Ukali na tishio kutumia nguvu wanavyofanya Raisi Samia na Mchengerwa "kulinda" amani ya Tanzania ni vigumu sana mtu kuamini Tanzania ni nchi ya amani!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
14,176
Reaction score
25,919
Nimewasikiliza Raisi Samia na waziri wake Mchengerwa wakiongea kuhusu "kulinda" amani ya Tanzania, kwa namna ya ukali na kuonyesha watatumia nguvu kubwa kuilinda hiyo "amani", kiasi kwamba najiuliza, kama Tanzania ni nchi ya amani, kwa nini muongee kwa ukali namna hii na kutoa vitisho vya ajabu kiasi hicho kwa watu wanaoishi ndani ya nchi ya amani?

Huko Mbeya Mchengerwa ameongea kama yeye ndio Raisi wa Tanzania, mabavu, na vitisho utafikiri yeye ndioanaamrisha majeshi ya Tanzania

Ni wazi kama Tanzania ni nchi ya amani, na kuna tatizo au jambo limejitokeza, basi utatumia njia za amani kushughulikia mambo yanayoletwa mezani. Kwa nini utumie ukali na kutishia watu kwamba watakiona cha mtema kuni ikiwa unatambua kwamba hao watu ni sehemu ya nchi yenye amani?

Ni wazi basi ni nani hapa anaetaka kuondoa amani ambayo Watanzania tumeizoea sana nchini. Iweze Raisi Samia katika nchi ya amani anawaambia JWTZ wajiandae na mapambano wakati wa uchaguzi? Tanzania nchi ya amani unawaambia JWTZ wakae tayari kwa ajili ya uchaguzi mkuu? Kupambana na nani, wananchi? JWTZ Vs WTZ?

Katika nyumba yenye amani, ikitokea mtu mmoja analeta jambo, hata kama hulipendi au anatumia njia usizopenda kuliwakilisha, wewe mwenye kutambua thamani ya amani utashughulikia hilo jambo kwa amani, la sivyo wewe unaweza kuwa mbaya kuliko huyo mtu unaemtuhumu kuwa anatishia amani.


View: https://www.youtube.com/watch?v=mxArtpEEGng

Your browser is not able to display this video.
 
Mtu na mkwe wake wanafarijiana
 
Inashangaza Sana. Ni sawa na mtu aseme muda aliopo ni mchana wakati anakuwa bize kuwasha taa!

Kama kweli kuna amani mbona vurumai za kutumia mabavu zipo nyingi?
Hilo ndilo linanishangaza.Watu hawa wanahubiri sana Tanzania ni nchi ya amani,lakini matendo yao kwa hao watu wali kwenye nchi ya amani ni tofauti kabisa na kauli zao za Tanzania ni nchi ya amani
 
Itafika 2100 bado mtasema hv hv
Unataka tuanze kusema tuchukue silaha? Kama ingekuwa ni kuchukua silaha kupambana na CCM na jeshi lao la polisi, huenda hata mie ningefanya hivyo. Lakini ukichukua silaha unawachokoza tu JWTZ ambao hawana kosa katika yote haya, lakini itabidi wao ndio watumwe kukabiliana na wewe, na itabidi watii amri ya Amri Jeshi Mkuu. Ila uwezo wa kuzuia nchi kufika huko uko mikononi mwao.
 
Amani wanataka kuipoteza wao kwa kukataa uchaguzi wa haki kwa wote
 
Kama huoni kosa kwa JWTZ unaonaje kosa kwa polisi wakati hao wote wanafuata amri ya boss wao?
 
Itafika 2100 bado mtasema hv hv
JPM Ndo muasisi wa Udikteta Tanzania ndio kazalisha madikteta wengine kama ilivyo kwa Uganda baada ya Idi Amin akaja Muse7 naye Dikteta so kwa hyojamaa wenu faru John hunambii kitu alikufa Yesu na Muhammad Kifo chake cha 17/3/2021 kinishtue hainihusu hiyo kafa kashakufa na wafuasi wake hamna la Maana basi Kateni rufaa kwa Mungu awarudishieni Mtu wenu
 
Hata ww siku yako ikifika utakufa tuu mkuu na watu watakula wali huku wanacheka
 
Kama huoni kosa kwa JWTZ unaonaje kosa kwa polisi wakati hao wote wanafuata amri ya boss wao?
Kuna sehemu ya uumizaji inafanywa na Polisi kwakuwa wametumwa,lakini sehemu kubwa ni yao wenyewe. Siolazima wafanye vile hata wakitumwa, kwa hiyo hawawezi kuepuka lawama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…