UKAWA poleni, mlipewa promo mkaitumia vibaya sasa inakula kwenu!

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,069
711
Poleni sana UKAWA hii ndiyo siasa, mlikuwa kila wakati mikia juu bungeni, mara this is shame, mara serikali lege lege, na nk. hamkujua kuwa serikali ambayo mnapambana nayo ndiyo ilikuwa inawapa airtime na kuonekana kwa wapiga kura wenu, mlikuwa mkitumia TV ya serikali ya CCM kuisema na kuishtaki kwa wananchi kuwa serikali inaminya uhuru wa vyombo vya habari, miaka ya nyuma mtu akikukuta unaangalia bunge alikuwa anakushangaa, lkn hivi karibuni Bunge lilikuwa linavutia kuangalia.

UKAWA mliitesa serikali ya CCM mpaka ikakoswa koswa kudondoshwa na wananchi kwa pesa zake zenyewe, sasa wamezinduka wakaona promo kwa wananchi tunawapa wenyewe harafu wanasema serikali inaminya vyombo vya habari. Ndg zangu wana UKAWA jipangeni upya kutafuta jinsi gani wabunge wenu watapata kuonwa na wapiga kura wenu, CCM kwa hili hawawezi kurudia kosa kuwapa promo.

Ushauri:
Tafuteni jinsi ya kurekodi mambo yenu bungeni hasa ile mijadara ya moto hata kwa kutumia simu then gharimieni kwenye TV nyingine km ITV, AZAM TV na nk. kwa sababu nasikia hairuhusiwi kuingia na camera, lkn huwezi kumzuia mheshimiwa mbunge kuingia na smart phone yake, fanyeni hivyo haraka la sivyo TBC watakuwa wanarusha vipindi vinavyoonyesha mambo mazuri tu.

Aksante Mh Mbowe, Lowassa na Mnyika kwa kusoma thread yangu.
 
Tutakao umia ni sisi wananchi,magufuli kaprove failure kwa hili!Anataka yeye tu ndio wananchi wamuone,shame
 
Aendelee kukurupuka na nape wake ukawa tuko smart watabana ila mwisho wataachia maana hakuna namna
 
utakuwa na matatizo ya kutojua kuwa kutoonyeshwa kwa bunge ni hasara kwako na ndugu zako waliopo vijijini sio chadema
kuwepo kwa bunge live kulitufanya kujua mambo mengi ambayo serikali ilikuwa inayaficha escrow na richmond ,serikali ilikataa,ununuz wa rada serikali ilikataa,lakini ushapavu wa viongoz wa upinzani ndio ulitufungua macho,sasa we baki unatanua meno ukifikiri inakomolewa chadema huku sukari unanunua 2500.
 
kwa taharifa yenu, ndiyo mmezidisha hasira kwa wananchi, subirieni 2020 ndiyo mtajua mbivu na mbichi, mtatafutana uchawi.
 
Akina Mbowe walifanya Siasa kipindi ambacho Mazingira ya kisiasa yaliboreshwa sana, unakuwa Mpinzani huku unafanya biashara wala hazisumbuliwi kwa Tax assesment wala figisu figisu, wanaokufadhili hawasumbuliwi na system mkajiona Makamanda wa Anga!
Sasa wajifunze kufanya Siasa kipindi hiki I'll wajue kuwa kulikuwa na Wapinzani wa kweli kuliko wao waliokubali kupoteza Mali mpaka madaraka.
Mzee Jumbe alikubali kupoteza Urais kuliko kupoteza Msimamo wake kwenye Muungano.
Oscar Kambona alikubali kupoteza Uwaziri na hata Uraia kuliko kupoteza Msimamo wake kwny Siasa ya kufikirika ya ujamaa
John Samwel Malecela alikubali kupoteza Uwaziri Mkuu kuliko kupinga Azimio la Bunge G55 1993 chini ya kina Njelu Kasaka.
Christopher Kasanga Tumbo kapoteza Mali na madaraka yake kwa kupinga Vijiji cha ujamaa.

We Mpinzani unaendesha Casino, unachukua Mikopo kwny Mifuko ya hifadhi ya Jamii n.n halafu unajiita Kamanda uliejitoa Mhanga? Hahaha
Mwingine yule wa Znz anajiita Mpinzani Watoto wake wapo vitengo nyeti vya serikali?

Wale Wapinzani wa Zamani wangekuwa wanapanga na kufanya Siasa katika mazingira ya Jk pengine wangefanya vizuri zaid ya hawa waigizaji!
 
Sasa ndio umeandika nini?
 
Mleta mada uelewa wake wa elimu ya uraia ni mdogo sana,jipime kabla hujatoa hoja jamii forum.La si hivyo unajivua.Kifupi hela ya serikali ni mali ya wote,siyo ya ccm.Ni kosa kisheria inaweza kupelekea kufungwa jela ukikwepa kulipa kodi uwe UKAWA au CCM.Hela ya serikali ni ya wananchi.
 
Mleta mada uelewa wake wa elimu ya uraia ni mdogo sana,jipime kabla hujatoa hoja jamii forum.La si unajivua uelewa wako.Kifupi hela ya serikali ni mali ya wote,siyo ya ccm.Ni kosa kisheria inaweza kupelekea kufungwa jela ukikwepa kulipa kodi uwe UKAWA au CCM.Hela ya serikali ni ya wananchi.
 
chama kinahangaika kujinusuru..cjui kitakatza nn tena aisee...ukiona mambo kama haya ujue ndio mwanzo wa mwsho wao
 
Ml
Mleta mada uelewa wake wa elimu ya uraia ni mdogo sana,jipime kabla hujatoa hoja jamii forum.La si hivyo unajivua.Kifupi hela ya serikali ni mali ya wote,siyo ya ccm.Ni kosa kisheria inaweza kupelekea kufungwa jela ukikwepa kulipa kodi uwe UKAWA au CCM.Hela ya serikali ni ya wananchi.

Mleta mada anaelewa sana. Tatizo hutaki kuelewa.
 
Bunge linapaswa kuonyeshwa live kwani wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao wanataka kuona wabunge wao wanachojadili kwa mstakabali wa maendeleo yao. Maendeleo hayana vyama, hivyo mbunge wa eneo husika anapojenga hoja juu ya changamoto fulani, na changamoto hiyo ikatatuliwa watakaofaidi ni wote bila kujalisha nani kampigia kura.
 
mkuu mleta mada,, ndio maana unaitwa MSHINO.
Kamuulize zzk jina lako linamaanisha nini
 
Back
Top Bottom