Ukata : Kuathiri Mila na Desturi za Makabila na Taifa

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,013
3,648
Baadhi ya mila na desturi za makabila yetu zimejengwa kwa muda mrefu kupitia misingi kadhaa. Baadhi ya misingi hiyo ni pamoja na,sherehe za kimila,koo kutembeleana,matamasha maalumu,michezo,ngoma,jando na unyago nk. Kwa kupitia hayo mambo kulikuwa na muendelezo wa mila na maadili mema yaliyofundishwa kwa vizazi vipya .Ili ufanikishe baadhi ya hayo hapo juu,uwezo wa kiuchumi, hamasa na muda vilihitajika. Kwa hali ilivyo ya ukata na mabadiliko ya kiuchumi sehemu mbalimbali nchini ,ni vigumu kujishughulisha na mambo hayo ya kimila. Madhara yake ni matarajio ya mabadiliko makubwa ya tabia na maadili ya kizazi kipya na cha zamani!
 
Back
Top Bottom