The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,778
- 8,209
.
Nimejifunza kuwa kwenye maisha siku moja wakati fulani wale watu tuliowategemea sana watatuacha.
Wapo watakaotuacha kwasababu majira yao kwenye maisha yetu
yameisha.
Kuna watakaotuacha kwasababu kusudi lao kwenye maisha yetu/yao limeisha.
Wapo watakaotuacha kwa kuchukuliwa kuondoka katika Dunia na ulimwengu huu.
Kuna watakao tuacha kwasababu kile walichokitaka kwetu wameshakipata hivyo hawaoni umuhimu wa kuendelea kuwa na sisi walikuja ili wapate kitu/vitu.
Kuna watakaotuacha kwasababu kuna kitu/vitu walitaka kwetu lakini muda umeenda na hawaoni wakipata walichokitaka hivyo hawataona umuhimu wetu tena manaa walichokitaka hawajakipata.
Wapo watakaotuacha kwa kuhamia mazingira mengine tofauti na tulipo sisi na kutuacha.
Wapo ambao wataamua kuachana na sisi ili na wao wakafanye mambo yao mengine tofauti na ya kwetu.
Wapo watakaotuacha kwasababu wamesikia/ wameambiwa mambo mabaya kuhusu sisi hivyo kutokuona umuhimu wa kuendelea kuwa kwenye mzunguko wa maisha yetu.
Haijalishi ni njia gani ambayo inaweza kukutenganisha na mtu/watu lakini moyoni mwangu nataka nikwambie kuwa kuna mtu/watu ambao hutaishi nao milele.
Kuna watu hawatakaa na kwako milele,kuna watu hawataambatana na wewe milele.
Wakati wa mtu ukifika wa kuondoka kwenye maisha yako ataondoka tu , kwa njia mojawapo kati ya hizo nimezitaja hapo juu .
Hao watoto wako ambao Mungu amekupa leo jitahidi kuishi nao vizuri kwa Upendo,wekeza muda kwao kwasababu siku moja watakuacha na kwenda kuishi maisha yao wenyewe.
,Usijenge nyumba kubwa sana kwa kutegemea watoto wako ndio watakuwa wanaisafisha na kuilalia.
Kuna wakati wataiacha na kwenda kutafuta maisha yao na kujenga nyumba zao.
Ni mwajiri kazini unao wafanyakazi hata kama ni wafanyakazi bora namna gani siku moja watakuacha kwasababu yoyote, hivyo jiweke katika mazingira ya kujipanga je huyu mfanyakazi siku akiondoka kazi zitaendaje? kama ni biashara je itaendelea au ndio itakuwa imekufa...
Mme/mke je umewahi kuwaza siku mwenzi wako akiondolewa maisha yako yatakuwaje?? wether unataka au hautaki siku moja wakati fulani lazima mmoja wenu atahamishwa na kutengwa naye hapa duniani, umewahi kujiuliza utaishije maisha baada ya hapo??
Kuna watu huwa wanasema sitaki kuwaza, ndio hata Mimi sitaki uwaze, lakini nataka nikwambie tu kuwa maisha yako lazima yaendelee baada ya mtu uliyempenda kutwaliwa, yataendeleaje hilo ndilo unatakiwa kuliwaza Sasa.
Dear maisha yetu yanatakiwa kumtegemea Mungu kwa asilimia mia moja kwa kila kitu kwasababu yeye tu ndiye atadumu milele baada ya kila kitu kukoma na kila mtu kutuacha hasa wale tuliohisi kuwa bila wao hatuwezi kuendelea.
Kuna watu huwa tunasema kuwa you are my heart beat,I can't live without you,you are my everything nk.
Hata kama unampenda mtu kwa kiasi gani usimwambie kuwa yeye ndiye mapigo yako ya moyo, maana Iko siku utaondoka na yeye ataendelea kuishi.
USHAURI WANGU
Tuwapende watu, tuonyeshe kuwahitaji lakini tusiwategemee sana watu maana siku moja wakati fulani watatuacha either kwa kuondolewa duniani, kwa kuhama au kwa majira yao kwenye maisha yetu kuisha , na hata hivyo hata baada ya hayo yote Maisha yetu lazima yaendelee.
Je unao watu ambao ulidhani kuwa bila wao huwezi kuishi lakini gafla ukajikuta hawako tena karibu na wewe /kwenye maisha yako?
je uliwezaje kuendelea kuishi? je uliwezaje kufanya vitu ambavyo walikuwa wanakufanyia .
Je uliweza kuendelea au ndio Mwisho wa kile ulichokuwa unafanya.
Jitambue, jiamini,jitume
Maisha hubadilika,majira hubadilika,na watu hubadilika,Mungu pekee habadiliki.Ukiijua hii kanuni itakusaidia sana kutokuishi maisha ya maumivu na majuto ktk maisha.
Huenda umeachwa na watu uliowaamini sana
Umeachwa na watu/mtu uliyempa siri za mpyo wako
Umeachwa na mtu uliyejua kamwe hatakuja kukuacha,umeachwa na mtu aliyesema hatakuacha kamwe lakini leo humuoni.
Mwingine kaondoka ili akukomoe maana aliona unamtegemea na kumuamini sana.
Yote katika yote
Futa machozi
Msihi Mungu akupe kuvuka
Usivuke na maumivu wala majeraha
Usivuke na visasi
Mabaya yote na maumivu yaache mwezi May
Mwezi June ingia na furaha na mtazamo chanya
Mungu atakusaidia tena.