Ukaguzi wa magari Mbeya umeanza kuleta kero

Mwee

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
240
602
Kufuatia agizo la IGP la ukaguzi wa magari nchi nzima ambayo ni nia njema tu limegeuka kero kwa wasafiri mbalimbali hapa mkoani Mbeya. Sijajua mikoa mingine lakini hili zoezi ni kama halikuandaliwa mazingira mazuri ya kukagua ili kutoathili usafiri.

Mfano, abiria wameshapanda ndani ya gari lakini anatokea askari anakuja kukagua na kuamuru abiria washushwe then ukaguzi unaanza. Unakalishwa zaidi ya saa 6 hadi wengine kulazimika kuahirisha safari.

Kuna basi kidogo askari anayekagua asababishe ajali baada ya kushindwa kulitest huku abiria wakiwa ndani.

Tunaomba serikali iliangalie suala hili ili ukaguzi ufanyike bila kuathili safari za abiria. Safari zinakuwa na sababu mbali mbali kiwemo matibabu, kazi nk.
 
Hii ni early warning: "Kuna basi kidogo askari anayekagua asababishe ajali baada ya kushindwa kulitest huku abiria wakiwa ndani."

Kwani sikio la kufa liliwahi kusikia dawa?
 
Jana nilikua natoka chunya kwenda makongolos.. Nimekaa stand toka saa tano mchana nimekuja kupata gari saa saba..
 
Back
Top Bottom