UKAWA kuitikisa Zanzibar leo

UKAWA kuitikisa Zanzibar leo

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
4,773
Reaction score
5,125
Dar es Salaam. Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.

Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19, mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo walishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya Sikukuu ya Pasaka.

Hata Aprili 23 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwa mkutano huo, ilikataliwa na polisi kwa madai kwamba askari na maofisa wa jeshi hilo walikuwa Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yaliyofanyika Aprili 26, mwaka huu.

Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina amethibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano.

"Tumewaruhusu kufanya mkutano huo lakini maandamano hayataruhusiwa kufanyika," alisema Mhina.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaoanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, utahudhuriwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa wa Chadema, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.

Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wawakilishi 10 kutoka kundi la 201 na wanachama mbalimbali kutoka umoja huo.

"Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni," alisema Mtatiro na kuongeza:

"Kesho (leo) tunafanya mkutano Unguja na keshokutwa (kesho) Pemba na tutatoa ratiba ya mikutano mbalimbali itakayofanyika Tanzania Bara kwa makundi tofauti." Aprili 16 mwaka huu, Ukawa wakiongozwa na Profesa Lipumba walisusia Bunge la Katiba na kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mienendo ya mjadala ya Bunge hilo.

Baada ya kutoka bungeni, walitangaza kufanya mikutano nchi nzima wakianzia Zanzibar.

chanzo:Mwananchi

-------------------------------------------------------------------

Matangazo ya moja kwa moja bonyeza hapa
 
Dar es Salaam. Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.

Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19, mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo walishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya Sikukuu ya Pasaka.

Hata Aprili 23 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwa mkutano huo, ilikataliwa na polisi kwa madai kwamba askari na maofisa wa jeshi hilo walikuwa Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yaliyofanyika Aprili 26, mwaka huu.

Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina amethibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano.

“Tumewaruhusu kufanya mkutano huo lakini maandamano hayataruhusiwa kufanyika,” alisema Mhina.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaoanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, utahudhuriwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa wa Chadema, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.

Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wawakilishi 10 kutoka kundi la 201 na wanachama mbalimbali kutoka umoja huo.

“Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni,” alisema Mtatiro na kuongeza:

“Kesho (leo) tunafanya mkutano Unguja na keshokutwa (kesho) Pemba na tutatoa ratiba ya mikutano mbalimbali itakayofanyika Tanzania Bara kwa makundi tofauti.” Aprili 16 mwaka huu, Ukawa wakiongozwa na Profesa Lipumba walisusia Bunge la Katiba na kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mienendo ya mjadala ya Bunge hilo.

Baada ya kutoka bungeni, walitangaza kufanya mikutano nchi nzima wakianzia Zanzibar.

chanzo Mwananchi

It's about time to pull the bull by its horns now!Good luck UKAWA.We are right behind you!!!!
 
Hongereni makamanda. No retreat no surrender. But tahadhari zichukuliwe dhidi ya hao mainterahamwe maana hawakawii kutega mabomu
 
Na unaweza kuta mwigulu kesha ratibu mlipuko halafu kakimbilia ughaibuni kupoteza boya
.
 
Hii ni habari njema sana. Wananchi tuko nyuma yenu.nawashukuru sana ukawa kwa uvumilivu wenu hii imeonesha ukomavu wa kisiasa na nia njema kwa wananchi juu ya katiba yao.Mungu awabariki.
 
Nawatakia Mkutano mwema Ukawa na Mungu awalinde.Shetani asipate nafasi ya kuja kuharibu hapo pakatokea vurugu.
 
Naona B7 wamepata kigugumizi baada ya kuona mirija yao inaanza kusinyaa
 
Wakuu hii itakuwa ni turufu ya hali ya juu kwanza ukawa wamekuwa wavulimilivu na kukubali kuhairisha mikutano inaonesha ni jinsi gan wako makini katika swala hili kwa kweli sisi wantanzania wote inabidi tuwauunge mkono
 
Mtu ukijipanga raha sana, maccm walijua UKAWA watapagawa baada ya kuzuiwa mara mbili kufanya mikutano hivyo walitegemea UKAWA wangefanya mikutano kinguvu ili wapate kusema hawa ni watu wa fujo na mambo kama hayo.

Nimewakubali sana UKAWA sasa huo ni msiba live kwa maintarehamwe zile hoja zao zote kunzia za jeshi kuwatisha UKAWA zilizotolewa na dhaifu zitajibiwa kirahisi sana Long Live UKAWA

BACK TANGANYIKA
 
Katika suala la kusimamia haki zao Wa Zanzibar ninawaamini sana. Hawana tabia za ukigeugeu hata kidogo. Pia hawadanganyiki kama ndugu zangu wa bara tulivyo. Big up ukawa

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Back
Top Bottom