UKAWA kuitikisa Zanzibar leo

UKAWA kuitikisa Zanzibar leo

Ndugu zangu UKAWA kwa heshima mlioipata kwa wa Tz wenyeuelewa tunawaombeni sana timizeni malengo yenu kwani wachamungu tunaamini kuwa jambo hili lina mkono wa Mungu.mtapingwa sana kwani hii ndiyo historia ya dunia naomba mkumbuke kuwa hata bwana wetu Yesu kristo alikfa msalabani ili tupate wokovu nanyi leo hii mmebeba msalaba huu ili taifa hili likombolewe.lakini mtambue kuwa binadamu tumeumbwa kukanusha ukweli uwe uongo.ukisoma maandiko ya bibilia yanatuonesha kuwa hata baada ya bwana Yesu kufufuka wapo watu walioamua kukanusha huku wakisema amebiwa na wanafunzi wake hajafufuka mpaka pale alipo watokea wanafunzi wake hivyo mimi nawatia sheme msirudi nyuma tena ukombozi unakaribia.
 
  • Thanks
Reactions: jme
Sijui kituo gani cha runinga kitakuwa hewani moja kwa moja kutoka kibanda maiti....
 
Mkuu Yericko,ben,mungi ivi haiwekani ITV wakombwa kurusha moja kwa moja kutoka kibandamaiti ili hoja zitakazotolewa ziwafikie wantanzania moja kwa moja ili itapoanza operation za maeneo mengine wananchi wawe na uwelewa ili wahadhina wasije wakaanza kujenga vijembe vyao?
 
!
!
ningeomba pia watu watakaohudhuria huko mtuletee kinachojiri kwa maana ya picha na maelezo. Anzisheni uzi wa kinachojiri huko. Lakini pia ongezeni umakini kwani sisiem wanaweza pandikiza fujo ili mkutano uvurugike na mpigwe na ffu.
Ningependa kujua pia kama Mh Jussa na Mh Lisu watahutubia.
Ombi maalumu kwa mtakaohudhuria ni kuchukua maoni ya Mchungaji Mtikila.
Saa ya ukombozi ni sasa.
Tanganyika's redemption
 
  • Thanks
Reactions: jme
Dar es Salaam. Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.

Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19, mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo walishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya Sikukuu ya Pasaka.

Hata Aprili 23 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwa mkutano huo, ilikataliwa na polisi kwa madai kwamba askari na maofisa wa jeshi hilo walikuwa Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yaliyofanyika Aprili 26, mwaka huu.

Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina amethibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano.

“Tumewaruhusu kufanya mkutano huo lakini maandamano hayataruhusiwa kufanyika,” alisema Mhina.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaoanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, utahudhuriwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa wa Chadema, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.

Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wawakilishi 10 kutoka kundi la 201 na wanachama mbalimbali kutoka umoja huo.

“Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni,” alisema Mtatiro na kuongeza:

“Kesho (leo) tunafanya mkutano Unguja na keshokutwa (kesho) Pemba na tutatoa ratiba ya mikutano mbalimbali itakayofanyika Tanzania Bara kwa makundi tofauti.” Aprili 16 mwaka huu, Ukawa wakiongozwa na Profesa Lipumba walisusia Bunge la Katiba na kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mienendo ya mjadala ya Bunge hilo.

Baada ya kutoka bungeni, walitangaza kufanya mikutano nchi nzima wakianzia Zanzibar.

chanzo Mwananchi

Je pana kituo gani cha TV kitakachoonesha mkutano huo moja kwa moja?
 
Sasa UKAWA leo tunataka mpigilie misumali kweli kweli sio manalalamika tu..tupeni plan B na nini tufanye
 
Wakumbuke kuzipeleka hadi kwenye mashina yao ya vijjjini, zisiishie tu kwenye mifuko ya Mbowe na Lipumb* plus huyo mpenda kesi Mtikila!
 
tunashukuru sana kwa hiyo link, natumaini mda ukifika itakuwa hewani bila shida
 
Safi sana mkuu! tunatega masikio kuhabarishwa maneno ya kizalendo.
 
Mkuu Yericko,ben,mungi
ivi haiwekani ITV wakombwa kurusha moja kwa moja kutoka kibandamaiti
ili hoja zitakazotolewa ziwafikie wantanzania moja kwa moja ili
itapoanza operation za maeneo mengine wananchi wawe na uwelewa ili
wahadhina wasije wakaanza kujenga vijembe vyao?

Wel said mkuu, Tena watuambie gharama za kurusha live huo mkutano kupitia Television ya wananchi ITV ni sh. ngapi na watuwekee A/c No. pamoja na Mpesa, Tigo pesa, Airtel money ili tuanze kuchangia.
 
  • Thanks
Reactions: jme
Back
Top Bottom