Kweli, mimi ni muumini wa upinzani tokea mwaka 1992,wakati huo huo wazazi wangu wote wawili walikuwa ni wanaccm,tena viongozi,ila nakumbuka mama yangu aliwahi kuninunulia kalenda niliyoipenda mwaka 2000 iliyokuwa na picha ya mgombea urais wa upinzani kwa sababu tu alijua naipenda!! Hata sasa Mama ni mwana ccm, najaribu kubadili itikadi yake taratibu bila karaha,ila sitavumilia siku nikikuta mwana ukawa mwenzangu akimzomea!!! Nitaweka itikadi pembeni!! Wengi wetu pia wana ndugu,jamaa ama marafiki walio upande mwingine wa itikadi,sidhani kama watavumilia kuona wakidhalilishwa kutokana na msimamo halali walionao,si heshima,si ustaarabu kumdhalilisha mwenzio kutokana na itikadi yake kutofautiana na yako,tuzomeane hukuhuku JF,yasifike kwenye familia zetu,kwenye jamii zetu,maana mtoto wako pia siku moja ataweza kukuzomea!utachukua hatua gani?