UK-Africa Investment Summit 2020: Where is top level Tanzania representative?

'Sie tuendelee kujifungia tu, fursa zitatufuata because we are very special breed in planet earth.'

Hahah no wonder Kigwangala alipoulizwa mna mpango wowote ule wa kuidhamini timu huko EPL ili itangaze utalii wetu akasema hapana lkn mpk timu kubwa za ulaya(Man u,Chelsea,Arsenal) hua zina tubembeleza tuzidhini,hahah akili zetu bana.

dodge
 
UK ni moja wa nchi yenye FDIs nyingi na inayotoa misaada mingi Tanzania. Kuikwepa ni sawa na kuingiza kichwa chini ya mchanga huku kiwiliwili chote kipo nje.

Kwahiyo ule mkutano ni wakujihakikishia uwekezaji zaidi?
 
Mnangagwa alikuwa DAVOS last year na aliona msaada.Je alipewa?
 
Wewe unaamini kweli kuwa UK inataka kufanya biashara na Afrika?

Kama kweli mbona wao wanafanya biashara na wachina wakati sisi wanatuzuia?

Umeamka sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nisiamini vipi kwani kilichofanyika ni siri? Kongamano hilo lilikuwa la kuipa fursa Africa kufanya biashara na UK sababu UK ikishatoka EU itakuwa na uwezo wa kufanya biashara moja kwa moja na nchi yeyote. Sio kama sasa biashara nyingi lazima zifate masharti ya EU. Kuhusu swala la kwa nini UK wanatuzuia kufanya biashara na China wakati wao wanafanya nao?? Wewe aliyekwambia UK wanatuzuia sisi kufanya biashara na wachina nani??? Hebu acha maneno ya uzushi yasiyo na ushahidi.
 
Kwa hiyo nyie mmechagua Ulaya?
 
Kama mna akili finyu wakati mwingine mkae kimya tu badala ya kubwata mambo ambayo hamyajui.

Rwanda baada ya vita wasamalia wema wamewapa pesa kibao. Wako wangapi? Wana soko gani ukilinganisha na sisi?

Kenya imeweka rehani bandari yake ya Mombasa kwa SGR ambayo imekost hela nyingi kuliko SGR yetu ya umeme kwa wachina. Uhuru alienda tena kukopa kwa ajili ya kuendeleza Reli amenyimwa. Sasa unata kutuambia nini? Kenya ni vibaraka wa Europe. Bila Europe Kenya haiwezi ku exist. Wakenya ni wanafiki sana. Kila kitu mzungu anacho taka nao wanakubali bila kujiuliza. Wakenya sio watu wa kuwaamini hata mara moja.

Wazungu lazima watupige vita sisi, kwani wanajua kuwa tukifanikiwa sisi tutakuwa mfano kwa nchi nyingi za Afrika. Wanaliogooa hilo. Hawata kuwa na watu wa kuwaheshimu na kuwasujudu tena. Wa Asia wanajiamini na kufanya mambo yao.
 
Ni msimamo mzuri sana. Asante.
 
Ni tatizo la nani sasa? La Magu? Acha kelele. Kosa la Magufuli ni kuwa anawapeleka wasomi wa vitabu na sio wasomi ambao wanajua thamani ya vitu.
 
Kwenye "akili finyu" hainipi shida kwa sababu nakufahamu vyema sana wewe kwa michango yako humu JF.

Kuhusu Kenya kuwa kibaraka na mnafiki, hapo nakupongeza sana kwa kulijua hilo, lakini sio jambo jipya ulilogundua wewe na kulifanya likuonyeshe wewe kutokuwa na akili finyu.

Kuhusu "wazungu kutupiga vita", hata mkijipiga vita nyinyi wenyewe mnalia "wazungu wanawapiga vita".

Sasa niambie, hii yako sio "akili finyu" kwa sababu gani?
 
Ni tatizo la nani sasa? La Magu? Acha kelele. Kosa la Magufuli ni kuwa anawapeleka wasomi wa vitabu na sio wasomi ambao wanajua thamani ya vitu.
Hapo tu, bado huoni unavyojipinga?
Kama sio kosa la Magufuli, kwa nini "awapeleke wasomi wa vitabu..."

Hivi unaelewa unachoandika, au unajiandikia tu!
 
Rwanda ametushinda maeneo yapi na kwa kiwango gani be specific, kwa propaganda sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…