UKAWA the walking dead!!

UKAWA the walking dead!!

KANYAMA

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2011
Posts
1,590
Reaction score
2,386
Ndugu wana JF:
Salaam.
Napenda niwapongeze kwa ukomavu wenu WA kujadili maswala mbalimbali ya kisiasa na mustakabali wa maendeleo Ya nchi yetu. tarehe 25-oktoba -2015 tutachagua viongozi WA kisiasa watakao tutoa hapa tulipo na kutufikisha ktk nchi ya ahadi ambayo sisi sote kama watanzania tutajivunia.

Mchakato wa kampeni unaoendelea unatoa taswira ya Nani ataweza kupata ushindi aidha mkubwa au kidogo. wakati kampeni zinaanza tuliona nguvu kubwa ya vyama vikubwa viwili yaani CCM na CHADEMA kupitia UKAWA. Hali ilikuwa ikionesha KUJAA kwa watu katika mikutano hasa ya vyama hivi na kutoa viashiria vya awali juu ya nini kinaweza kuwa ni kipimo katika kubashiri matokeo ya kura.

Jambo la pili likawa ni kunadi SERA na mikakati iliyomo katika ilani za vyama hivi. uwezo wa wagombea katika kunadi na kuzielezea sera hizo na namna ya utekelezaji wake umekuwa ni MTIHANI mwingine unaohitaji uelewa mpana wa maswala ya uraia kwa Wapiga kura. mathalani wagombea wamekuwa wakitoa ahadi bila kutoa ufafanuzi wa Kina na mipango inayofikirika ya jinsi ya kutekeleza mikakati hiyo.

Katika mwendelezo wa mambo yote haya linajitokeza swala la UTULIVU ndani ya vyama au umoja. tumeshuhudia UKAWA ukipata misukosuko mingi inayosababishwa na muundo wa umoja huo na hata kusababisha baadhi ya viongozi wake wa muhimu kabisa(prominent leaders) wakiachia madaraka ndani ya vyama vinavyounda umoja huo. hii inanogeshwa nakutiwa Chumvi na migogoro ya wagombea wa udiwani na ubunge ambapo kwa Makubaliano ya UKAWA wangeweza kusimamisha wagombea kutoka chama kimoja na hatimaye Kaungwa mkono na wote. kimsingi mikakati huu ulikuwa ni sahihi kabisa katika kuhakikisha UKAWA wanapata ushindi na kisha kuitoa CCM madarakani.

Upepo wa KUHAMA kwa viongozi na wanachama Umegeuka na sasa kunashuhudiwa viongozi na wanachama wengi zaidi kutoka vyama vinavyounda UKAWA kwenda CCM ukilinganisha na hapo awali wakati wanachama na viongozi wengi kutoka CCM walihami a UKAWA.

Mtizamo wangu na wengine wenye kufatilia mambo haya bila ushabiki Watakubaliana nami Kuwa hali ndani ya UKAWA ni sawa na mtu anayetembea akiwa mfu.

Najua kutakuwa na kukinzana kwa mitizamo ila ni bora kumeza dawa kuliko kutomeza kabisa na Hali ikiwa mbaya zaidi matibabu yake huwa nikupelekwa kaburini. uwezekano wa UKAWA kuweza kupata ushindi unafifia zaidi kadri siku zinavyosonga. watanzania wamemulika nini kitatokea kama UKAWA watapewa ridhaa. MIGOGORO, mfumo wa uundwaji na Makubaliano ya uwepo wa UKAWA na utekelezaji wa yale yaliyokubaliwa unazidi kuongeza MASHAKA miongoni mwa watanzania juu ya muskabali wa uongozi wa taifa hili chini ya UKAWA.

Wengi wanahoji juu ya AFYA ya Mh. Lowasa na uwezo wake wa kuelezea na kusimamia mikakati na sera za chadema ndani ya UKAWA kwenye majukwaa mbalimbali ndani na nje ya nchi. Majukwaa kama ya world economy forum na mengine. hili linajidhihirisha pale Mh Lowassa anapomudu kuhutubia kwa dakika chache tu kunadi na kueleza mikakati ya kina ni kwa kiasi gani ataenda kamaliza matatizo yaliyopo. Zaidi zimeshuhudiwa ahadi ambazo watanzania wengi wamezizoea kuzisikia.

KARIBUNI..
 
Ukawa wameshakata tamaaa, wajipange 2020 na. Waje na mgombea mwingne la sivyo Zitto kabwe atawaprove wrong
 
kwenye hili la kutoelewana ndani ya vyama, ni kweli magufuli amemfukuza mwigulu kutoka kwenye campaign team yake?, nithibitishieni ili nimpe crediti mzee maguufuli
 
Nafikiri ccm ndo wamechanganyikiwa zaidi ukiona mgombea anaanza kunadi Sera za wapinzani wake, akaanza kutumia nembo za wapinzani akidhani labda ataaminika zaidi.Jiulize kama kwenye mikutano yake anajaza watu wengi kwanini anababaika kupita kiasi hadi kufikia hatua ya kusema Saddam alikuwa rais wa kuwait, hivi nyie hamuoni kuwa hizo ni kasoro kubwa ?, sasa ameanza kutumia na misiba, toka lini Magufuli akawa karibu na jamii iliyomzunguka ? Huyu marehemu sidhani kama aliwahi kununulia hata VOCHA.Huko biharamulo/chato albino walikuwa wanapata shida kweli wakati wa mauaji ya kikatili lakini mliwahi kumuona magufuli anatoa msaada wowote kwa hao waathirika, lakini sasa ivi anajifanya kuwa nao karibu
.hizo hadaa watu tumeishazichoka.
 
UKAWA>IKAWA>UKIWA. Yaani MAGUFULI FOR CHANGE Ndo mpango mzima
 
Ndugu wana JF:
Salaam.
Napenda niwapongeze kwa ukomavu wenu WA kujadili maswala mbalimbali ya kisiasa na mustakabali wa maendeleo Ya nchi yetu. tarehe 25-oktoba -2015 tutachagua viongozi WA kisiasa watakao tutoa hapa tulipo na kutufikisha ktk nchi ya ahadi ambayo sisi sote kama watanzania tutajivunia.

Mchakato wa kampeni unaoendelea unatoa taswira ya Nani ataweza kupata ushindi aidha mkubwa au kidogo. wakati kampeni zinaanza tuliona nguvu kubwa ya vyama vikubwa viwili yaani CCM na CHADEMA kupitia UKAWA. Hali ilikuwa ikionesha KUJAA kwa watu katika mikutano hasa ya vyama hivi na kutoa viashiria vya awali juu ya nini kinaweza kuwa ni kipimo katika kubashiri matokeo ya kura.

Jambo la pili likawa ni kunadi SERA na mikakati iliyomo katika ilani za vyama hivi. uwezo wa wagombea katika kunadi na kuzielezea sera hizo na namna ya utekelezaji wake umekuwa ni MTIHANI mwingine unaohitaji uelewa mpana wa maswala ya uraia kwa Wapiga kura. mathalani wagombea wamekuwa wakitoa ahadi bila kutoa ufafanuzi wa Kina na mipango inayofikirika ya jinsi ya kutekeleza mikakati hiyo.

Katika mwendelezo wa mambo yote haya linajitokeza swala la UTULIVU ndani ya vyama au umoja. tumeshuhudia UKAWA ukipata misukosuko mingi inayosababishwa na muundo wa umoja huo na hata kusababisha baadhi ya viongozi wake wa muhimu kabisa(prominent leaders) wakiachia madaraka ndani ya vyama vinavyounda umoja huo. hii inanogeshwa nakutiwa Chumvi na migogoro ya wagombea wa udiwani na ubunge ambapo kwa Makubaliano ya UKAWA wangeweza kusimamisha wagombea kutoka chama kimoja na hatimaye Kaungwa mkono na wote. kimsingi mikakati huu ulikuwa ni sahihi kabisa katika kuhakikisha UKAWA wanapata ushindi na kisha kuitoa CCM madarakani.

Upepo wa KUHAMA kwa viongozi na wanachama Umegeuka na sasa kunashuhudiwa viongozi na wanachama wengi zaidi kutoka vyama vinavyounda UKAWA kwenda CCM ukilinganisha na hapo awali wakati wanachama na viongozi wengi kutoka CCM walihami a UKAWA.

Mtizamo wangu na wengine wenye kufatilia mambo haya bila ushabiki Watakubaliana nami Kuwa hali ndani ya UKAWA ni sawa na mtu anayetembea akiwa mfu.

Najua kutakuwa na kukinzana kwa mitizamo ila ni bora kumeza dawa kuliko kutomeza kabisa na Hali ikiwa mbaya zaidi matibabu yake huwa nikupelekwa kaburini. uwezekano wa UKAWA kuweza kupata ushindi unafifia zaidi kadri siku zinavyosonga. watanzania wamemulika nini kitatokea kama UKAWA watapewa ridhaa. MIGOGORO, mfumo wa uundwaji na Makubaliano ya uwepo wa UKAWA na utekelezaji wa yale yaliyokubaliwa unazidi kuongeza MASHAKA miongoni mwa watanzania juu ya muskabali wa uongozi wa taifa hili chini ya UKAWA.

Wengi wanahoji juu ya AFYA ya Mh. Lowasa na uwezo wake wa kuelezea na kusimamia mikakati na sera za chadema ndani ya UKAWA kwenye majukwaa mbalimbali ndani na nje ya nchi. Majukwaa kama ya world economy forum na mengine. hili linajidhihirisha pale Mh Lowassa anapomudu kuhutubia kwa dakika chache tu kunadi na kueleza mikakati ya kina ni kwa kiasi gani ataenda kamaliza matatizo yaliyopo. Zaidi zimeshuhudiwa ahadi ambazo watanzania wengi wamezizoea kuzisikia.

KARIBUNI..

Mtazamo wako sio sahihi na sio wa kisomi, ila ulichokiandika ni mtazamo wa kishabiki. Kama wewe ni msomi basi acha ushabiki na angalia uhalisia wa mambo
 
Najua yamkini wewe ni mshabiki wa ccm, vizuri. Lakini hebunishawishi katika hili. Mie sioni sababu ya ushabiki wako, labda kwanini magufuli awe ndo mpamgo mzina???? Huu sio wakati wa chama tawala kutupa ahadi, kwamba waanze kusema tutafanya hiki na kile.... Kwanini hawajaffanya ayo wanayoahidi kufanya kwa kipindi ambacho walikua madalakani???? Huu ni wakati kwa ccm kutuambia kile walichokifanya kwa muda wa miaka 30 tukianzia utawala wa mwinyi. Wanapoendelea kutoa ahadi wananipa mashaka..... Tunahitaji uongozi utakaoleta maendeleo. Ninauhakika 100% kua UKAWA ikiingia kutakua na maendeleo makubwa kwa sababu kama wasipoleta maendeleo ni lazima watatolewa madalakani, so lazima maendeleo yatakuwepo...... Na hii ni M4C yaani Movement For Change
 
Back
Top Bottom