Ujumbe Wa Maalim Seif Shariff Hamad Kwa Wazanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe Wa Maalim Seif Shariff Hamad Kwa Wazanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Jul 3, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  ”Kila Mzanzibari mwenye haki, ahakikishe anajiandikisha kwenye Daftari!”

  • Akagua shughuli za Chama, kuhamasisha Daftari
  • Aonya rafu za CCM, ZEC na Afisi ya Vitambulisho
  • Amwambia Kikwete hatapata kumweka kibaraka wake kuchimba mafuta ya Wazanzibari
  • Afanya mikutano mitano ya hadhara
  • Jumapili aunguruma Gombani


  Katibu Mkuu wa The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi), Maalim Seif Sharif Hamad, yuko kisiwani Pemba katika ziara ya wiki moja.

  Ziara hiyo ilianza tarehe 31 Juni na itamalizika tarehe 4 Julai kwa mkutano mkubwa wa hadhara kwenye viwanja vya Gombani, Chake Chake.

  Hadi sasa, Maalim Seif ameshatembelea na kufanya mikutano ya hadhara katika majimbo ya Micheweni, Tumbe na tarehe 3 Julai atakuwapo kwenye jimbo la Mgogoni.

  Mbali na kukagua uhai wa Chama na kuonana na wananchi, Maalim Seif anatumia fursa ya ziara hizi kupeleka ujumbe maalum kwa wakaazi wa Pemba, ambao ni kuwataka wajitokeze kwa wingi kwenye zoezi la kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuanza katika wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini, Pemba, kuanzia tarehe 6 Julai mwaka huu. Kwamba kila mmoja ahakikishe kuwa anaandikishwa kuwa mpiga kura. Ujumbe huu unakwenda sambamba na azma ya CUF kuhakikisha kuwa Pemba inabakia kuwa ngome yake isiyopenyeka wala kutetereka.

  Ujumbe huu wa Maalim Seif unakuja katika wakati ambapo tayari CUF imekusanya ushahidi wa kutosha unaothibitisha kuwa kuna ‘utatu’ usio mtakatifu (trinity of the demons) baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Idara ya Vitambulisho Zanzibar, unaopanga njama za kuhakikisha kuwa wakaazi wengi wa Pemba hawaandikishwi kuwa wapiga kura. Katika mtandao huu, njama iliyopangwa ni hii: SMZ iwatumie masheha wake kuhakikisha kuwa hawatoi barua za uthitisho kuwapa watu wanaodai vitambulisho vya Uzanzibari, Idara ya Vitambulisho isimpe kitambulisho hicho mtu ambaye hana barua ya sheha na ZEC isimuandikishe kuwa mpiga kura mtu ambaye hana kitambulisho. Hadi sasa watu 18,000 kisiwani Pemba pekee wamesharipoti kunyimwa vitambulisho hivyo vya ukaazi huku hata zoezi la uandikishaji wapiga kura likiwa halijaanza. Lakini, licha ya kuwepo kwa taarifa hizo, ujumbe wa Maalim Seif kwa wananchi wa Pemba unabakia kuwa ule ule: lazima wahakikishe kuwa kila mwenye haki ya kuwa mpiga kura anaingia kwenye Daftari hilo.

  Kwa ZEC, SMZ na Idara ya Vitambulisho, ujumbe wa Maalim Seif ni kwamba kinachofanywa na taasisi hizo kinaipeleka nchi katika machafuko na matatizo makubwa, ambayo ni wao ndio watakaobeba lawama kwa matokeo yoyote yatakayotokea. CUF kila siku itasimama upande wa haki na sio tu kuhakikisha kuwa haki hiyo ipo, lakini kuona kuwa haki hiyo inatendeka.

  Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete, ujumbe wa Maalim Seif uko wazi. Kwamba Rais Kikwete ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na kwamba yeye ndiye mwenye dhamana ya usalama wa raia na mali zao. Kwa hivyo, asijiwache kuchukuliwa na andasa za kihafidhina zilizopo Zanzibar na kuja kusababisha kuvunjiwa heshima yake. Atumie nafasi zake alizonazo kuhakikisha haki inatendeka Zanzibar na sio kutumia nafasi hizo kutafuta wakala wa kumuweka madarakani kwa lengo la kupata wepesi wa kuyachimba mafuta ya Wazanzibari. Hilo halitavumiliwa hata kidogo na Wazanzibari na halitakuwa na manufaa kwake binafsi na kwa nchi nzima kwa jumla. Maalim Seif anamtaka Rais Kikwete asifuate nyayo za mtangulizi wake, Benjamin Mkapa, ambaye anajuilikana kwenye kama kiongozi aliyesimamia mauaji ya Januari 2001 na kuzalisha wakimbizi kwa mara ya mwanzo katika historia ya Tanzania huru.

  Kwa jumuiya za kimataifa, hasa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), ambalo linafadhili zoezi hilo la kuandikisha wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu, ujumbe wa Maalim Seif ni kwamba taasisi hiyo ya kimataifa ijitoe mara moja katika ufadhili huo hadi hapo itakapohakikishiwa kwa vitendo kwamba SMZ na ZEC hazitumii nafasi zao kuwanyima haki zao Wazanzibari. Kuendelea kufadhili zoezi hili, anasema Maalim Seif, ni sawa na taasisi hiyo ya kimataifa kushiriki katika mpango wa kuiviza demokrasia Zanzibar, ilhali ilivyotakiwa ni kwamba UNDP isaidie kuimarisha demokrasia na haki za binaadamu.


  SOURCE: KURUGENZI YA UENEZI NA MAHUSIANO YA UMMA,
  THE CIVIC UNITED FRONT,S.L.P 3537,SIMU 0777 414112
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Jamani mjumbe hauwawi ehh
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tatizo sio kujiandikisha wala kupiga kura, wenyewe wanasema ile nchi ya mapinduzi haitolewi kwa kipande cha karatasi!
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sisi yetu macho lakini sijaona tofauti kati ya Jk na Mkapa na hii itadhibitisha mwakani wakati wa uchaguzi maana wakati ule Mkapa nguvu za CUF zilimshindwa ndio maana akamua kutumia Nguvu Kubwa sana
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Maalim Seif Shariff Hamad awaachie wengine kila uchaguzi ni yeye tu haoni wenza Mbowe,Cheyo na Mzee wa Kiraracha wamekimbilia kwenye majimbo yao uchaguzi.Maalimu Seif badala ya kuimarisha CUF bara kaamua kubaki na Pemba yake !!!.Ndiyo maana Lwakatare kawakimbia baada ya kubaini hyiki chama macho na masikio yako Zanzibar tu.


  Maalim Seif Shariff Hamad hajui mafuta ni mambo ya muungano na yataendelea kuwa ya muungano atake asitake.Lau kama anataka kubadili katiba sharti hoja ilepelekwe bungeni si Gombani au Chake chake.
   
 6. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tabaan. Hauwawi !!!Junius. Tunashukuru kwa hayo uliyotuwekea jamvini. Mimi nikichangia mada nasema kwa maoni yangu. Seif Muflis- hana mpya. Nielewe Junius siikandii CUF hata siku moja. Nina imani kamili na CUF.
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Haya mwanakwetu nitafune huku unanipuliza.
  Lakini Pakacha,nkukumbushe kitu, namkumbuka Marehemu Prof. Haroub Othman(Mw'mungu amrehemu) wakati fulani akisema katika mambo aliyokuwa hakubaliani nayo na yakimchukiza (akitaka kutoka machozi akisema hivi) ni mbinu na hila za makusudi zinazofanywa na wakubwa za kuwazuilia watu wenye haki,haki zao za msingi kama kujiandikisha na kupiga kura n.k
  Kwani kuna tatizo gani ikawa kila mwenye haki ya kuandikishwa akapata haki yake akapiga kura kwa amani na utulivu, ikawa uchaguzi wa kura moja mtu mmoja, halafu chama chochote kikashinda na walishindwa wakaheshimu matokeo?
   
 8. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bali?
   
 9. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Khee!! imekuwa nongwa!!! Waliosema hayo wako wapi? Njooni katika kisanduku cha kura mkishindwa -basi mkae chonjo- Hiyo ndo Demokrasia. Huo ndio ustaarabu.
   
 10. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 341
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Aagh huyu Ba Hamad hana mpya hata mimi sina tatizo na cuf, tatizo ni huyu jamaa. Hivi zbar hakuna chama cha tatu chenye nguvu!
   
 11. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Amekuchukulia mke wako au nini, kama amechaguliwa na wanachama lazima ukubaliane na demo-crazy
   
 12. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sasa hiyo ndio demo-crazy. CUF is good -Seif anaiharibu CUF.
   
 13. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Demo-crazy. Si ndio Seif huwaambia wale ndugu zetu kule eti waandamane waende vituoni kwa Polisi wameshika mawe na mapanga. Unafikiri Polisi atafanya nini? Si atafyatua risasi tu? Seif amewauwa (na amewahujumu) wale Ndugu zetu waliopigwa risasi. Huyo jamaa hatufai Bwana
   
 14. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 341
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Acha us-e-nge wewe, unawashwa!
   
 15. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Vipi tena mbona unakurupaka? what is your point?
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nguvu za CUF zilimshinda Mkapa au Karume? CUF was no threat to Mkapa's presidency because Mkapa alishinda uchaguzi kwa about 70% of the vote so kura za Z'bar zisinge change matokeo. Ni Karume ndiye aliyekuwa in danger.
   
 17. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Seif hana jipya agombee ubunge atulie.....
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kama miaka 15 ya mfumo wa vyama vingi Maalim Seif kawa hana mpya, vp chama chetu kitukufu cha Mapinduzi(CCM) katka miaka zaidi ya 40 ya utawala wake,kuna lolote la kujisifia kwa mwananchi wa kawaida, mlala hoi bin miguu juu kama mm?(sjuwi ww mwenzangu)
   
 19. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mengi tu. Kila ndege huruka kwa ubawa wake. Hatutegemei sisi wa chini CCM ituletee maisha mazuri kama wale walioko Dubai. Lakini kwa ubawa wetu hatuwezi kuwa wakosefu wa shukurani.
   
 20. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Dunia hii kweli ya miujiza! tu-ndege wa ubawa mmoja lakini wengine mwisho wetu kuruka ni vitawi vikavu na kivuli kisichotosheleza kujificha jua. Wengine miaka hiyo 40 wamefaidi peke yao kuruka mbaali na kufikia vitawi vibichi vya "matunda ya Mapinduzi" na "kivuli" cha neema "daima", kibaya zaidi "hata hizo punje punje zinazodondoka,sisi wenye vibawa vidogo vidogo tusioweza kuruka mbaaali kama wenzetu tunapunjwa, tunaambiwa eti sisi "makinda" bado. Haya na tubembeze hizo "Riale" na "paundi" mbilitatu, tusijekufa njaa, maana tushaambiwa kama "hatuyaoni maendeleo tuhame".
   
Loading...