NEC lazima muelewe kwamba hii Tanzania ya leo sio ya malofa kama watuitavyo wengine.Tanzania ya leo kila mtu anaiwezo wa kuchuja na kutathmini mambo.
Hivyo basi tumesubiri sana inatosha sasa toeni tamko juu ya haya matatu kwa magufuli ili kulinda heshima yenu kama mlivyofanya kwa kosa la mära moja alilofanya ndugu Lowassa
Kwanza: siku ya uzinduzi wa kampeni za CCM mgombea alizidisha muda hadi leo mko kimya,
Pili: Mgombea huyo huyo akiwa Morogoro alizidisha muda bado mko kimya!
Tatu: Mgombea Magufuli amehonga pesa hadharani kule Tanga! Sasa tunaomba tamko.
Hivyo basi tumesubiri sana inatosha sasa toeni tamko juu ya haya matatu kwa magufuli ili kulinda heshima yenu kama mlivyofanya kwa kosa la mära moja alilofanya ndugu Lowassa
Kwanza: siku ya uzinduzi wa kampeni za CCM mgombea alizidisha muda hadi leo mko kimya,
Pili: Mgombea huyo huyo akiwa Morogoro alizidisha muda bado mko kimya!
Tatu: Mgombea Magufuli amehonga pesa hadharani kule Tanga! Sasa tunaomba tamko.
Wana JF,
Naomba nichukue fursa hii kuwakumbusha UKAWA/CHADEMA kuhusu hatari inayowakabili hapo mbeleni wasipochukua hatua sasa. UKAWA/CHADEMA msidhani kuna mtu au Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawajali, na itaeweza kuchukua hatua iwapo hakutakuwa na shinikizo kutoka kwenu. Pia lazima mjue kwamba CCM inatumia kila njia na itatumia kila njia ili kuhakikisha kwamba inabakia madarakani. Lakini njama zao zitashindwa tu iwapo na nyie UKAWA mtakuwa serious kufuatilia haya mambo. Mimi kama mtanzania na mpenda nchi yangu naomba nitoe tahadhari kwa UKAWA/CHADEMA kuhusu impact ya haya mambo ambayo yawezekana kwa kujua au kutojua wanayapuuzia bila kujua kwamba yana spillover effects kubwa sana kwa wananchi wa kawaida hasa kadri siku zinavyokaribia uchaguzi mkuu hapo Oktoba 25.
Mambo hayo yanayohitaji hatua za haraka ni kama yafuatvyo (ziko kwenye number kulingana na uzito wake):
1. Kitendo cha Magufuli kurudia rudia kwenye mikutano yake mifano ya Libya, Iraq, Misri, n.k, imelenga hasa kuwaogofya wananchi ili wasichague chama chochote nje ya CCM kwenye uchaguzi mkuu. Nawaomba UKAWA/CHADEMA msidhani kwamba wananchi wote hasa wanaokaa maeneo ya vijijini wako well informed kuhusu hiyo mifano ambayo CCM na hasa mgombea wake amekuwa akitumia katika mikutano yake mbalimbali. CCM wanaelewa fika kwamba mtaji wao mkubwa ni watu wa vijijini ambao wengi wao hawana elimu ya kutosha katika mambo mengi. Na mkumbuke kwamba, hawa ndio wapiga kura wa kutosha. Kwa msingi huo, hawa wananchi wanapojazwa UOGA huu na CCM, matokeo yake wataacha kuwachagua UKAWA na wagombea wake, kwani tayari wakishaambiwa na CCM habari za kuogofya na za kutisha huku UKAWA wakiendelea kukaa kimya katika hili. Kwanza mnapaswa kuongea na waandishi wa habari kuhusu impact ya hivyi vitisho kwa wananchi, lakini ni pia mpate maelezo kutoka NEC kuhusu hizi kauli za Magufuli na timu yake kuhusu mambo ya Libya, Iraq, na hata Misri. Kumbuka, magufuli ametumia hii kauli alipokuwa nyanda za juu kusini, majuzi Morogoro na hata jana Tanga.
Na katika kulitekeleza hili na baada ya kuona UKAWA wako kimya katika hili, jana pia katika mkutano wa kampeni ya CCM kule Bukoba uliohudhuriwa na Benjamin Mkapa, kulikuwa na mama mmoja anahutubia pia ule mkutano na kutoa vitisho kwa wananchi kwa kutoa mifano ya maiti iliyokuwa inaeleaelea kama matokeo ya uchaguzi wa nchi jirani ya Burundi (Naomba mwenye clip ya ule mkutano aweke hapa ili muweze kuuona, kwani mimi niliona kwenye Azam Two taarifa ya habari ya saa 2 usiku). Hii mifano yote imelenga katika kuwajengea hofu wananchi, hasa wale wa kawaida ambao hawana uelewa mkubwa ya mambo na matokeo yake yanajenga chuki katika jamii. Kwa msingi huo, UKAWA ni lazima muamke na mchukue hatua sasa, vinginevyo mkiendelea kukaa na kudhani kwamba NEC au mtu yeyote atawaonea huruma, basi mjue mmekwisha.
Katika hili, niwaombe pia wanaharakati za haki za binadamu pia kuliongelea, kwani inaweza kutufikisha pabaya kama taifa.
2. Jambo la pili ambalo ni la mwisho ni la muda wa mikutano. Hili mliliona pale Jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM na hata majuzi kwenye kampeni kule Morogoro. Mikutano ya CCM na mgombea wao wamezidisha muda wa mikutano na mpaka sasa hakuna onyo lolote toka NEC na mbaya zaidi Lema wa CHADEMA alipozidisha dakika 6 tu, aliswekwa Lupango na kulala na hata sasa ana kesi ya kujibu. UKAWA wameendelea kukaa kimya wakidhani NEC itawonea huruma! Nawapa pole zenu, kwani msipochukua hatua sasa basi msahau ushindi wa kishindo. Ni vema mkahitaji majibu ya NEC ni kwanini hayo yanakubaliwa CCM na kwa wengine ni NO.
3. Naomba sasa niwaulize swali UKAWA, hivi mmeshajiulza ni kwanini Katibu mkuu mstaafu Yusuf Makamba amerudishwa kwenye ulingo wa siasa pamoja na kwamba hakuwa katika ile listi ya watu 32 wanaomkampenia Magufuli??? Je, mmewahi kujiuliza ni kwanini kwasasa imekuwa kawaida kwa CCM kutoa mifano ya kuogofya na kuwatisha wananchi (rejea no 1 hapo juu) kwenye mikutano yao??? Je, hamuwezi kuona au kuhisi kwamba kuna kitu kinaandaliwa kadri tunavyokaribia uchaguzi (rejea chaguzi mbili zilizopita CUF 2005 na CHADEMA 2010)???
Ushauri wangu kwa UKAWA/CHADEMA:
Chukueni hatua stahiki sasa badala ya kukaa mkisubiri huruma ya NEC , CCM , na wananchi; kwani msipochukua hatua sasa, mtakuja kujikuta mmefungiwa mlango wa Safina nje (rejea habari ya Nuhu kwenye Maandiko Matakatifu).
Mbarikiwe sana.
Jatelo.