Ukaguzi wa Watanzania airport ughaibuni:

Ukaguzi wa Watanzania airport ughaibuni:

Nimjuavyo Kikwete mimi, hapa atakuwa kakaa ikulu anaangalia hii katuni na kucheka ile mbaya.
 
Nasikia kituo kimoja cha kuponda maraha cha wazungu wa unga na unga unauzwa njenje ni pale Bilicanas.
 
Mbona huyo muhusika kwenye hiyo katuni anafanana na msanii Diamondi?

Nawasikitikia sana hawa GREENGUARD tunaoambiwa wanafundishwa UJASIRIAMALI ambao sasa tumegundua ujariamali wenyewe ni kugeizwa punda wa kubebeshwa madawa ya kulevya.

Ngoja tuone baba yao DHAIFU atachukua hatua gani kuwakomboa hao vijana zaidi ya 200 ktk nchi tofauti kama alivyomkomboa mwanae kwa dhamana ya gesi mtwara.
Niko na jamaa yangu ambaye ni Msingapore hapa Australia, Marekani yenyewe ilichemka kwa hiyo nchi. Kulikuwa na issue fulani hata Bill Clinton alimtwangia simu kiongozi wa Singapore ili wapindishe sheria lkn jamaa akasema no, no, no no. hawezi kfanya hivyo. Kwa hiyo kwa Singapore, mkuu atafanya ziara nyingi tu za kushtukiza na kuchomekea lkn kuwatoa hao mules asahau. Hiyo nchi inafuata sheria kwa 100% na iko huru mno katika maamuzi yao. Kumbuka hao jamaa hata chew-gum kwao haziruhusiwi ili kuogopa kuchafua mji seize kuwawekea mateja mitaani kama Ilala na Magomeni!?
 
Mimi sioni kama mnadhalilishwa ila tunajidhalilisha.Kama nchi haitaki kuharibiwa raia wake kwa unga na watanzania wanalazima wapitishe unga kuna kosa gani kupekuliwa.Lakini mimi Nasema WAPEKUENI mpaka huko nanihii.
Yaani...mimi ndo mhanga wa haya masaibu...siku hizi nikifika tu airport ya hapa nilipo lazima saa nzima ikatike napekuliwa. April rafiki yangu kaja kabeba viungo vya pilau na vingine vilivyosagwa...jamaa walichukua hadi sample wakazifanyia test, kama haitoshi wakachukua hadi unga wa mahindi kuufanyia test..almost two hours ndo wanamwachia. Tunadhalilishwa sana na wenye mamlaka ya kukabiliana na haya masuala.
 
Wiki iliyopita nilikuwa naenda mahala, kasheshe airport niliulizwa swali moja tu 'ur from Tanzania right? ' nikamjibu ndio, kilichofuata nikaambiwa ingia kule, moyo wangu ulinipiga kwa mshangao nikajiuliza kunani? Kumbe kukaguliwa ile mbayaa na maswali juu, cjuhi nchi yetu inakwenda wapi? ??
 
Mimi sioni kama mnadhalilishwa ila tunajidhalilisha.Kama nchi haitaki kuharibiwa raia wake kwa unga na watanzania wanalazima wapitishe unga kuna kosa gani kupekuliwa.Lakini mimi Nasema WAPEKUENI mpaka huko nanihii.
This is ---- Mkuu!! Kama hayakukuta si bora ukae kimyaa. Mko wasafiri kama 200 mmefika airport, harafu peke yako unakalishwa karibu masaa 2, utajisikia vizuri kweli au ndo unadhani watu wote wanaosafiri tunafanya biashara?
 
mimi yalinikuta hayo bado pichu tu sikuvuliwa lakini nilisachiwa kila kitu kuanzia mizigo yangu na mimi mwenyewe
Kweli zamani tulikuwa tukisafiri walahatukuwa na wasiwasi lakini siku hizi utaijuwa joto ya jiwe

laiti kama ningeliweza basi ningelibadilisha uraia wangu kuepuka na ghadhabu hizi halafu ukute una watoto nawe unapigwa bamba sachi na watoto wako wakikuangalia
 
Back
Top Bottom