Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
Napenda kutumia fursa hii kuwataarifu wapenda mabadiliko kuwa Jimbo LA Namtumbo lipo hatarini kupotea hivyo msaada Wa haraka unahitajika ili kuokoa jimbo lisipotee. UKAWA iliwapa jimbo hili CUF ila mtandao wa cuf ni mdogo na mgombea wao hakubaliki Kwa wapiga kura walio wengi.
Mgombea Ubunge wa CUF hakuwahi kufanya siasa katika jimbo hili hivyo inamuwia vigumu kupokelewa na wapiga kura wakati huu Wa kuomba kura. Hali ya sintofaham ilitokea Jana katika Kata ya Lusewa na Msisima ambapo mgombea huyo alifukuzwa na wapigakura wakisema wao hawamtambua wanamtambua mgombea wa Chadema Wa udiwani na Ubunge.
Tuwakumbushe viongozi Wa UKAWA kuwa kura ni hiari ya MTU. Huwezi lazimisha mtu atoe kura Kwa mgombea asiyemtaka. Kuendelea kulazimisha wananchi wamchague mmgombea wasiyemkubali ni kutafuta kupoteza kura za madiwani na za rais wetu NA hatimaye kuhatarisha ushindi wetu Kama UKAWA.
Nionavyo Mimi Kama ni lazma huyu mgombea awe mbunge basi mpeni Ubunge Wa kuteuliwa. Huu Ubunge Wa kugombea ni lazma MTU aaminike NA kukubalika katika jamii ya wapiga kura.
Kuendelea kupingana NA maamuzi ya wapiga kura ni dalili kuwa mgombea Wa cuf na cuf huku Namtumbo wapo Kwa ajili ya maslahi binafsi na sio maslah ya wapiga kura ambao mgombea Ubunge anataka kuwapigania. Kama kwel UKAWA na mgombea Ubunge Wa Cuf wanawapenda wananchi Wa Namtumbo na wanataka wasiwe chini ya Ccm basi kubalini hamuwezi kuzuia mafuriko Kwa mikono. Mpeni nafasi hiyo mgombea anaye kubalika na wananchi walio wengi ili tushinde. Mgombea asiyekubalika hawezi kumwombea kura Diwani wala rais.
Wanajamvi mlio karibu na viongoz wa ukawa Tunaomba mtusaidie kufikisha ujumbe huu Kwa wahusika.