Ninaitwa Juma Hassan, kijana mhitimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam-UDSM 2015 katika kitivo cha humanitia na sayansi ya jamii.
Kutokana na hali ya serikali kupanga bajeti bungeni na kuipitisha kwamba wataajiri waalimu elfu 40 na baadaye kutuaminisha kwa kupitia tangazo lililotolewa na wizara ya TAMISEMI tarehe 13/5/2016 kukanusha uvumi uliokuwa umeenea kwamba serikali haita ajiri waalimu wa masomo ya sanaa na biashara ni uwongo tulifurahi na kutulia tukijua mambo yako mbioni kwa waalimu wote.
Kitu ambacho kimetuhuzunisha na kutukatisha tamaa hasa wahitimu waliosoma masomo ya sanaa ni kauli za serikali toka TAMISEMI, WIZARA YA ELIMU NA UTUMISHI zinatofautiana katika kutoa kuhusu ajira za waalimu.
TAMISEMI na UTUMISHI walituaminisha kwamba ajira zipo na ni zakutosha, lakini tunashangaa ubaguzi wa kutoa ajira ulio anza kwasasa
Ni jambo la kusikitisha sana kuona tulipewa matumaini makubwa sisi watoto wa masikini wa nchi hii tunaojaribu kuchukua fani ya ualimu kama kimbilio letu la kuokoa maisha yetu sasa tunaonekana kama tumepoteza muda shuleni kwa kusomea ualimu miaka yote.
Wanaosomea ualimu wengi wanatokea familia duni na wana amua kusomea ualimu iwe kama fani yao kwasababu hawana uwezo wa kifedha wa kusomea vitu vingine hiyo ni kutokana na utoaji wa mikopo vyuo vikuu nk.
Wizara ya Elimu na serikali kwa ujumla imeleta mfumo wa kibaguzi wa kuwatenga watu kwa masomo na kuaminisha jamii kwamba sisi waalimu wa sanaa hatukufaulu wala kufanya vizuri na tulikuwa vilaza shuleni ndio maana hatuajiriwi. Je bila waalimu wa sanaa mnao wakataa sasa hivi, wanasheria, waandishi wa habari hata nyie mlio wengi serikalini mngekuwa wapi?
Ukisoma C.V ya wabunge na mawaziri wengi kwenye tovuti ya bunge, utagundua asilimia 99.9 wamesoma masomo ya sanaa na leo hii wanaongea kwa kejeli kana kwamba wao ni majinias wa dunia nzima.
Yani mtoto wa masikini anasoma miaka zaidi ya 16 akitumaini atakuja kupata ajira kwa kupitia ualimu lakini leo anaambiwa akajiajiri.Hivi nyie mbona hamjawahi kujiajiri tokea nchi ipate uhuru? tunasikia mnafanya kazi za serikali tu.Sasa kijana aliyetokea chuoni tena aliyesomea fani ya ualimu mnataka ajiajiri kwa namna gani wakati mikopo yenyewe inatolewa kwa masharti magumu huko mabenki? Hivi kwanini mmekosa utu na kujifikria wenyewe bila kuwafikiria na watu wengine?
Mfano, sikuwahi kusikia Ndalichako amejiajiri mwenyewe tokea amalize chuo, lakini sasa hivi amekomalia vijana wajiajiri bila kusema wajiajiri kwenye nini na wapi.Viongozi wa serikali mnatoa kauli za ajabu na za kebehi kwa watoto wa watanzania wenzenu bila kuzingatia maisha yalivyo.
Kumbukeni mnapomwathiri mwalimu mmoja, mmeathiri sehemu kubwa ya familia na ukoo walioko nyuma yake wanaomtegemea.
Sasa hivi vijana wa 2015/16 wako mtaani yapata mwaka mmoja bila ajira maalum, halafu mtu anasema tufanye kazi bila kutuambia ni kazi gani.Wataalamu wa elimu ambao wangekuwa wanainua elimu nao wamegeuka kuwa wanasiasa.Wanahubiri chuki na uwongo kila kona ya nchi kwamba waalimu wa sanaa wametosheleza wakati kuna shule kibaoooo hawana waalimu hata hao wa sanaa.
Kama mnaona waalimu wa sanaa na wa shule za msingi wametosheleza kwanini mnazidi kuwapokea huko vyuoni na kuwapa mikopo? Mbona mnazalisha uasama wenyewe? kwanini msifute kozi za ualimu sanaa na muweke kozi za kijasiriamali ili mtu anapotoka chuo ajiajiri? hata hivyo sio kujiajiri tu mtoe na mikopo yenye kueleweka na sio kuongea kama miungu watu.
Kwamba ni awamu hii ya 5 ndio waalimu waliokufa, walio staafu nk wamefufuka baada ya uhakiki wa vyeti.Maana mlituaminisha kwamba baada ya vyeti feki kuisha mtawaajiri vijana wengi wenye sifa kujaza nafasi za wenye vyeti feki, lakini leo hii naona hata hao waliokuwa na vyeti feki namba yao inatajwa kwenye makaratasi tu bila ukweli wowote.Acheni siasa haya ni maisha ya watu.
Mbona watoto wenu hamwasitishii ajira BOT wala kuhakiki vyeti vyao? Haya ni maisha tu Ndalichako, maana wewe na viongozi wa juu ktk serikali ndio mmekuja na sera za kupunguza waalimu kwa uwongo kwamba wametosheleza.Hivi bajeti mlipitisha bila kujua kwamba mnahitaji waalimu wangapi? mlikurupuka kwanini? je watakao hitimu 2017 mtazidi kuwadampo mtaani kama mlivyo tudampo?
Kwanini msiseme tu kwamba serikali haina pesa tu ijulikane kuliko kutumia sababu za kudhalalisha kwamba waalimu wa sanaa wametosha? mbona madaktari,maafisa kilimo,maakimu nk mmekoswa sababu za kutoa kuhusu ajira zao? kwahiyo madaktari naowametosha kwenye awamu hii kurupushi ya maigizo? Tatizo mmliingia kwa akili kubwaaa mkidhani ni rahisi, sasa hivi mmebakia kuwatishia watu kwa kauli za ajabu.
Ndalichako punguza maneno, ishi kama mama mwenye utu na penda kuongea ukweli mtupu.Umekazania sayansi, sayansi wakati bajeti mmepitisha ya kuajiri waalimu wote bila,kwahiyo kumbe bajeti yenu ilikuwa hewa? au tuamini nini? Jafo na Simbachawene pamoja na Kairuki hivi ajira mlizokuwa mnawatangazia watanzania kwenye magazeti yako wapi? ajira elfu 71 mme mpa nani? Kumbukeni wakati wenu utapita na mnakufa n kuwa mizoga tu kama wanyama wengine.
Mnasababisha watoto wa masikini wanarudi kuanza upya na kuonekana hawakusoma kabisa.Hivi kwa mfano, katika akili ya kawaida, ni kozi gani ya ualimu inayofundishwa inayohusiana na kujiajiri?mbona nyie mmekaa serikalini na watoto wenu bila kuanzisha hata bustani tu ya nyanya? Mnakula kwa kupitia jasho letu la kodi, mnafurahia maisha kwa kutoa lugha za ajabu mbele ya raia lkn mwisho wenu utafika na mtapita kama upepo.
Mnajenga chuki baina ya wasomi walioko mashuleni,mnazidisha hamasa ya watu kuchukia kazi za ualimu na hata kukosekana kwa watakao soma kozi hizo zinazoonekana kama ni za laana kwa sasa.
Kozi za ualimu sio za kusoma halafu ukae mtaani, mtu akwambie ujiajiri.Ujiajiri kwa kufanyeje labda maana hamsemi tujiajiri wapi.Shule binafsi ni zenu nyie viongozi wa juu lakini cha ajabu ili mjue kwamba nyie ni wanafiki,waongo na wasaliti mme waa ajiri raia wa kenya na Uganda eti kisa wanajua kiingereza.Ujinga.
Endeleeni kufikiria kwamba haya maisha ni yenu na mtakaa wizarani daima.Hata Samwel Sitta alikuwa na ndoto za kuwa Rais lakini sasa hivi hatunaye, kwahiyo mtambue kwamba hapa tunapita tu.Viongozi wa serikl ya awamu ya 5 wanaongea kama vile wao ndio wanamiliki dunia.Tena wengine wameteuliwa tu.
Nawashangaa wabunge wa Tanzania walivyo vilaza, yaani utashangaa bajeti ijayo wanaipitisha kwa mbwembwe wakati hata iliyopita haijatekelezwa walau robo.Yaani kitendo cha serikali kununua ndege ndio mmeona mme maliza? kwamba tumbua tumbua mnaona mmefanya kazi kubwaaa na kutembea nchini mkiongea maneno ya kebehi.Fanyeni hayo lakni mjue wale watanzania wajinga wakuburuzwa wanazidi kupungua kila kukicha, mtawadanganya watu lkn sio wote.
Ifike hadi Serikalini kwa viongozi wenye roho mbaya na wajue kwamba huku mtaani, hatuwaelewi kabisa.Msifikirie mkishangiliwa kwamba mnakubalika,kuna wengine wanashangilia kwasbb mmewapa pesa wafanye hvyo na wengine wanazomea kama hamjui.
Ni mhitimu chuo kikuu cha Dar 2015