PRESHA inazidi kuongezeka kila kukicha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2015 ambapo sarakasi mbalimbali za kisiasa zinaendelea kuchezwa na wafuasi wa vyama vyote bila kujali chama tawala au vyama vya upinzani.
Macho na masikio ya wengi, yameelekezwa kwenye muungano wa vyama vinne vya kisiasa vya upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR Mageuzi na NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Dar es Salaam , Mwenyekiti Mwenza wa Umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba alisema, wanashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kama Ukawa na watasimamisha mgombea mmoja maeneo yote ya nchi.
Lipumba alisema kwa kuzingatia jinsi Wajumbe wa CCM wa Bunge Maalumu la Katiba walivyochakachua upigaji kura, hivyo kikiendelea kubaki madarakani hakutakuwa na Katiba ya Wananchi, ambapo wameungana ili kuhakikisha inapatikana.
Alieleza kuwa lengo kuu la muungano huu ni kuing'oa CCM madarakani, ili ipatikane Serikali yenye maslahi na wananchi, hivyo wapo tayari kuungana na asasi zisizo za kiserikali, viongozi wa dini, asasi za kiraia kuhakikisha lengo la kupata Katiba iliyosimamia maoni ya wananchi inapatikana.
JInsi muda unavyokwenda wananchi wamekua wakitoa maoni tofauti kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mwezi october ambapo inaonyesha watu wengi wanataka mabadiliko makubwa ambayo hayajawai tokea tokea nchi imepata uhuru mwaka 1961.
AJIRA kwa vijana imekuwa tabu ndio maana wengi waliotoa maoni wanapendekeza umoja vya vyama vya siasa UKAWA kupata nafasi ya kuongoza nchi ili kuona kama wanaweza kuleta mabadiliko kwa kipindi hicho cha miaka mitano
RUSHWA NA UFISADI. rushwa na ufisdi uliokidhiri umefanya wananchi wengi kutokuwa na imani na serikali ya chama tawala kwa sera ya kulindana.
Vijana nao wamefunguka wakati baadhi ya wazee wamesema enzi za Mwalimu rushwa na magendo ilkuwa ni adui wa demokrasia na uhai wa chama kipindi hicho.Lakini sasa hivi ni kama jambo la kawaida kwa maana ukila rushwa unasifiwa na kusafishwa.
Walienda mbali zaidi na kusema kuwa mwaka 2010 upinzani ambao ulikuwa ujaungana ulipata 39% ya kura zilizopigwa
kwa mara ya kwanza haijawai tokea kwa vyama upinzanzi kupata asilimia nyingi namna hiyo ila wananchi wamechoka hali ngumu ya maisha kwa hiyo wanatafuta mbadala wa chama tawala pia hayo matokeo yameonekana kwenye chaguzi za serikali za mtaa mwaka jana hamasa ilkuwa kubwa sana na watu wengi walijitokeza kupiga kura ata zile zilikuwa ngome za ccm vyama vya upinzani viliweza kupenyeza na kuibuka na ushindi.
Kwahiyo hali ya kisiasa ndani ya umoaja wao inaonekana inatoa matumaini ya ushindi mwezi octoba kwa kuibuka na ushindi wa asilimia 56% ambazo zitatosha kuunda serikali ya umoja wao na inakadiriwa kupata wabunge 176 kama hali ikiendela kama sasa hivi na uandikishaji ukafikia asilimia mia moja.