Ukaguzi wa Watanzania airport ughaibuni:

Ukaguzi wa Watanzania airport ughaibuni:

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,931
Mtanzania airport.jpg

Ndio itakuwa hivi (au tayari ndivyo)!
 
Mkuu Dingswayo inasikitisha sana kusema kweli, kama hali ya kupoteza imani katika jumuiya ya Kimataifa itaendelea itafikia wakati Watanzania wenye safari za kihalali nchi za nje kuzikataa safari hizo kwa kuogopa kudhalilishwa kiasi hiki.
 
Last edited by a moderator:
La kusikitisha ni kwamba wale wanaohusika na kutusababishia kadhia, dhihaka na manyanyaso haya yote wao hupita VIP bila bughudha wala kukaguliwa.
 
Mkuu Dingswayo inasikitisha sana kusema kweli, kama hali ya kupoteza imani katika jumuiya ya Kimataifa itaendelea itafikia wakati Watanzania wenye safari za kihalali nchi za nje kuzikataa safari hizo kwa kuogopa kudhalilishwa kiasi hiki.

Mkuu BAK, zamani miaka ya 80 hadi 90 nilipokuwa nikisafiri nje ya nchi, nilikuwa najivunia sana passport yangu. Chanzo cha kujivunia kilikuwa ni passport yangu, ambayo mara nyingi ilinitambulisha kama Mtanzania na kuulizwa kuhusu Rais Nyerere. Nawaonea sana huruma vijana wengi wa Kitanzania ambao nashuhudia wakisumbuliwa kwa kuwekwa pembeni ili kuhojiwa na kupekuliwa. Ile heshima tuliyopewa zamani imepotea kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama nchi heshima yetu imeshuka sana katika jumuiya ya Kimataifa. Na hakuna dalili zote kama walio madarakani wanafanya lolote lile ili kuirudisha heshima hiyo iliyopotea.

Mkuu BAK, zamani miaka ya 80 hadi 90 nilipokuwa nikisafiri nje ya nchi, nilikuwa najivunia sana passport yangu. Chanzo cha kujivunia kilikuwa ni passport yangu, ambayo mara nyingi ilinitambulisha kama Mtanzania na kuulizwa kuhusu Rais Nyerere. Nawaonea sana huruma vijana wengi wa Kitanzania ambao nashuhudia wakisumbuliwa kwa kuwekwa pembeni ili kuhojiwa na kupekuliwa. Ile heshima tuliyopewa zamani imepotea kabisa.
 
Nikikumbuka alichofanya Mwalimu Nyerere juu ya huyu jamaa 'JK' kwa kile alichodai "hajakomaa kisiasa" nimegundua alikuwa anayajua mapungufu yake yenye madhara kwa Taifa, kweli bana leo nimeelewa!
 
La kusikitisha ni kwamba wale wanaohusika na kutusababishia kadhia, dhihaka na manyanyaso haya yote wao hupita VIP bila bughudha wala kukaguliwa.

Hilo ndo linalokera sana. Tumejiharinia mno kama taifa.
 
swali moja muhimu: "ni nani katufikisha hapa??"
 
Yaani...mimi ndo mhanga wa haya masaibu...siku hizi nikifika tu airport ya hapa nilipo lazima saa nzima ikatike napekuliwa. April rafiki yangu kaja kabeba viungo vya pilau na vingine vilivyosagwa...jamaa walichukua hadi sample wakazifanyia test, kama haitoshi wakachukua hadi unga wa mahindi kuufanyia test..almost two hours ndo wanamwachia. Tunadhalilishwa sana na wenye mamlaka ya kukabiliana na haya masuala.
 
Kuna watu wana hofu na nchi kuja kutawaliwa na wauzaji wa madawa ya kulevya,wengine wanatuambia wauza unga tusiwape madaraka, mkuu wa nchi anasema ana orodha ya wauza unga, sasa kama wanajulikana wote hao, kwa nini tusianze na hao wanaofahamika? Tunazidi kupoteza utu wetu katika ramani ya dunia.
Siku hizi hatumalizi wiki bila kusikia mtanzania kanaswa na madawa ya kulevya sehemu flani. so sad
 
Tatizo kubwa ni nchi kuongozwa kimjini mjini, watawala wameamua kutosimamia viapo vyao na kutupilia mbali vitabu na misahafu waliyotumia kuapa. Tamaa ya kujaza matumbo yao na kutaka kumilikisha familia zao rasilimali na utajiri wa nchi yetu imepelekea taifa kutumbukia kwenye dimbwi la uchafu na uozo uliokidhiri.
 
kikwete anawajua wauza madawa. Ila hataki kuwatajana ktk ile list ya amina chifupa idd azzan yupo.
 
Mbona huyo muhusika kwenye hiyo katuni anafanana na msanii Diamondi?

Nawasikitikia sana hawa GREENGUARD tunaoambiwa wanafundishwa UJASIRIAMALI ambao sasa tumegundua ujariamali wenyewe ni kugeizwa punda wa kubebeshwa madawa ya kulevya.

Ngoja tuone baba yao DHAIFU atachukua hatua gani kuwakomboa hao vijana zaidi ya 200 ktk nchi tofauti kama alivyomkomboa mwanae kwa dhamana ya gesi mtwara.
 
Inadhalilisha sana, most of countries washaanza kutokuwa na iman na sisi tena
 
Inatia huruma. Passport ya bongo haina thamani tena. Nakumbuka nilisafiri bila ya kizuizi miaka ya 85. Uingereza wanakupa Miezi 6 heathrow airport , scandinavia unapita kirahisi na viza za airport, shengen visa na viza za marekani unapata siku hio hio bila ma interview wala nini. Wakaja wabebaji wa unga na wakimbizi Feki na kutuharibia. Sasa hata Thailand hawatupi viza tena airport mpaka uombe viza zao Nairobi. Hong Kong nao karibu watagoma kutoa viza airport. Halafu eti si ruhusa kuwa na Uraia wa nchi mbili! Vichekesho!
 
Nikikumbuka alichofanya Mwalimu Nyerere juu ya huyu jamaa 'JK' kwa kile alichodai "hajakomaa kisiasa" nimegundua alikuwa anayajua mapungufu yake yenye madhara kwa Taifa, kweli bana leo nimeelewa!

Hakuna nchi yeyote duniani inayojiendesha bila miiko so ukipewa jukumu la kuwatumikia wananch lazma ujiheshmu haiwezekani upewe nafasi ya kuwatumikia wananch halafu unaonekana unapita barabarani na wakina mama kama hauwezi acha ukafanye uhuni wako-mwl jk nyerere
 
Exactly...

Haya ndo naanza kuyakumbuka kumbuka kabisaaa!
 
Back
Top Bottom