Ukanda na Udini Waitesa na Kuisambaratisha CCM!

Ukanda na Udini Waitesa na Kuisambaratisha CCM!

Nafikiri ukanda na udini viko CDM zaidi kuliko CCM!

CCM ukisema kuna kundi la mafisadi na wanaopinga ufisadi hapo naweza kukubaliana na wewe, sio udini wala ukanda.
 
Majungu,fitina na uongo+propaganda kwangu mwiko kushabikia

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hayo ya ukanda na udini mbona yanajulikana yapo chama gani? Au unajaribu kugeuza usiku kuwa mchana na mchana kuwa usiku.
mkuu ni kweli tupu udini na ukanda umeingia kwa kasi sana ndani ya ccm,inasemekana ndani ya kamati kuu waislamu ni wengi kuliko wakristo!
 
utakufa wewe na kizazi chako na jamaa zako ccm mtaiacha. Au kwa maana ingine ccm daima
unamfahamu kupe?. ng'ombe anapelekwa machinjioni kupe ameng'ang'ania, anachinjwa kupe ameng'ang'ania, ngozi inaaanikwa kupe ameng'ang'ania, ngozi ikashakauka ndo kupe anashituka, hee! kumbe ng'ombe kashakufa!. wafuasi wa ccm huwa nawafananisha na kupe. hadi sasa hawaoni kama ccm imekufa. mia
 
Udini ndani ya ccm sio propaganda ni ukweli mtupu,hoja inayojengwa ni kuwa wakristo wameongoza miaka 33 kwenye urais na waislamu wameongoza miaka 20,nimeongea na kiongozi wa ndani wa ccm,amesema hata viongozi wa dini zote wanatumika kwenye mpango huu ndani ya ccm!
 
Dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mfu, ukianza huachi na hiyo dhambi itakutafuna hadi ikumalize. Propaganda za CCM kuhusu udini na ukabila walizokuwa wanazushiwa vyama kam CUF enzi hizo na sasa CDM, lazima ziwatafune wenyewe. Kiukweli mambo ya UDINI na UKABILA yameletwa na kukuzwa sana na CCM wakidhani ni njia sahihi kuviangamiza vyama vya upinzani, sasa itawarudi ni suala la mda tu. Kila mwenye mapenzi mema na nchi angetamani CCM kwakweli ipotee kwenye anga za siasa, kwani ni janga la taifa
 
CCM's they are planting the seeds of their own destruction !
 
wakati wewe unakufa na husuda na chuki ambayo itakusababishia vidonda vya tumbo, ccm kinaendelea kuwaletea maendeleo watanzania. Pia wananchi watazidi kujenga imani yao kwa ccm chini ya uongozi imara wa rais kikwete
Wacha ndoto za mchana...ni wananchi gani wanaozidi kujenga matumaini na CCM?? au ni wale wanachama wenu million 5???
 
Kuelekea uteuzi wa mgombea wa urais kupitia CCM. Chama hicho kimejikuta kwenye mgogoro mkubwa kupita ule wa CCM-Orignal na CCM-Magamba. Mgogoro mkubwa unaoelekea kupigia msumari wa mwisho kwenye jeneza la marehem ccm ni ule wa "Udini na Ukanda".

Kuna mgawanyiko mkubwa baina ya wanaotaka rais ajaye kupitia CCM kwamba panga pangua awe ni mwiislam. Kwa upande wa pili, kuna kundi linalodai kwamba rais ajaye ni lazima awe mkristo. Kundi la kwanza linaongozwa na JK mwenyewe ambaye ameeapa kwamba mrithi wake ni lazima awe mwislam.

Jk anapata shinikizo hili kutoka kwa wanazuoni na wazee wa pwani ambao wanataka kukamilisha misheni yao inayodaiwa eti kuondoa mfumo kristo na kuweka mfumo islamu. JK amepongezwa na wanazuoni hao kwa kufanikisha kuteua waislamu wengi kwenye nyadhifa muhimu serikalini na kwenye mashirika ya umma.

Kwa upande wa watetezi na wanaotaka rais ajaye kuwa mkristo wanadai kwamba nchi hii kila inapokuwa chini ya rais mwiislam mambo huenda shaghala baghala. Ni wakati wa vipindi vya marais waislam ambapo nchi hugawiwa waarabu kwa fujo. Mfano, Loliondo. Huku wairan wakiingia mikataba ya kumiliki ardhi na kuifanya ni maeneo ya kuzalishia vyakula kwa ajili ya nchi zao mfano, ardhi ya rufiji kwa wairan (washiraz).

Kundi hili linaongozwa na Lowassa, Sitta. Mwakyembe na wengine. Katika eneo hili tofauti zinazotangazwa na vyombo vya habari juu ya watu hawa imefutika na haipo katika mkakati huu.

Kwa upande wa UKANDA; kuna kundi linalodai kwamba haiwezekani rais ajaye atoke kanda ya pwani kwa mara nyingine. (Mkapa-Mtwara, Mwinyi-Kisarawe,au Zanzibar; na Kikwete-Pwani). Kwa hiyo, zamu hii rais anapaswa kutoka ukanda tofauti na huu.

Wakati huo, watetezi wa ukanda wa pwani, wanaona ni vema Membe kuwa mgombea kuliko mtu mwingine ye yote. Aidha, Membe anaonekana kufaa kwa kuwa pia anatetea na kuona umuhimu wa Tanzania kujiunga na OIC. Vile vile, hana matatizo na uwekezaji wa kifisadi wa waarabu katika ardhi ya Tanzania.

Madai haya ya ukanda yanaonekana kuwa na nguvu kiasi fulani. Ni madai ambayo yameweza kuwaunganisha watu wenye nia ya kugombea urais kikanda. Watu wa magharibi, wanadai wamesahaulika sana. Na kwa madai haya, Pinda, Lage na hata mbunge wa Chadema Zitto anaafikiana nalo. Zitto na Pinda walionekana kuongea lugha moja linapokuja suala la reli na miundombinu mingine.

Kwa hiyo, pamoja na makundi ya ufisadi na matabaka kati ya wenye fedha (hujiita ''CCM ina wenyewe'') na wasio na fedha ambayo yanakitesa chama, hili la udini na ukanda limeanza kuwa na nguvu mno. Makundi haya yameweza kuwaunganisha hata mahasimu wa makundi ya awali.
Tangia nianze kuwa shabiki wa JF mpaka kuja kuwa member sijawahi kukutana na thread mbovu kama hii.
 
Naona umeamua kuwapa watengeneza sumu dose yao wenyewe.
Hakuna atakayesalimika tukiangukia kwenye udini na ukabila/ukanda. Kenya watatucheka sana!
 
Back
Top Bottom