ujumbe wangu wa leo asubuh

ujumbe wangu wa leo asubuh

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956
1382924_523439647743245_1186629633_n.jpg
 
Kitu pekee kwa mtu mweusi kupambana na UBAGUZI na kujiketea heshima ni kupitia mitazamo ya Marcus Garvey yani GURVEYISM.
Lazima uonyeshe kwamba una uwezi kwa mtu anayekubagua kama kuendesha meli ukianzia kumiliki shirika la meli nk. Ukidai uhuru kujitawala lazima uonyeshe uwezo wa kiuongozi. Afrika bado hatujaonyesha hilo.
Kuhusu Gurvey kutokanyaga afrika ni kwamba harakati zake zilizimwa na weusi wenzake hasa nahodha na wafanyakazi wengine wa meli kwa kushirikiana na FBI. Nahodha Joshua Cockburn alitumwa kwenda kukagua meli na Umoja wa weusi wa UNIA chini Gurvey ili wanunue meli, FBI wakamwambia amwambie gurvey bei ambayo ni mara 6 gharama halisi, nyingine aweke mfukoni.
Akafanya hivyo na wafanyakazi wengine wakapewa hela waweke vitu kwenye injini inoki. Meli kwanza ilikuwa chakavu ilitumika vita ya 1 ya dunia.
Baada ya hapo basi wakamwandalia kesi ili wamfunge kwa kuwatumia weusi wasiojitambua kwa ujira kama unavyoona vipngozi wetu bongo. Sasa walimkamata kw mail fraud yani alitangaza hisa za kampuni kabla ya meli kununuliwa. UKWELI: aliimiza kuanzishwa umoja wa weusi na badala ya kukaa kudai uhuru na haki alitaka waonyeshe wanaweza kujiongoza, kufanya biashara, nk mengine yote yatajileta. Na akasema afrika kwa mwaafrika, ulaya kwa wazungu. Biashara walichanga wakaanzisha nyingi mno kama mighahawa, kumbi za mikutano ( liberty hall), shirika la meli (black star liner) na meli ili badae ziwarudishe afrika. Sasa mail fraud weusi waliolipwa na FBI kumruka walisema kwamba amewachangisha pesa kabla meli kununulia na hata pale iliponunuliwa faida hawapati mgawo wa hisa.
Kumbuka FBI walishatumia weusi kuziua meli, na meli zilinunuliwa kwa michango ambayo waliahidiana kulipana kama hisa kulingana na mchango. Hivyo mwaka 1923 alifungwa miaka mitano na mwaka 1928 alirudishwa jamaica. Mwaka 1940 alifariki kwa mshtuko wa moyo uingereza alikoenda kuanza upya maisha na badae aje afrika.
MEMO za FBI zilitoka zikionyesha kwamba hawakuwa na ushaidi labda wamtoe kama mhamiaji haramu.
Walimwona tishio kwani alifanya waafrika wajione wanaweza na alianzisha kundi kama mgambo hivi.
Nitumie email nikupe maandiko yangu yasiyo rasmi juu yake
 
Back
Top Bottom