Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,390
Kwa kadri siku zinavyoenda, tunashuhudia jinsi wanasiasa wa vyama vya upinzani pamoja na mawakala wao walivyo wanafiki. Unafiki huu umekuwa ukijengwa na kubadilika kila uchwao kutokana na mazingira yaliyopo. Wapinzani ni wepesi wa kubadili gia angani ambazo kwa kiasi kikubwa zinawagharimu wao. Ona baadhi ya mambo yafuatayo ambayo kwa hakika wamejichanganya mpaka wasijue wapi wanaelekea.
1. Tanzania tuige kwa Rwanda kwani licha ya nchi kuwa ndogo na rasilimali kiduchu, wametuzidi kimaendeleo.
-Ni aibu kwa Rais Magufuli kuiga kutoka kwa Rwanda nchi ambayo imepigana vita kwa muda mrefu.
2. Rais Kikwete ameua mahusiano ya Tanzania na Rwanda. Amejenga uadui ambao hauna maana kwa taifa
- Rais Magufuli ameenda Rwanda kujifunza udikteta wa kukandamiza upinzani
3. Rais Kikwete anasafiri sana nje ya nchi. Jina linalomfaa ni Mr FastJet
-Kuna haja kwa Rais Magufuli kusafiri sana nje ya nchi ili apate forum ya kubadilishana mawazo na wakuu
Wenzake jinsi ya kuendesha nchi.
4. Tunataka Rais dikteta ili nchi isonge mbele.
-Tunanyimwa uhuru wa kujieleza. Demokrasia inabinywa. Rais huyu ni Dikteta
Wadau, yapo mengi sana yanayokera kuhusu undumilakuwili wa hawa wapinzani. Wananchi wamewqchoka ila kwa sasa wanalazimisha waonekane wapo na wananchi.