Ukatili huu uliofanywa na Polisi Simiyu kwa Watoto wa shule, ni aina nyingine ya "ukaburu mamboleo"

Kweli hili linazidi kudhihirisha UKWELI wa Uislam, moja kati ya mafunzo ya Mtume Mohammad (s.a.w) amesama watakuja watu siku za baadae ambao wawo watakua ni WATU wa MOTONI watu hawa watakua na fimbo mikononi mwao za urefu kama mikia ya nyumbu KAZI zao zitukua ni KUWAPIGA WATU kwa UONEVU pasina kuangalia( mtoto wala mkubwa) basi eleweni ya kuwa makazi ya watu hawa ni JAHANAMA.
 
Duuhh nimekuelewa
 
Inavyoelekea, kuna maeneo tuna viongozi wa hovyo ambao haijawahi kutokea.

Nilipokuwa shule ya msingi miaka ya 80, darasa letu lilibomoka. Siku 2 tukakosa masomo, tuliandamana. Hatukuguswa na mtu, mpaka tukafika tulikokusudia. Tulipofika tukasoma risala yetu ndogo tuliyoiandika, ikapokelewa. Viongozi tukaitwa ofisini kwa katibu tarafa. Kwanza alitusifu kwa kujali elimu yetu. Baadaye akasema kuwa tulifanya kosa kwa sababu sheria hairuhusu kuandamana.

Tulivyotoka nje Mwalimu Mkuu akasema kwa kuwa tumefanya makosa, itabidi tuomba msamaha, tukakubali. Akutuambia ni kwa namna gani tuombe msamaha. Tukafikiria wenyewe. Tukaandika risala fupi, tukarudi ofisini kwa Katibu Tarafa, tukaomba msamaha. Wakati tunasoma risala, wenzetu walikuwa wamepiga magoti. Katibu Tarafa alitusifu kwa hatua tuliyoichukua ya kuomba msamaha. Kesho yake darasa lilianza kujengwa, kila kiongozi wa eneo lile akiwepo.

Kama hawa viongozi wa kipindi kile walifanya hivyo, ina maana walikuwa na akili, busara na uelewa kuliko hawa tulio nao leo? Hao viongozi walioamrisha au kutenda unyama huo huko Simiyu waliokotwa wapi? Viongozi wa namna hiyo wapo tu huko Simiyu au wapo na kungine?

Viongozi waliotoa amri za kuwapiga watoto wa shule ambao walikuwa hawaandamani kwa vurugu, wafukuzwe kazi na washtakiwe. Pia wapimwe ili kujua kama ni mentally fit maana si rahisi mtu mwenye akili kutenda waliyoyatenda.
 
Mkuu umetoa mifano mizuri, hapa wengi wetu tunalaumu polisi, sawa polisi wametenda unyama ila polisi sio chanzo cha tatizo, polisi kuna mtu kawapa amri, yaani kwa ufupi viongozi ndio wametenda unyama.
Polisi hata aone watu wanaandamana hawezi kuwazuia wala kukataza bila kupewa amri

Tukubali hatuna viongozi wazuri maeneo hayo, huwezi kutumia polisi kuzuia maandamano ya watoto wa shule.
Mwaka mmoja baada ya Mimi kuhitimu kidato cha nne, niliowaacha kidato cha tatu waliandamana mpaka kwa REO wakishinikiza mkuu wa Shule ahamishwe na hakuna aliyewapiga mabomu wala makofi tena walitoka kijijini mpaka katikati ya mji bila tatizo, sasa hapo kiongozi alikua na utu wala hakuona sababu ya kutumia polisi, aliposikia kuna wanafunzi wanakuja mjini kwa maandamano akasema waacheni waje cha msingi lindeni wasiharibu miundombinu na rasilimali za jamii.

Sasa hivi tuna viongozi wanaojiona miungu watu, tatizo sio polisi na kama polisi ni tatizo basi mchango wao juu ya kusababisha tatizo ni kama 0.5% tu 99.5% ni viongozi
 
Nahisi police wakipewa order huwa hawaruhusiwi kufikili ila kuacf tuu

Ni kama marobot tuu
 
Nahisi police wakipewa order huwa hawaruhusiwi kufikili ila kuacf tuu

Ni kama marobot tuu
Ukijua hivi ni heri ukawadharau tu, ukiona wanakuja wewe mapema jiepushe nao.

Maana tutaishia tu kutoa mapovu kama hivi wewe tayari ni kilema.
 

nashangilia na pilau napika nakula nakunywa na soda
 
Unafikiri mbwa aanakili ,ukimwambia shikaaaaa,hata mama yako atamshika na kumng"ata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…