Ujumbe wangu wa Mei mosi

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,942
2,000
1)Mamkuzi na salamua,juu yenu iwe amani
Salamu kwetu muhimu,tena jambo la imani
Kusalimu yalazimu,ni kale tangu zamani
Mei mosi na ujumbe,natamani kuutoa
2)Heko kwa wafanyakazi,walioko makazini
Wale wafanyao kazi,hata wakiwa nyasini
Leo tweke mambo wazi,siyo tuache sirini
Siri ya maendeleo,ni watu kufanya kazi
3)Hii wamu ya kazi,asiejua ni nani
Kazi tusake hijazi,hata kama mashambani
Tuutumie ujuzi,tufurahi maishani
Siri ya maendeleo,ni watu kufanya kazi
4)Masilahi yaboreshwe,mashahara siwe duni
Watu haki wafundishwe,hata ka kitamaduni
Haki zao waonyeshwe,iwatoweke huzuni
Siri ya maendeleo,ni watu kufanya kazi.
5)Mishahara ipandishwe,hata kama viwandani
Li maisha yaboreshwe,na familia nyumbani
Pia vyeo wavalishwe,watu wawaze vichwani
Siri ya maendeleo,ni watu kufanya kazi
6)Tabia undugu ndugu,haipo maofisini
Lilikuwa donda sugu,raisi kapiga chini
Leo hatuna magugu,tuna raisi makini
Siri y maendeleo, ni watu kufanya kazi.
7)Vijana nawausia,lazima changamkeni
Vyema fursa kutumia,tusilale vijiweni
Ubunifu kutumia,kutwa tusicheleweni
Siri ya maendeleo,ni watu kufanya kazi.
8)Serikali na kwa wingi,ajira zitangazeni
Tena zitangazwe kwingi,kila pala zenezeni
Tutayaepuka mengi,pamoja tupendezeni
Siri ya maendeleo,ni watu kufanya kazi.
9)Hata kama tunachoka,tamaa tusikateni
Nchi yetu tajawika,na mazuri kusheheni
Tukitaka nawirika,hili tuzingatieni
Siri ya maendeleo,ni watu kufanya kazi.
10)Kalamu naweka chini,ujumbe uko mwishoni
Raisi pendwa tawika,tapendwa kote moyoni
Nchi inanawirika,kazi tuweke rohoni
Siri ya maendeleo,sisi kujituma sana.
SHAIRI-MEI MOSI
MTUNZI- Idd Ninga
Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom