UK: Wazee wa Uingereza watatizwa na upweke

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,157
2,000


Maelfu ya wazee wa UK wapigia simu huduma ya kijamii ya Silver Line angalau kupata fursa ya kuzungumza kama njia ya kukabiliana na upweke
Huduma za simu iitwayo Silver line iliyoanzishwa kusaidia wazee wanaokumbwa na upweke huko Uingereza imepokea idadi kubwa ya wapigaji simu.
Zaidi ya simu mia elfu zimepokelewa katika kipindi cha miezi sita tangu huduma hiyo kuanzishwa.

Bi Esther Rantzen mwanzilishi wa huduma hiyo Silver Line, anasema kiwango hicho kikubwa cha wapigaji simu ni dhihirisho halisi la tatizo la upweke linalokumba wengi wa wazee katika mfumo wa kisasa wa maisha nchini Uingereza.

Mfumo wa kisasa wa maisha wa Uingereza walaumiwa kuchangia upweke unaokumba wazee.

Wengi wa wazee hao waliopiga simu huelezea jinsi wanavyoishi peke yao na mara nyingi hukosa hata mtu wa kuzugumza nao tu ndiposa hupiga simu laini hiyo kutafuta angalau sikio la kuwasikiliza.

Nusu wa waliopiga simu wamesema wanaeza kukaa kutwa bila kuzungumza na mtu , ilhali mmoja kati ya kumi wakasema huchukua hata zaidi ya wiki nzima bila kupata mtu wa kuzungumza nao.

Utafiti wa kisaikolojia wasema upweke mwingi unaeza kuleta madhara kama vile majonzi, msongo wa mawazo na athari nyenginezo za kiafya na hasa kiakili.

Tahadhari imetolewa kwa nchi zinazoendelea hasa barani Afrika kufanya jitihada kuzuia mmomonyoko wa kimaadili na utamaduni wa kutunza wazee ili kuepukana na hali kama hiyo.

Source: BBC
 

Fabolous

JF-Expert Member
Sep 23, 2010
1,866
2,000
Ni kweli kabisa Wazee wengi UK wanakabiliwa na Upweke sana kutokana na mfumo wao wa maisha, kuna Mzee mmoja nilikua nafanya nae kazi katika Jiji la Bristol alikua mzungumzaji sana tukiwa kazini. Aliniambia anapenda kuongea sana akiwa kazini kwasababu ana miaka karibu 30 anaishi peke yake tu na paka wake nyumbani kwake. Sehemu pekee ya kukutana na kuongea na watu ni kazini muda wa break. Afrika ni Watu wachache sana wanaishi kwa upweke kutokana na mfumo wa maisha yetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom