UKAWA,anzeni na Serikali za mitaa

UKAWA,anzeni na Serikali za mitaa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Lile lengo lenu la kusimamisha wagombea wa pamoja anzieni kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa. Chaguzi hizo zitakazofanyika mwaka huu si za kuzipuuza.Ni muhimu sana. Zinatoa dira na kuonesha hila za kupambana nazo mwakani. Sisi CCM tumeshamaliza maandalizi.Tumeshaandikisha tunavyovitaka na kwa idadi tuitakayo. Baada ya Rasimu unafuata msimu adimu na muhimu.

UKAWA, mkichelewa mtakuta mtoto si wenu. Nawashauri tu kama wapinzani wetu wa jadi bila kadi maridadi. Sikieni na muufanyie kazi ushauri wangu huu tu: chaguzi za Serikali za Mitaa ni muhimu kidira na kisera. Mkishangaa tutapita bila kupingwa na kibingwa bila kufungwa.Kumbukueni kuwa hata mbuyu huanza kama mchicha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Tupa tupa ahsante kwa taarifa, tupo sawa ukizingatia gia ya katiba waliyo ichakachua wameumia.
 
Mzee tupatupa bwana.... mie napenda sana mabandiko yako mzee
 
Lile lengo lenu la kusimamisha wagombea wa pamoja anzieni kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa. Chaguzi hizo zitakazofanyika mwaka huu si za kuzipuuza.Ni muhimu sana. Zinatoa dira na kuonesha hila za kupambana nazo mwakani. Sisi CCM tumeshamaliza maandalizi.Tumeshaandikisha tunavyovitaka na kwa idadi tuitakayo. Baada ya Rasimu unafuata msimu adimu na muhimu.

UKAWA, mkichelewa mtakuta mtoto si wenu. Nawashauri tu kama wapinzani wetu wa jadi bila kadi maridadi. Sikieni na muufanyie kazi ushauri wangu huu tu: chaguzi za Serikali za Mitaa ni muhimu kidira na kisera. Mkishangaa tutapita bila kupingwa na kibingwa bila kufungwa.Kumbukueni kuwa hata mbuyu huanza kama mchicha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Ushauri n mzuri sana. Hakuna maandalizi so far yaliyofanyika kwa upinzani. Sioni pia namna ya kushinda uchaguzi huo Desemba. Sisi upinzani tumekosa mbinu. CCM nyie mna mbinu nyingi za kushinda uchaguzi. Hadi sasa hatuna wagombea wa uhakika.
 
Tunasikitika sana sisi upinzani kwa kutanguliza matumbo mbele na kuvurugwa na kirusi cha ubaguzi.Sisi wapinzani kwa sasa hatujajiandaa kabisa tunaomba nyie CCM endeleeni kutuongoza maana nyie ndo mna dira na maono kwa maslahi ya watanzania.
Sisi upinzani siku tukiwatoa hawa waliojifanyia chama chetu km SACCOS na kuwaweza viongozi dhabiti na wazakendo ndo tutaanza kupambana na nyie CCM.
Kila la kheri mzee tupa tupa na Mungu awaongoze katika chama chenu.
Kidumu cha cha mzee tupa tupa na ife UKAWA
 
Back
Top Bottom