top Bottom