UKAWA mjitafakari, mmepwaya sana

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,954
Mimi sipendi wala sitaki siasa zenye mwendelezo wa matukio lazimishi bila vision.
Kwa ujumla watanzania makini wanashindwa kuelewa muelekeo wa siasa za upinzani ndani ya nchi hii.

Sina uhakika kama wakuu wa ukawa wakiongozwa na CHADEMA kama wanaliona hili, lakini ni ukweli ulio wazi kwamba kuna ombwe kubwa la uongozi ndani na nje ya bunge letu tukufu.

Nje ya bunge ni kama hakipo ilhali ndani ya bunge ni ziro .
Nalazimika kuamini kwamba huenda Zuberi zitto kabwe na Dk wilbroad slaa ndio waliokuwa nguzo kuu ya uongozi wa chama hicho.kwani tangu viongozi hao kujiengua ndani ya CHADEMA, chama kimepwaya kama ndege yenye rubani bila kapteni.

CHADEMA imeongeza idadi kubwa ya wabunge lakini hakuna miongoni mwao anayeonekana kuwa na uwezo wa kujenga hoja kama ilivyokuwa enzi za Dk slaa na Zitto kabwe.

Upinzani bungeni una serkali kivuli bungeni,lakini imekuwa dormant. Ni kama haipo au kama ipo basi inafuata ushauri wa mtu au kundi fulani lenye malengo yake tofauti na lengo halisi la kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Mawaziri wake wamekosa uwezo na weledi wa kukusanya taarifa mbalimbali muhimu zinazovutia, zinazoweza kuitwa taarifa mbadala za baraza la Mawaziri kivuli wa kambi ya upinzani bungeni.

Badala yake Mawaziri kivuli wamebaki kutumia taarifa za matukio yaliyopita bila kutoa. .way forward, mwelekeo wa wapi sasa kama taifa tunapaswa kuelekea kisera na kisekta. Pamoja na kulalamika kwamba CCM wamepora sera zenu. Lakini mbona hamziendelezi katika hotuba mbadala zenu ili wananchi tuwaelewe na kuamini mnayoyasema?
Kwamba Server ya sera hizo mnazo?

Badala yake sasa mmebaki na na kukariri historia ya escrow, uuzwaji nyumba za serikali, bungeni live, nk.

Hakuna jipya la kuishauri serkali, au hata jipya la kuwashauri watanzania badala yake mmekuwa watu wa HARAKATI bungeni.wakati mnaelewa kabisa mnawawakilisha wapiga kura majimboni kwenu.sikatai au watanzania hawakatai msikemee au kufichua maovu yoyote ndani ya nchi yetu, huo ndio hasa wajibu wenu, Lakini changamoto hapa ni kwamba muwe mnakuwa na njia mbadala pale mnapokosoa ni vema kuwa na ubunifu wa njia au sera mbadala badala ya kugeuka wapingaji badala ya wapinzani.

Muwakumbuke wapiga kura wenu kuhusu maisha bora kule waliko miundombinu ya barabara, madawati, madawa, na hata walimu bora na sio bora walimu kama hili sakata la udom sasa hivi mnapolifanya kuwa mtaji wenu kisiasa au uklfichwaji wa sukari.

Mjipange kabla ya kukurupuka, mfano waziri kivuli mambo ya ndani anapokwenda kusoma taarifa ya uuzwaji nyumba za serikali. Wakati mnaye msemaji rasmi kambi ya upinzani bungeni wa wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano wapi na wapi?

Kwa hiyo mnapojiandaa kufanya kile mnachoamini nyinyi kama kuishitaki serikali kwa wananchi, pia mjiulize hao wananchi kweli kero yao kubwa ni ipi kati ya rushwa, ubadhirifu, elimu bora, madawa hospitali za umma,barabara, na miundombinu ya reli? ?

Au bunge live Wakati asilimia kubwa ya wananchi wenu au wapiga kura wenu wakiwa wanatumia vibatali bila umeme wa kuangalia hiyo television?

Ingawa ukweli huwa ni mchungu kuukubali mimi nimeanza kwa kuwakumbusha kwamba pamoja na bungeni live.lakini hiyo si kipaumbele cha walalahoi wa nchi hii, bali bungeni live huenda ikawa Ni mtaji zaidi kwenu kutegemea na matakwa ya wafadhili wenu ili waweze kuwaona mkitimiza kile walichowatuma live!

Ila pia muelewe karata hii ni kamari mnataka kuicheza. ...ikila kwenu hili mlitambue nikiwakumbusha mh kafulira alivyoweza kutuibulia masuala nyeti ya kutaifa Lakini akawa mzito jimboni kurudi kuwajulia kero wapiga kura hatimae kilichojiri Ni historia.

Najua kuna matusi yatakuja hapa ila nimetimiza wajibu wangu kama mtanzania commonmwananchi karibuni tuchangie
 
Wajukuu wa mwendo kasi wapi kazini, ila tulikuwa tunamkumbusha Baba wa mwendo sukari inashuka bei lini?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo kutegenea VILAZA kuongoza na kuwa wafuasi wa CDM limekuwa janga
Nabado
 
Kulia, kucheka, zote kelele, we mfate Dr slaa Canada, kama mbali mfate zito yupo hapa dar usibaki kulialia bila sababu, unachowaza ni kwa manufaa yako na familia yako, endelea kusimamia familia yako mambo ya chadema achana nayo, kama kinakufa we subiri mazishi.
 
Tatizo lako bado una amini katika watu, na ndipo ujinga wako umetamalaki.
 
Mleta mada kaandika jambo kuntu sana kwa wapenzi wa CDM wanaojitambua kamwe hawawezi kucomment pumba kama wanazo comment baadhi hapo juu...
 
Ni kweli kabisa Ukawa (upinzani) wa sasa ni tofauti na ule wa kina slaa na Zitto.

1. Upinzani wa akina Zitto na slaa ulikuwa ni wa kiwanaharakati.

2. Upinzani wa sasa (ukawa) ni wakiutawala. Hivyo Ukawa unajiamini kuwa Wao wanauwezo zaidi wa kiuongozi kuliko hii serikali ya "HAPA KASI TU" na huo ndio ukweli ulivyo.

Elewa upinzani unaojijenga kwa kutegemea kutunga hoja hao hawajakamilika kiuongozi.

Upinzani unajiamini kiuongozi huo unategemea kujijenga kimipango zaidi.

Msalimie Jesca na umuulize... AMEFIKAJE UDOM?
 
Mimi sipendi wala sitaki siasa zenye mwendelezo wa matukio lazimishi bila vision.
Kwa ujumla watanzania makini wanashindwa kuelewa muelekeo wa siasa za upinzani ndani ya nchi hii.

Sina uhakika kama wakuu wa ukawa wakiongozwa na CHADEMA kama wanaliona hili, lakini ni ukweli ulio wazi kwamba kuna ombwe kubwa la uongozi ndani na nje ya bunge letu tukufu.

Nje ya bunge ni kama hakipo ilhali ndani ya bunge ni ziro .
Nalazimika kuamini kwamba huenda Zuberi zitto kabwe na Dk wilbroad slaa ndio waliokuwa nguzo kuu ya uongozi wa chama hicho.kwani tangu viongozi hao kujiengua ndani ya CHADEMA, chama kimepwaya kama ndege yenye rubani bila kapteni.
CHADEMA imeongeza idadi kubwa ya wabunge lakini hakuna miongoni mwao anayeonekana kuwa na uwezo wa kujenga hoja kama ilivyokuwa enzi za Dk slaa na Zitto kabwe.

Upinzani bungeni una serkali kivuli bungeni,lakini imekuwa dormant. Ni kama haipo au kama ipo basi inafuata ushauri wa mtu au kundi fulani lenye malengo yake tofauti na lengo halisi la kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Mawaziri wake wamekosa uwezo na weledi wa kukusanya taarifa mbalimbali muhimu zinazovutia, zinazoweza kuitwa taarifa mbadala za baraza la Mawaziri kivuli wa kambi ya upinzani bungeni.
Badala yake Mawaziri kivuli wamebaki kutumia taarifa za matukio yaliyopita bila kutoa. .way forward, mwelekeo wa wapi sasa kama taifa tunapaswa kuelekea kisera na kisekta. Pamoja na kulalamika kwamba CCM wamepora sera zenu. Lakini mbona hamziendelezi katika hotuba mbadala zenu ili wananchi tuwaelewe na kuamini mnayoyasema?
Kwamba Server ya sera hizo mnazo?

Badala yake sasa mmebaki na na kukariri historia ya escrow, uuzwaji nyumba za serikali, bungeni live, nk.
Hakuna jipya la kuishauri serkali, au hata jipya la kuwashauri watanzania badala yake mmekuwa watu wa HARAKATI bungeni.wakati mnaelewa kabisa mnawawakilisha wapiga kura majimboni kwenu.sikatai au watanzania hawakatai msikemee au kufichua maovu yoyote ndani ya nchi yetu, huo ndio hasa wajibu wenu, Lakini changamoto hapa ni kwamba muwe mnakuwa na njia mbadala pale mnapokosoa ni vema kuwa na ubunifu wa njia au sera mbadala badala ya kugeuka wapingaji badala ya wapinzani.
Muwakumbuke wapiga kura wenu kuhusu maisha bora kule waliko miundombinu ya barabara, madawati, madawa, na hata walimu bora na sio bora walimu kama hili sakata la udom sasa hivi mnapolifanya kuwa mtaji wenu kisiasa au uklfichwaji wa sukari.

Mjipange kabla ya kukurupuka, mfano waziri kivuli mambo ya ndani anapokwenda kusoma taarifa ya uuzwaji nyumba za serikali. Wakati mnaye msemaji rasmi kambi ya upinzani bungeni wa wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano wapi na wapi?

Kwa hiyo mnapojiandaa kufanya kile mnachoamini nyinyi kama kuishitaki serikali kwa wananchi, pia mjiulize hao wananchi kweli kero yao kubwa ni ipi kati ya rushwa, ubadhirifu, elimu bora, madawa hospitali za umma,barabara, na miundombinu ya reli? ?

Au bunge live Wakati asilimia kubwa ya wananchi wenu au wapiga kura wenu wakiwa wanatumia vibatali bila umeme wa kuangalia hiyo television?

Ingawa ukweli huwa ni mchungu kuukubali mimi nimeanza kwa kuwakumbusha kwamba pamoja na bungeni live.lakini hiyo si kipaumbele cha walalahoi wa nchi hii, bali bungeni live huenda ikawa Ni mtaji zaidi kwenu kutegemea na matakwa ya wafadhili wenu ili waweze kuwaona mkitimiza kile walichowatuma live!
Ila pia muelewe karata hii ni kamari mnataka kuicheza. ...ikila kwenu hili mlitambue nikiwakumbusha mh kafulira alivyoweza kutuibulia masuala nyeti ya kutaifa Lakini akawa mzito jimboni kurudi kuwajulia kero wapiga kura. .hatimae kilichojiri Ni historia.

Najua kuna matusi yatakuja hapa ila nimetimiza wajibu wangu kama mtanzania commonmwananchi karibuni tuchangie

Sawa! Ni akili yako amaa ndivyo ulivyofundishwa kuwaza?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jesca amefikaje chuo kikuu?
Hili ndo swali sijaona majibu yake bado, watu midomo mireefu, majibu hakuna. Watuambie ilikuwaje vijana zaid ya 7000 watoto wa masikin, wakafukuzwa kama Mbwa na askar wenye silaha za moto usiku usiku, bunge la CCM likabariki na kuwafukuza UKAWA nje, wakat chuo hicho hicho kuna watu wasio na sifa mpaka leo wapo?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom