Ukanda na Udini Waitesa na Kuisambaratisha CCM!

Ukanda na Udini Waitesa na Kuisambaratisha CCM!

M.L.

Senior Member
Joined
Feb 11, 2012
Posts
185
Reaction score
120
Kuelekea uteuzi wa mgombea wa urais kupitia CCM. Chama hicho kimejikuta kwenye mgogoro mkubwa kupita ule wa CCM-Orignal na CCM-Magamba. Mgogoro mkubwa unaoelekea kupigia msumari wa mwisho kwenye jeneza la marehem ccm ni ule wa "Udini na Ukanda".

Kuna mgawanyiko mkubwa baina ya wanaotaka rais ajaye kupitia CCM kwamba panga pangua awe ni mwiislam. Kwa upande wa pili, kuna kundi linalodai kwamba rais ajaye ni lazima awe mkristo. Kundi la kwanza linaongozwa na JK mwenyewe ambaye ameeapa kwamba mrithi wake ni lazima awe mwislam.

Jk anapata shinikizo hili kutoka kwa wanazuoni na wazee wa pwani ambao wanataka kukamilisha misheni yao inayodaiwa eti kuondoa mfumo kristo na kuweka mfumo islamu. JK amepongezwa na wanazuoni hao kwa kufanikisha kuteua waislamu wengi kwenye nyadhifa muhimu serikalini na kwenye mashirika ya umma.

Kwa upande wa watetezi na wanaotaka rais ajaye kuwa mkristo wanadai kwamba nchi hii kila inapokuwa chini ya rais mwiislam mambo huenda shaghala baghala. Ni wakati wa vipindi vya marais waislam ambapo nchi hugawiwa waarabu kwa fujo. Mfano, Loliondo. Huku wairan wakiingia mikataba ya kumiliki ardhi na kuifanya ni maeneo ya kuzalishia vyakula kwa ajili ya nchi zao mfano, ardhi ya rufiji kwa wairan (washiraz).

Kundi hili linaongozwa na Lowassa, Sitta. Mwakyembe na wengine. Katika eneo hili tofauti zinazotangazwa na vyombo vya habari juu ya watu hawa imefutika na haipo katika mkakati huu.

Kwa upande wa UKANDA; kuna kundi linalodai kwamba haiwezekani rais ajaye atoke kanda ya pwani kwa mara nyingine. (Mkapa-Mtwara, Mwinyi-Kisarawe,au Zanzibar; na Kikwete-Pwani). Kwa hiyo, zamu hii rais anapaswa kutoka ukanda tofauti na huu.

Wakati huo, watetezi wa ukanda wa pwani, wanaona ni vema Membe kuwa mgombea kuliko mtu mwingine ye yote. Aidha, Membe anaonekana kufaa kwa kuwa pia anatetea na kuona umuhimu wa Tanzania kujiunga na OIC. Vile vile, hana matatizo na uwekezaji wa kifisadi wa waarabu katika ardhi ya Tanzania.

Madai haya ya ukanda yanaonekana kuwa na nguvu kiasi fulani. Ni madai ambayo yameweza kuwaunganisha watu wenye nia ya kugombea urais kikanda. Watu wa magharibi, wanadai wamesahaulika sana. Na kwa madai haya, Pinda, Lage na hata mbunge wa Chadema Zitto anaafikiana nalo. Zitto na Pinda walionekana kuongea lugha moja linapokuja suala la reli na miundombinu mingine.

Kwa hiyo, pamoja na makundi ya ufisadi na matabaka kati ya wenye fedha (hujiita ''CCM ina wenyewe'') na wasio na fedha ambayo yanakitesa chama, hili la udini na ukanda limeanza kuwa na nguvu mno. Makundi haya yameweza kuwaunganisha hata mahasimu wa makundi ya awali.
 
Siku ya siku wananchi wataamua kumchagua raisi wao wamtakaye, awe Mwislamu, Mkristo au wa Kolelo!
 
Waache wagombane, 2015 out Magamba, hakuna cha rais muislam wala mkristo, ndani ya magamba hakuna mwema, wote wachawi na wezi.
 
Hilo na mm mwenyewe nimelikia ila wamesema atakaye tangaza kwa sasa kuwa atagombea urais wa Hilo na mm mwenyewe nimelikia ila wamesema atakaye tangaza kwa sasa kuwa atagombea urais wako tayari kumfuta uanachama.
 
Uamuzi ni waTZ wenyewe, kama wataendelea kutawaliwa na mafisadi au la
 
Hayo ya ukanda na udini mbona yanajulikana yapo chama gani? Au unajaribu kugeuza usiku kuwa mchana na mchana kuwa usiku.
 
Kumbuka maneno aliyoyasema mtei baada ya zitto kutangaza nia kugombea urais na kilichotokea juzi baada ya mbowe kumtangaza slaa kuwa ndiye mgombea pekee wa urais kupitia chadema
 
Pole yao...natamani hata leo ccm ife kabisa....

ccm haiwezi kupotea mkuu, utakufa wewe na husuda zako na chuki zako ccm itazidi kuchanja mbuga ikiwaletea maendeleo watanzania ukiwemo wewe
 
Pole yao...natamani hata leo ccm ife kabisa....
wakati wewe unakufa na husuda na chuki ambayo itakusababishia vidonda vya tumbo, ccm kinaendelea kuwaletea maendeleo watanzania. Pia wananchi watazidi kujenga imani yao kwa ccm chini ya uongozi imara wa rais kikwete
 
Ni chama gani hapa tanzania ambacho kinatuhumiwa kuwa ni cha ukanda wa kaskazini? Mleta mada hujafanya uchunguzi wa kutosha
 
Kazi ipo kwa akili ya kawaida huo ni ulafi wa madaraka na ifike mahala tuwe macho na hawa wenzetu nchi imeshawashinda.
 
bado wanauota urasi wakati wanajua fika 2010 wananchi hawakuwachagua bali walijichagua wenyewe
piga ua 2015 lazima rais aotoke upinzani, la sivo nchi haitatawalika
kila mtu kachoka na CCM
 
Back
Top Bottom