UKAWA Aibu! Tena Makonda umedhihirisha: Meya wa Kinondoni Umechemka Sana Mzee

Umechukizwa kwa hiyo kila anachofanya makonda ni sawa mnamsifia, akifanya mayor wa chadema mnaponda Hata kama ni kizur . Think twice acha kukurupuka.

Nimechukia kukaa kwenye TV nakuongea kitu cha kupotosha watu. huku talaamua na sheria ipo tofauti.
 
huyo mkandarasi unajua anaitwa nani,somebody Mushi hapo ndio utajua kwanini meya anamtetea.Kwa mtu unayejali kazi yako huwezi kujenga chini ya kiwango sababu ya michoro huu ni utetezi wa kijinga
 
Kila tenda ya makandarasi unayoiona inakuwa na wahusika wa 20% ambao hupeana cintract kwa kufahamiana wewe hata kama ni mkandarasi mtaalamu unawekwa pembeni wenye pesa wanapeta.
 
Makonda amenifurahisha alipo deal pia na wahandisi wa manispaa. Inaonesha hawa wahandisi wa manispaa na wakandarasi walikuwa na kolabo ya ubadhirifu.

Kudos Makonda.
 
Hasira brother mimi sipendi hii kitu ya siasa hewa
Hujapenda kuumbuliwa kwa makonda au? Kwani si ni kweli barabara hizo zilijengwa yeye akiwa mkuu wa wilaya? Kosa la meya liko wapi kama wasimamizi walipiga pesa na kupokea barabara mbovu? Mbona ile kilwa road ilijengwa chini ya kiwango na msimamizi wa wizara ndio huyu huyu mtumbuaji na hajajitumbua hadi leo? Meya usirudi nyuma, fukua kila kona kuutafuta uchafu ili hao wanaojifanya wasafi tuwaone usafi wao.
 
Mimi nimechukizwa na kile kitu bwana nimeandika kutokana na hasira tu. Siasa hizi zilikuwa za awamu ya nne ni muda sasa wakuwa na wisdom so kwenda kusoma kitu usiku na kutolea tamko. wazungu wanatucheka sipendagi mambo hii
Wazungu ungerezani wamepiga kura kujiondoa EU, ndio unaowasifia!! hujagundua kuwa kichwa chako kimebeba ubongo wa mtu mwingine???
 
Ninavyojua mkandarasi anajenga kulingana na mchoro, kama unajenga daraja la miti kwa kuwa mchoro unaonyesha hivyo na atajenga la zege kwa kuwa mchoro unaonyesha hivyo, sasa tatizo kwenye vyombo vya habari viongozi hutangaza barabara itatumia 8 billions lakini nyuma ya pazia mkandarasi kapewa 4 billions na atakachotakiwa kufanya ni kujenga barabara inayofanana kwa muonekano kama ulivyo kwenye mchoro lakini kwenye ubora ulingane na 4 billions, na unakuta barabara inakabidhiwa na serikali inakubali kwa kuwa hawa wanaokabidhiwa ndiyo waliokula hela ya hiyo barabara sasa hapo mkandarasi anakosa gani?, mfano hai ni club zetu za mpira huwa wanatangaza wanamlipa mchezaji fulani 5 millions lakini ukweli jamaa analipwa 1.5 millions lakini mashabiki na watz wanaamini analipwa mshahara wa 5 millions, hakuna mtu ambaye akupe pesa ya kununulia ngamia halafu umletee panya akakuelewa lazima muagizaji alitoa pesa ya panya na siyo ya ngamia
 
Hii tu pekee imenifanya nitilie mashaka uelewa wako, kiasi cha kupuuzia yote uliyoandika. Unasema makandarasi wanasoma 'Engineer drawings' na 'Environmental Engineering'? Hivi hawa makandarasi, mbona ni wafanyabiashara tu wenye mitaji? Ngoja nikae kimya kwanza, labda nitajua humu chuo kinachowafundisha makandarasi
Mpekuzi ni kweli kampuni za makandarasi ni wengi wafanyabiashara. Lakini wanatakiwa waajiri wasomi wanaoijua kazi hiyo
 
Shida yangu unapojenga mchoro tofatuti sehemu tofatuti si tatizo la mchoraji ni tatizo la mjenzi hiii imekaaa kitaluma na kisheria zaidi. Na egineer waaaaa mkandarasi ndio wa kushitakiwa wa kwanza
So hivyo tu Pascal, uko sahihi, Katika ujenzi kuna vikao vya kitaalam kila mwezi kati ya Mjenzi, Engineers, na client kuangalia changamoto na maendeleo ya ujenzi, wataalam hueleza kasoro, ongezeko la gharama na the likes. Mjenzi huwezi weka nondo mbili ktk mazingira uliyokuta yanagitaji nondi sita. Mchori kitu kimoja, mazingira halisi ya site kitu kingine unayoa ushauri.
 
Nimechukia kukaa kwenye TV nakuongea kitu cha kupotosha watu. huku talaamua na sheria ipo tofauti.
Mkuu wakati mwingine uwe unaangalia vya kuponda ili ufanikiwe kwa lile unalotaka.. Ila kwa habari hii umechemka big time..! Meya alizungumza baada ya vikao vilivyowajumuisha wahusika wote (pamoja na Makonda mwenyewe) na kugundua tatizo lilianzia kwa wahandisi wa manispaa kushindwa kutoa maelezo ya kina juu ya barabara inavyotakiwa kujengwa na hali halisi ya eneo husika.. Na ndo maana mwisho wa siku hata Makonda mwenyewe amekubaliana na madiwani..

Uwe unafanya research Mkuu..
 
Hii tu pekee imenifanya nitilie mashaka uelewa wako, kiasi cha kupuuzia yote uliyoandika. Unasema makandarasi wanasoma 'Engineer drawings' na 'Environmental Engineering'? Hivi hawa makandarasi, mbona ni wafanyabiashara tu wenye mitaji? Ngoja nikae kimya kwanza, labda nitajua humu chuo kinachowafundisha makandarasi

Ufahamu wake kwenye " construction industry" ndipo ulipoishia
 
Kwenye ujenzi kuna wati wawili
1. Consultant ambapo kwa kazi za manispaa Engineer wa manispaa ndio consultant na yeye ndie anaye sema kila kitu kinacho takiwa kufanywa.

2. CONTRACT ambaye ndiye anayefanya kazi za ujenzi.

Kwa kesi ya makonda nadhani amechemka kwa sababu kiutendaji aliye takiwa kuwajibishwa ni engineer wa mkoa. Mkandarasi anafuata maelekezo ya mhandisi.

Hata barabara ya mwenge morroco mhandisi wa mkoa wa tanroad ndiye consultant.

Kwa kawaiada consultant anatakiwa kuwa ni kampuni nyingine lakini kubana matumizi ndio watu wanaweka maengineer uchwara.
 
Baada ya Mbuge mmoja kushuku uelewa wa spika sasa Mwingine tena anawatetea wasiyo na ujuzi ama wamesahau material ama wanatumia udhaifu wa mamlaka, Kujenga barabara mbovu nakutoa kisingizio cha aibu kuabisha taaluma za makandarasi.

Nimeshangaa kuona ITV Meya wa chadema anaongea kwa confidence akiwalaumu wakina Makonda kwa kuwasimamisha makandarasi wachovu huku akiangaliwa na dunia nzima kupitia Tv mbalimbali.

Hivi huyo kandarasi amesoma wapi mpaka apewe michoro na kuimini na kuanza kujenga bila kufanya tathimini ya eneo. Yaani kwa taaluma ya ujenzi hata sehemu haijawahi kupitisha maji miaka 1000 iliyopita ukisoma tabia ya eneo utajua hapa mafuriko lazima yatakuja tu.

Angeomba eneo hilo lifanyiwe upembuzi yakinifu upya kabla ajajenga . Sasa kama huyo kandarasi kama akijenga gorofa si ataua watu ama daraja ni mauaji.

Ndio maana kuna somo la engineer drawings,Environmental Engineering kwa makandarasi.

President Shule imepanda kichwani nadhani kama alikuwa anaangalia TV alicheka kidogo kimchomekeo.

uelewa mdogo sana, watia aibu agrrrrrrrrrrh!
 
Kama ndio hivyo Tegemea makubwa kutoka kwa makandarasi awamu ya 5. kufungwa na kunyang'anywa Leseni. maana Sheria inahitaji lazima kuwepo na registered engineers katika company kabla ya kujenga barabara.
Ni kama wewe hauishi Tanzania na wala siyo Mtanzania. Unachokiandika hata hukijui ila umeona ulete yale uliyokariri ambayo hayaendani na hali halisi. Pamoja na kuwepo kwa sheria unazosema za kuwataka makandarasi kuwa na registered Engineers, Lakini kwani hujui sisi watanzania tulivyomabingwa wa kudulufu vitu. Kandarasi ana mtaji wake anakuja kwangu na kwa mwingine ambaye ni registered engineer ana nipa mpunga nampa CV yangu kuonyesha kuwa anawataalamu wa fani hiyo. Ana mwaga rushwa kwa watendaji wa serikali ana pata tender wakati huo hana mtaalamu hata mmoja.
Jitahidi kuelewa vitu kabla hujaja na arguments zisizo na mashiko Mkuu. Zaidi ya hapo utaonekana mkurupukaji na kupata negative criticism watu wanaokuona hata unachoandika hukijui.
 
Jengo likianguka anakamatwa nani turudie hapo kwanza achana na kazi nani kampa kampa vipi rushwa na yote hayo hayahusu kuanguka kwa jengo Vivyohivyo kwenye barabara
Hivi jengo la serikali likijengwa bondeni halafu likasombwa na maji, atakayelaumiwa ni aliyetoa idhini ya ujenzi au aliyepata tenda ya ujenzi?
 
Kwanza umeleta mada kidada sana,pili unaongea vitu ambavyo huna uelewa navyo yani unaonekana kichwani bado ni butu..vijana msipende kufanya vitu kwa sifa ili muheshimiwa awaone na kupewa zawadi..
 
Shida yangu unapojenga mchoro tofatuti sehemu tofatuti si tatizo la mchoraji ni tatizo la mjenzi hiii imekaaa kitaluma na kisheria zaidi. Na egineer wa mkandarasi ndio wa kushitakiwa wa kwanza

Unachanganya mambo, inawezekana hujui kabisa mambo yanavyofanyika katika kuomba na kupata miradi hii, kuna consultants na contractors, consultants tunakuta ma Architects, Engineers, Quantity surveyors n.k. Hawa ndio wanahusika na feasibility study, design na preparation of tender docments, evaluation na supervision.

Mkandarasi kazi yake ni kutekeleza kilichopo kwenye michoro, kulingana na vigezo, masharti na maelekezo wanayopewa na hawa consultants, na kwenda kinyume na hapo ni kujitafutia matatizo.

Kosa liko kwa consultants kama walishindwa kukagua kazi kama zipo katika standard zao na matarajio yao, wao walitakiwa kukagua na kuthibisha

Kosa lipo kwa mkandarasi, kama alifanya kazi chini ya kiwango na hakurekebisha na kama aliwapa consultants rushwa ili apitishe kazi zao

Kosa kubwa lipo kwa hao walioipokea hiyo miradi na kuridhika nayo. Ina maana hawakuwa competent kung'amua

Kumsimamisha mkandarasi pekee ni kosa kubwa sana wakati kazi imekubaliwa na waliokuwa wanamsimamia, na kuwaacha wasimamizi na waandaaji wa huo mradi ina maana kuna uonevu unaondelea

Mkandarasi akitumia material zisizo na kiwango ujue kabisa engineer consultant karuhusu, akijenga kitu ambacho sicho ujue kabisa ndivyo alivyoambiwa ajenge,
 
Mpekuzi ni kweli kampuni za makandarasi ni wengi wafanyabiashara. Lakini wanatakiwa waajiri wasomi wanaoijua kazi hiyo
Angesema Engineer sasa, sio mkandarasi. Lakini Engineer wa mkandarasi yupo kikazi zaidi, sio kimaamuzi. Walioamua miundombinu ijengwe hapo ni mainjinia wa jiji, sasa kwa nini aadhibiwe mkandarasi wa ujenzi? Wewe umeajiri fundi, ameanza kujenga hadi kozi nne, mkeo anakuja anasema hapendi hiyo ramani ya nyumba, mnaamua kusimamisha ujenzi. Fundi atalipwa au hatalipwa kwa kazi iliyofanyika hadi pale?
 
Back
Top Bottom