UKAWA hamna haja na Mainstream Media?

UKAWA hamna haja na Mainstream Media?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,860
Reaction score
50,646
Tangu zianze Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hatujaona mikutano "Live" ya UKAWA zaidi ya ule wa Uzinduzi pale Jangwani. Hatuyaoni matangazo ya maana kwenye TV na Magazeti ya kuhamasisha wale wasiohudhuria mikutanoni. Tatizo ni Gharama au siyo sehemu ya mikakati yenu??
 
Hata mimi hiki kitu kinanishangaza sana. Mpaka sasa UKAWA/CHADEMA haijatumia vizuri media kufanya kampeni. Redio na TV ni vyombo vinavyowafikia watu wengi sana kwa wakati mmoja.
Sasa kwa nini wahaweki hata clip ya dakika moja au mbili kwenye redio na TV?
Wapiga kura wengi hawaendi kwenye mikutano hivyo wanapata information kupitia media.

Wengi wa wananchi hawana TV wala mitandao ya internet. Wanategemea zaidi redio.
 
Wachukuwe hatua na kulifanyia kazi ndani wiki hizi mbili zilizobaki.
 
Kweli walau ile ya kuomba kura waweke kiclip radio one
 
Km ipoipo tu ccm wamenunua media zote. Mpaka mabango tukibandika wanatoa. Wamezuia viwanja vyote vikubwa wanatumia wao kwa kusomba watu kwa magari na kugawa T-shirt na kofia .Lakini UKAWA popote watu wapo wanajitoa wenye. MUNGU AKIWA UPANDE WETU NANI ATAKUWA JUU YETU
 
Back
Top Bottom