UKAWA tuache Kuzomea Wavaa Nguo za CCM

UKAWA tuache Kuzomea Wavaa Nguo za CCM

lonyorengai

Member
Joined
May 12, 2008
Posts
71
Reaction score
35
Imekuwa kero sasa hususan katika miji mikubwa kuona au kusikia zomea zomea kutoka kwa wapenzi, wanachama na mashabiki wa muungano UKAWA kwa wananchi wanaopita mitaani hali wamevaa nguo za CCM. Hili la kuzomea si sahihi kwa kuwa sio lazima wote tuwe wana UKAWA. Tuwasamehe na kuendelea kuwa wastaarabu kwa kuwa tunafanya kampeni za kistaarabu.Najua ni vigumu kuendelea kuona nguo za ccm au ccm yenyewe lakini mwisho wa yote tutaishi ndani ya Tanzania yetu tukiwa tofauti kiitikadi japokuwa ccm watakuwa wachache sana ama hakuna kabisa. Tuwaache na ubaya wao na maangamizo ndani ya mioyo yao kwa kukataa ukweli wa kukataliwa na wapenda mabadiliko. Suluba ya UKAWA inawatosha tusiwaumize zaidi.
 
Mpende adui yako na umuombee wandugu ingawa ngumu. Tudumishe amani
 
Lowasa aliwaambia mjitahdi kuwa wastaarabu.Anajua kuwa nchi haiwezi kabidhiwa kwa wahuni.Na tabia hzo zinazidi kuwafanya jamii iwaone msio kuwa na sifa ya kuongoza nchı.
 
Tuushinde ubaya kwa wema. Magamba sio lazima yanyofolewe. Unaweza tu kuloweka yakadondoka yenyewe
 
Hata mimi huwa cwezi vumilia nikiona mtu kavaa jez za sisiem
 
haya majamaa au mawomen ya ccm ni kuyazomea tu... kwani yanataka kutuchelewesha kuing'oa ccm!
 
Kweli, mimi ni muumini wa upinzani tokea mwaka 1992,wakati huo huo wazazi wangu wote wawili walikuwa ni wanaccm,tena viongozi,ila nakumbuka mama yangu aliwahi kuninunulia kalenda niliyoipenda mwaka 2000 iliyokuwa na picha ya mgombea urais wa upinzani kwa sababu tu alijua naipenda!! Hata sasa Mama ni mwana ccm, najaribu kubadili itikadi yake taratibu bila karaha,ila sitavumilia siku nikikuta mwana ukawa mwenzangu akimzomea!!! Nitaweka itikadi pembeni!! Wengi wetu pia wana ndugu,jamaa ama marafiki walio upande mwingine wa itikadi,sidhani kama watavumilia kuona wakidhalilishwa kutokana na msimamo halali walionao,si heshima,si ustaarabu kumdhalilisha mwenzio kutokana na itikadi yake kutofautiana na yako,tuzomeane hukuhuku JF,yasifike kwenye familia zetu,kwenye jamii zetu,maana mtoto wako pia siku moja ataweza kukuzomea!utachukua hatua gani?
 
Simnatuita Wanywa Viroba! Zomea Haooo Majiziiii Oooooooooo!
 
Back
Top Bottom