UKAWA nusura wazichape, kikao chavurugika. Ni kuhusu posho za Bunge

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Katika kikao chao cha jana walikuwa na agenda mbili. Moja, ni kuhusu hali ya siasa nchini baada ya jeshi la polisi kuzuia mikutano yao kufanyika kanda ya ziwa. Na pili, ni kuhusu agenda ya Naibu Spika kuweka msimamo rasmi kwa wabunge wanaotoka nje kutopokea posho tena kuanzia sasa..

Hii agenda ya pili ilipasua kikao, na mpaka ilifikia hatua ya ngumi kurushwa. Hali hii ilitokea baada ya wabunge wengi kutaka hatua ya kurudi bungeni na kulaumu uongozi kuwa ulikurupuka kuchukua maamuzi na kwa upande mwingine uongozi wa chama hicho wakitetea msimamo wao na kuapa kutokurudi bungeni kama Dr. Tulia atakuwa kwenye kiti.

Mpaka dakika za mwisho, baadhi ya wabunge walizira na kutoka nje ya kikao. Huku wakiapa kuwa kuanzia kesho wataanza kuingia na liwalo liwe hata kama ni kufukuzwa chama... "Hatuwezi kuvumilia hali hii, tuna majukumu majimboni, tuna familia, tuna watoto shule sasa kama wanataka tusichukue posho ni ukomo wa akili uliokithiri. Hatuwezi kamwe, na kuanzia kesho tunarudi mjengoni"... Moja wao amenukuliwa..

Mytake: Njaa haina baunsa!
 
Jamani ccm wanapata shida sana ukawa wasipoingia bungeni

Na waza tu,hivi jana Rais alitoa offer kwa ajili ya Vilaza tuangalie Bunge??Maana lilikuwa live jana.Au pesa jana zilitolewa kwa ajili ya waccm kuonekana wakipiga makofi ya furaha kwa kufanikiwa kuwatoa wapinzani ili Bajeti yao ipite bila bughudha.??

Nimemsikia Mwakyembe akisema Wapinzani 2020 wataisoma number sijui watanzania ni wale wale tunaosubiria wabunge wakipongeza kwa kuchaguliwa na kuipongeza serikali mwisho wa siku kuilaumu??Sijaelewa labda ndiyo sababu wanapata shida kukaa Bungeni
 
Kwa magufuli kila goti litapigwa walikuwa wanajishaua sasa moto wanaanza kuona unavyowaka pole yao.
 
Back
Top Bottom