Ukaidi wa Zitto kwa Serikali

Ccm: mcubic
 
zzk kavunja sheria za lumumba ndio maana wanamwandama [emoji13]
 
Hivi aliyoyaongea zitto wewe unaona sio sawa? Kuna mahali gani zitto kakosea? Kwa nini Hampendi kusikia ukweli?
kwa nn watu tunaangalia pa kwenda kusali japo kote inaweza kuwa mahubiri yanamhusu mungu? jibu ni moja tu tunaangalia wanaohubiri watendacho. zito hivo vote anavyoviongea yeye mwenyewe havifanyi. ni mtu wa kujidaidai na kujiweka mbelembele. huyu zito asme tu wazi anataka jpm afike bei ili kumsilence hakuna jingine lolote. wafuasi wa zito poleni
 
Mwana asiesikia LA mkuu ....yetu macho ,walikuwepo wa aina yake .
 
Alaah! Atajuta? Nadhani ni vyema umwelekeze namna sahihi ya kufanya siasa. Inawezekana uchanga wake unamsumbua au vipi? Mwelekeze kijana wetu maana bado tunakwenda na kumhitaji sana
 

JokaKuu
..Nakubaliana na wewe Raisi alimsifia Zitto na sifa sio kitu constant. sifa ni variable
.. swali umajuaje Raisi ndo anatuma askari, kwani kuzuiwa kufanya mikutano imeanza kipindi hiki tu?
.. Kwanini unaamini hawajiamini kwa vigezo vipi, nafikiri serikali inayojiamini inazuia wanasiasa kufanya siasa za fujo kama wanazotaka kufanya wanasiasa ktk awamu ya tano. Hakuna nchi yoyote inayoruhusu vitu hivyo.
.. Huwezi waruhusu wabwabwaje wakati unataka mikutano yao ilindwe na polisi. Wakati polisi ni resources adimu. Inatakiwa kuwe na hoja wakati na kipindi cha kupiga siasa.
 
Reactions: mmh
Hivi aliyoyaongea zitto wewe unaona sio sawa? Kuna mahali gani zitto kakosea? Kwa nini Hampendi kusikia ukweli?
Chunguza makala nyingi .wasiopenda kusikia ukweli ni chadema na Ninakuhakikishia itawagharimu .mboe kawashikia akiri zenu.
 
Ndo maana Donald alisema waafrika tumejaa unafiki ni kweli badala ya kutoa support kwa ndugu yetu kutetea Uhuru wa kukosoa serikali pale tunapoona inaenda kinyume na sheria ya nchi tunabaki kumponda zito.

Anyway kumponda hakutasaidia chochote ila unaemponda unaonesha ni jinsi gani unahitaji msaada wa kifikira.
 

Kama huyu Zitto angekuwa na "brain kubwa mno!" kama unavyodai, chama cha ACT sasa hivi kingekuwa ndio chama kikuu cha upinzani, na CHADEMA kingekuwa mfu. hizo ndio zilikuwa hesabu za akina Zitto, Kitila na Mwigamba et. al. Rejea kauli za kuvuna wabunge zaidi ya 50, rejea ile "build up towards General elections 2015", pia rejea mashambulizi ya akina Zitto kwa UKAWA, badala ya kuelekeza mashambulizi kwa CCM moja kwa moja.

lakini "brain kubwa mno" ya Zitto imekuja kutoa mbunge mmoja tu kwa ACT, ambaye ni Zitto mwenyewe. Fine, mimi sisemi kwamba Zitto ni "ignorant", lakini ana mapungufu mengi mno na kwa hiyo hafai kuwa kinara katika chama. anafaa kuwa mtu fulani msaidizi, wa kutumwa hapa na pale, lakini hana "Chairman material". na hata hiyo ya kutumwa, ni shida pia, anahitaji kusaidiwa sana tu. mfano angalia alipokuwa Waziri kivuli wa fedha. ndio alikuwa njia ya Mwigulu Nchemba kupandia, alipoichana ile hotuba yake ya bajeti. alifanya makosa mengi ambayo yaliufanya upinzani uwe "embarrassed" na "on the defensive". Zitto haongozwi na logic, bali anaongozwa na tamaa ya madaraka, kujiamini kulikopitiliza, utayari wa kuwa "malaya wa kisiasa" alimradi akidhi haja zake, ambazo ni kubwa kuliko uwezo wake wa kuzifikia.

Nikimlinganisha Zitto na Mbowe, ijapokuwa Zitto ana vyeti vingi zaidi vya darasani kuliko Mbowe, lakini Mbowe ana CV kali zaidi katika utendaji wake. Ukiangalia across the distance ambapo Mbowe alishika hatamu za CHADEMA mpaka hivi sasa, amesafiri umbali mrefu sana, na amekipaisha chama chake. amekipitisha katika maamuzi magumu sana na amefaulu kuyasimamia mpaka kwenye "conclusion". Na kadiri siku zinavyokwenda, tunamshuhudia Mbowe anayezidi kukomaa katika siasa za Vyama vingi, na kuwa "prove wrong" wale ambao wamekuwa wanakitabiria CHADEMA kifo.
 
Zitto kakosea wapi? Alichokiongea kina shida gani?
 
Councils to be given powers to ban peaceful protests that might disturb local residents
Anger mounts at ‘shockingly open-ended’ Anti-social Behaviour, Crime and Policing Bill that could also see youngsters banned from skateboarding, forbid teenagers from using local parks and prevent demonstrators from gathering outside council offices
Councils to be given powers to ban peaceful protests that might
 

Mkuu JokaKuu,

Ukomavu wa kisiasa pale mtu anapokuwa jukwaani au kwenye mihadhara ni pamoja uchaguzi wa maneno ya kutumia katika hotuba zake.

Mheshimiwa Zitto sina uhakika kama ana "hard copy" ya anachokizungumza majukwaani na hasa yake aliyoyasema pale Mbagala, maana wenzie anaoongozana nao wanafanya hivyo.

Atumie walau muda kupitia hotuba au maoni yake kwani yamejaa jazba na maneno ya kashfa.

Hata kama amesema raisi JPM alikwenda Rwanda kwa Kagame kujifunza kubinya demokrasia, lakini nina uhakika wa 100% angesema maneno yake kule Kigali leo hii angekuwa kizuizini.

Hivyo ukimya wa raisi JPM haumaanishi kwamba watu watumie maneno ya kashfa kwa kiongozi wa nchi alie madarakani.
 
mbowe ni heri mara 100 kuliko zitto. makosa ya mbowe ni machache na yanarekebishika with time, mara nyingi mbowe yuko smart kwa kweli na yuko kiasi. eti kiongozi mkuu wa chama!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…