Wapendwa wana-TzECA,
Natumaini bado mpo na hamjambo.
Mimi Joseph Payne, mzungu ambaye alikuweko Edinburgh zamani, akaenda Dar es Salaam akasikika akiimba Bongo Fleva na mwishowe akawa mtu maarufu, n.k.
Nataka kukujulisheni nyote - lakini hasa wale waliohitimu shahada katika vyuo vya Uingereza na ambao wamesharudi kuishi Tanzania - kwamba linaanzishwa shirika la wahitimu wa vyuo vya Uingereza nchini Tanzania (UK Alumni Association Tanzania).