Ukarabati Sekondari ya Mzumbe kuchunguzwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amuagiza uongozi wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuuchunguza mkataba wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya Wavulana-Mzumbe, ulioingiwa kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Shirika la Nyumba la Taifa-NHC ili kujiridhisha kuhusu gharama halisi za mradi baada ya kubaini kiasi kinachodaiwa kutumika kukarabati shule hiyo kinatofautiana na fedha halisi zilizotolewa na Serikali

Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo alipotembelea na kufanya ukaguzi wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya wavulana ya Mzumbe iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro na kuelezwa na viongozi wa wilaya hiyo akiwemoo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kutokuwa na taarifa zozote kuhusu mradi huo.

Dkt. Kijaji alishangazwa na utofauti wa kiwango cha fedha kilichoainishwa katika taarifa ya gharama ya ukarabati wa shule hiyo kwamba ilikuwa shilingi milioni 999.7 wakati kiasi cha fedha kilichotolewa na Serikali ni zaidi ya shilingi bilioni 1.

Alitoa wito kwa wakuu wa wilaya kote nchini kufuatilia kwa karibu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili kujiridhisha kuhusu fedha zinazotumika kwenye miradi hiyo, kukagua thamani ya fedha kwenye miadi husika, pamoja na mikataba yote inayohusika ili kujua mawanda (scope) ya miradi hiyo

"Kila anayekuja kutekeleza miradi katika Wilaya ni vema akaulizwa amekuja kufanya nini na kwa namna gani kwa kuwa lengo ni kuwasaidia wananchi wa maeneo husika na Taifa kwa ujumla na hakuna siri kwenye miradi hiyo kwa hiyo ni lazima muijue kwa undani" alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa, Shule Kongwe ya Mzumbe imekarabatiwa na mabadiliko yanaonekana lakini ni vigumu kujua ilitakiwa kukarabatiwa kwa kiwango kipi na maeneo gani kwa kuwa wahusika wakiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na Mkuu wa Shule hiyo hawafahamu mawanda ya mradi huo.

"Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero hakikisheni mnapata mkataba wa ukarabati wa shule hii ili kupata uhakika wa nini kilitakiwa kifanyike kwa kuwa bado maeneo mengi hayajakarabatiwa na Mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa lakini tayari amekabidhi kazi" alisisitiza Dkt Kijaji.

“Dhamana ya Wizara ya Fedha na Mipango ni kutafuta fedha, kupeleka maeneo husika kwa ajili kubadili maisha ya watanzania na kukagua matumizi yake, hivyo hali hiyo iliyojitokeza inaenda kufanyiwa kazi kwa lengo la kuongeza ushirikiano”, alieleza Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kyombo, aliishauri Serikali kuona namna bora ya kuboresha ushirikiano wakati wa utekelezaji wa miradi kama hiyo kuanzia kwenye upembuzi yakinifu wa majengo yanayokarabatiwa, nini kikarabatiwe, wakati gani, na kuwahusisha wataalam wa wilaya wakati wa kukagua na kutathimini kazi iliyofanyika kabla ya mkandarasi kulipwa

Naye Mkuu wa Shule hiyo Kongwe ya Mzumbe Bw.Wal Kihongosi, aliishukuru Serikali kwa hatua yake ya kuboresha shule hiyo ya vipaji maalum kwa kuwa hapo awali mazingira yake yalikua hayasadifu hadhi ya kuwa na wanafunzi wenye vipaji.

Pia akaiomba Serikali kusaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi, kuongeza vifaa vya maabara kwa kuwa havitoshi, kujengewa jengo moja jipya kwa ajili ya ofisi ya taaluma pamoja na idara zake tisa na pia kuongeza idadi ya watumishi wakiwemo wapishi na walinzi walioajiriwa wa muda mrefu badala ya waliopo ambao ni wa mkataba wa mda mfupi ambao udhibiti wake kulingana na unyeti wa kazi hizo ni mgumu.
 
... hii nchi ina mchwa kila mahali! Na mchwa hawa, always wana mikadi ya kijani mifukoni mwao.
 
Had nashikwa njaa duuh kila mtu ni mpgaji
 
Hajui hata kiasi, anaposema zaidi ya 1B maana yake nini?
Aseme halisi walizotoa na zilizotumika halisi zipo 999.7m na salio lirudi na sioni sarakasi hapo.
Angesema tu tumetoa kiasi fulani na zimetumika kiasi fulani ila zilizopo ni kiasi fulani. Hapo ni upande wa uhasibu baadae unafanya tathmini ya thamani ya fedha ya mradi huo na kujiridhisha kama ipo.
Hawa viongozi sijui wakoje, wanakurupuka tu na taarifa nusu nusu ili wainekane wapo ila weredi hakuna kwa sababu wanaamini kuteuliwa kwao ni kwamba wanajua kila kitu.
 
Uongozi wa wilaya haufahamu mradi huo alaf uongozi huo huo unaagizwa kuchunguza mradi usioufahamu. Hapo inamaana wizara ya Elimu iliingia mkataba na NHC pasipo kuhusisha uongozi wa shule na uongozi wa wilaya. Kama ndivyo, uongozi wa wilaya hauna ubavu kuichunguza wizara na NHC kuhusu mradi huo. Mtoto amchunguze mzazi????,_Hapo atumwe CAG kuchunguza na sio uongozi wa Wilaya. Angalau Mzumbe imekarabatiwa, je shule ambazo mkandarasi ameondoka kabla ya kutekeleza mradi, waziri anasemaje?, Mfano ni Jabgwani na Kibaha sekondari ambako TBA kishafungasha na ukarabati haujafanyika?. Bado sana, wasaidizi wa JPM hawawajibiki ipasavyo, hili nalo mpaka Mh. Rais aingilie kati wakati wasaidizi mpo?. Tusimchoshe Mh. Rais na vijimambo vidogo vidogo ambavyo wstendaji wa chini wanavimudu.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amuagiza uongozi wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuuchunguza mkataba wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya Wavulana-Mzumbe, ulioingiwa kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Shirika la Nyumba la Taifa-NHC ili kujiridhisha kuhusu gharama halisi za mradi baada ya kubaini kiasi kinachodaiwa kutumika kukarabati shule hiyo kinatofautiana na fedha halisi zilizotolewa na Serikali

Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo alipotembelea na kufanya ukaguzi wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya wavulana ya Mzumbe iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro na kuelezwa na viongozi wa wilaya hiyo akiwemoo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kutokuwa na taarifa zozote kuhusu mradi huo.

Dkt. Kijaji alishangazwa na utofauti wa kiwango cha fedha kilichoainishwa katika taarifa ya gharama ya ukarabati wa shule hiyo kwamba ilikuwa shilingi milioni 999.7 wakati kiasi cha fedha kilichotolewa na Serikali ni zaidi ya shilingi bilioni 1.

Alitoa wito kwa wakuu wa wilaya kote nchini kufuatilia kwa karibu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili kujiridhisha kuhusu fedha zinazotumika kwenye miradi hiyo, kukagua thamani ya fedha kwenye miadi husika, pamoja na mikataba yote inayohusika ili kujua mawanda (scope) ya miradi hiyo

"Kila anayekuja kutekeleza miradi katika Wilaya ni vema akaulizwa amekuja kufanya nini na kwa namna gani kwa kuwa lengo ni kuwasaidia wananchi wa maeneo husika na Taifa kwa ujumla na hakuna siri kwenye miradi hiyo kwa hiyo ni lazima muijue kwa undani" alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa, Shule Kongwe ya Mzumbe imekarabatiwa na mabadiliko yanaonekana lakini ni vigumu kujua ilitakiwa kukarabatiwa kwa kiwango kipi na maeneo gani kwa kuwa wahusika wakiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na Mkuu wa Shule hiyo hawafahamu mawanda ya mradi huo.

"Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero hakikisheni mnapata mkataba wa ukarabati wa shule hii ili kupata uhakika wa nini kilitakiwa kifanyike kwa kuwa bado maeneo mengi hayajakarabatiwa na Mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa lakini tayari amekabidhi kazi" alisisitiza Dkt Kijaji.

“Dhamana ya Wizara ya Fedha na Mipango ni kutafuta fedha, kupeleka maeneo husika kwa ajili kubadili maisha ya watanzania na kukagua matumizi yake, hivyo hali hiyo iliyojitokeza inaenda kufanyiwa kazi kwa lengo la kuongeza ushirikiano”, alieleza Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kyombo, aliishauri Serikali kuona namna bora ya kuboresha ushirikiano wakati wa utekelezaji wa miradi kama hiyo kuanzia kwenye upembuzi yakinifu wa majengo yanayokarabatiwa, nini kikarabatiwe, wakati gani, na kuwahusisha wataalam wa wilaya wakati wa kukagua na kutathimini kazi iliyofanyika kabla ya mkandarasi kulipwa

Naye Mkuu wa Shule hiyo Kongwe ya Mzumbe Bw.Wal Kihongosi, aliishukuru Serikali kwa hatua yake ya kuboresha shule hiyo ya vipaji maalum kwa kuwa hapo awali mazingira yake yalikua hayasadifu hadhi ya kuwa na wanafunzi wenye vipaji.

Pia akaiomba Serikali kusaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi, kuongeza vifaa vya maabara kwa kuwa havitoshi, kujengewa jengo moja jipya kwa ajili ya ofisi ya taaluma pamoja na idara zake tisa na pia kuongeza idadi ya watumishi wakiwemo wapishi na walinzi walioajiriwa wa muda mrefu badala ya waliopo ambao ni wa mkataba wa mda mfupi ambao udhibiti wake kulingana na unyeti wa kazi hizo ni mgumu.
 
Mbali na fedha za serikali wana M.A.V.I Alumni Tulitoa Michango yetu kufanya ukarabati wa shule.
 
Mkuu wa shule, mkurugenzi na DC hawajui chochote? Basi mradi wa wakubwa wizarani na pengine waziri yumo. Tumemwona waziri wa Elimu akiwaajibisha wakuu wa vyuo vya ualimu Mpwapwa na Patandi lakini Mzumbe yupo Kmyaaa. Kulikoni?
 
Back
Top Bottom