UKAWA kurudi bungeni

UKAWA kurudi bungeni

Kikwete aliwaambia hata mkisusa mtarudi tu mimi ndio Rais wenu.

Tulia nae amewaambia hata mkisusa mtarudi tu mimi NS wenu tena wa miaka mitano.

Na huyu mama muda sio mrufu atakua Spika kamili.
 
Nimeona wanahangaika sana. Mbatia amesimamishwa tu nikagundua kuwa kweli wanalazimishwa na Mbowe.
 
kuna watu wamewekwa na kambi zote humu wanalipwa pesa kwa ajili hiyo, hata usiumize kichwa zana!
Ndio maana mi nilikua sielewi kiukweli
Mfano kuna mtu anasema ukawa hawajielewi na wameshawafahamu kwa upuuzi wao. Ni sawa kabisaa na ukawa wanasema tutawashikisha adabu,
Swali je! Utamshikisha adabu ukiwa nje?

Haya kambi ya ccm nayo haioni jinsi wabunge wa CCM wanavyotunyima raha wanainchi wameligeuza bunge kama kikao cha kitchen party, kama imefikia hatua mtu anachangia kwa kutaja ratiba ya familia yaje na kujipongeza kupata mtoto na jina atakalompa, hilo balo watu wanashangilia na kupiga makofi anashindwa jua kua wanainchi wao wakoje?? Mtu wa CCM atakwambia tunawakomesha UKAWA


Hizi kambi mbili zimetukosesha uelekeo kiukweli japo kila pande inasema nyingibe haijiewi na wanainchi huku wanadai hawaelewi sio CCM sio UKAWA.


Kwa mwendo huu taifa leti maendeleo yake yatabaki majukwaani na kwenye dayare za wagombea.

Mtugawe wakayi wa kampeni sasa mnatugawa mpaka nyakati za utendaji??

Hapa tunahitaji maombi ya pande zote tatu kwa waislam, wakristo na wapagani.

Kama kutipoteza kwa maslahi yenu kiukweli mmefanikiwa, lakini naamini machozi yetu Mungu anayaona na mtayalipa mwisho wa siku.

Wewe unayejiita mwana UKAWA unaishiia kuutetea ukawa wako ukasahau mawazo na matatizo ya wanainchi yaliyoshindwa kutekelezeka kwa wawakilishi wao kutoyawakilisha na wewe unatetea kwa maslahi yako ki ukweli hiyo dhambi itakutafuna wewe na vizazi vyako.

Wewe unayejiita mwana CCM unayetetea kila upuuzi pale unapoambiwa na aliyekulushia kifurushi cha internet ukakubali kuuficha ukweli wa mamilioni ya watanzania na kuamua kuunga mkono kila wazo ili mradi tu kalito mwana ccm yako, walahi nakuapia machozi ya wanyonge wanaishi hata kwa chini ya mlo mmoja yatakutafuna na utayalipa.


Kwa nyoote mliovibarua vya ukawa na ccm mjue mmesomeshwa na wazazi wenu wengi historia zenu mnazifahamu wenyewe ili mzikwamue familia zenu na kutengeneza taifa bora kwa kutumia ujuzi wenu kulijenga taifa kwa nguvu na akili mlizopewa, sasa mnazitumia akili na ujuzi wenu kwa kutetea vyama vyenu mnachangia kuligawa taifa lenye umoja kwa vyama vyenu walahi tukibaki nyuma kimaendeleo kwa Mungu mtawajibika


OMBI

Kwa wale ambao hatupo kambi yoyote tunaogemea kwenye ukweli, tuzidi kulipgania taifa hili mi naamini ipo siku tutafika mbali kuliko kukalia majungu
 
Kama kweli wanarudi kwaajili ya jambo moja tu, basi maswali mengi yataibuka katika vichwa vya wenye kufikiri kwa kina!!
 
Acheni taarabu zenu za kujifariji na vijigazeti vyenu uchwara,

Haya leo wametoka tena leteni story zingine.
 
Kama wabunge wanajadili majina ya watoto wao hiyo ina maslai gan kwa wanannchi warudi wakaokoe jahaz
Kweli njaa mbaya, nimeamini. Hatutarudi bungeni kama Dr Tulia Acksoni anaendesha vikao kauli ya MWENYEKITI WA KUDUMU. Kwa Magu kila goti litapigwa hakuna pesa ya bure
 
huu ni upumbaf na ulofa tuu. hakuna hoja hapa sema njaa tu imewakamata. wanatafuta gia ya kuingilia mjengoni. katika sakata hili kiukweli wamechemsha. wote wanaonekana wana akili za kitoto

kweli kabisa mkuu
 
...Silinde amesema kitakachowarudisha bungeni ni kwenda kujadili masuala yanayohusu maslahi ya taifa na siyo vinginevyo. Mojawapo ya masuala hayo amesema ni lile la sakata la Lugumi.

Wacha wakaokoe jahazi, wabunge wa CCM wanajadili bajeti kama huyu:

Mbunge Mary Chatanda ametaka katiba ibadilishwe ili vyama vya upinzani visiruhusiwe kufanya mikutano ya hadhara kama ilivyo baadhi ya nchi nyingine ili kuachia serikali kutekeleza ilani yake
 
UKAWA wanataka kutuambia kuwa yanayojadiliwa kwa sasa wakiwa nje ya bunge hayana maslahi ya kitaifa!

Kwa hiyo UKAWA wanataka tuamini kuwa mijadala kuhusu bajeti haina maslahi ya kitaifa!

UKAWA wanataka tuamini vipindi vya maswali na majibu bungeni havina maslahi ya taifa!

Kigezo/vigezo gani vinatumika katika kufahamu kama ni mjadala wa kitaifa au la?

Katiba ya Tanzania inatuambia kila mjadala bungeni unahusu maslahi ya kitaifa kama ambavyo Katiba ya Tanzania 1977 imeainisha katika Ibara ya 63(1-3) kuhusu madaraka ya Bunge.

Ninaamini hii siyo sababu ya msingi itakayowafanya kurudi bungeni.
jibu lako lipigie mstari.pumba tupu.

swissme
 
Kwanza hata wakirudi hawapo kwenye orodha ya wachangiaji wataenda kulala tu bungeni.
Unafikiri wabunge wanaolala bungeni husababishwa na kukosa nafasi ya kuchangia? Sababu kuu ya kulala bungeni ni uwezo mdogo wa kuelewa kile kinachojadiliwa bungeni hususani "budget". Hawa wanaolala bungeni ni wale waliozoea kusoma magazeti ya udaku, walikuwa wanalala hata walipokuwa shuleni.
 
Acheni taarabu zenu za kujifariji na vijigazeti vyenu uchwara,

Haya leo wametoka tena leteni story zingine.
Kutoka leo bungeni haina maana kuwa hawawezi kuingia tena bungeni.

Haya ni mahojiano na Mbunge Silinde.

Kama magazeti yametengeneza habari, Silinde atakanusha.
 
Back
Top Bottom