SOCIOLOGISTTZ
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,615
- 929
1. Utangulizi UKAWA ni Umoja wa Kutafuta Katiba ya Watanzania, ambayo imehasisiwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, CUF na CHADEMA. Katika kuwepo kwake UKAWA imewafungua wananchi wengi macho kuhusu katiba iliyopo na mapungufu yake.Kujitoa kwa UKAWA kwenye bunge la katiba inaashiria kwamba katiba mpya haitaweza kupatikana kivyovyote vile. CCM na vibaraka wake wanaweza kuchakachua kanuni na kufanya uharamia wa kupindisha sheria ili katiba yao ipitishwe na bunge la katiba. Lakini hata wakifanya hivyo uzoefu unaonyesha kwamba hawataweza kupata theluthi mbili ya kura za maoni kwa wananchi wa Zanzibar hata kama watatumia jeshi kupora kura.
2. Ushirikiano ndani ya Bunge Ushirikiano ulioonyeshwa na Bunge la katiba unapaswa uendelezwe ndani ya bunge la Jamhuri ya Tanzania. Ili kufanikisha hayo mambo mawili makubwa inabidi yafanyike; · Mgawanyo wa mawaziri vivuli ufanyike upya ili kuruhusu vyama vya CUF na NCCR Mageuzi kuingia kwenye baraza kivuli. Ambalo linaweza kuwa hivi; Freeman Mbowe waziri mkuu kivuli na kiongozi wa upinzani bungeni, Habib Mnyaa – Naibu kiongozi wa Upinzani bungeni na waziri kivuli wa fedha, James Mabatia waziri kivuli wa Elimu nk. · Wapiganie kwa nguvu zote ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano sheria ya Tume ya Uchaguzi ifanyiwe marekebisho makubwa kwani haiko huru kabisa. Hata Mwenyekiti wa tume alishakiri kuwa tume yake haipo huru mbele Jaji Joseph Warioba.
3. Ushirikiano kwenye Uchaguzi.
Ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa timu ya UKAWA inahitajika ushirikiano usiokuwa na chembe ya hila kwa manufaa ya UKAWA na wananchi kwa ujumla wake Ili kufikia malengo hayo napendekeza yafuatayo; (a) Nafasi ya Urais na Wabunge Zanzibar iyachiwe CUF (b) Nafasi ya Urais Bara (Tanganyika) iyachiwe CHADEMA. (c) Prof. Ibrahimu Lipumba agombee Ubunge Tabora mjini (d) Freeman Mbowe agombee Ubunge jimbo la Hai (e) James Mbatia agombee ubunge wa Vunjo (alishawahi kuwa mbunge 1995 – 2000). (f) Nafasi za ubunge zinazoshikiliwa na washirika zibaki kwa chama husika, mfano; Lindi mjini – CUF, Ubungo – Chadema, Kasulu – NCCR Mageuzi. (g) Viti vya ubunge vingine vilivyobaki vigawanywe kulingana na matokeo ya uchaguzi 2010 na chaguzi nyingine ndogo zilizofuatia. Mfano mahali ambapo Chama washirika kilikuwa cha pili kutoka CCM basi kiruhusiwe kusimamisha mgombea. (h) Nafasi za madiwani nazo zifanywe kama nafasi za ubunge.
4. Hitimisho Ushirika huu umeonyesha ukomavu wa kisiasa uliopitiliza kuanzia hoja, hotuba na ushahidi kutoka katika nyaraka mbalimbali. Kazi hii UKAWA walioifanya inastahili pongezi kwa wananchi wote wapenda demokrasia na amani ya nchi hii. Ni matuamini ya Watanzania kuwa hamtaishia hapo bali mtachukua hatua mbele zaidi ya hapo na ikionekana inafaa basi mapendekezo niliyoyatoa kama mwananchi wa kawaida yazingatiwe kwa umuhimu wake. Kama Coalition itaingizwa kwenya mabadiliko ya tume ya uchaguzi basi jina la UKAWA liwe ni coalition mojawapo kama coaliaton zilizopo Kenya za CORD na JUBILEE. Mungu Ibariki Tanganyika, Mungu ibarika Zanzibar, Mungu Ibariki UKAWA na wananchi wote.
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Viongozi wa UKAWA ni wasikivu sana,
Jana kwenye mkutano wa UKAWA Pemba nilimsikia Freeman Mbowe akisema watashirikiana mpaka kwenye chaguzi mbalimbali. Big up sana UKAWA tupo pamoja na nyie.
Ma CCM yalikuwa yakisema Chadema ni chama cha wakristo na CUF ni chama cha waislamu, sasa wameungana na kuunda UKAWA. CCM wakiendelea kutumia hayo maneno watabaki na dini ya wahindu na wachache wasikuwa na dini kama Kingunge Ngombale Mwiru