Ujumbe Maridhawa kwa Wanawake Wote

Ujumbe Maridhawa kwa Wanawake Wote

Mango juice

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Posts
345
Reaction score
469
Ndugu wanajamvi natumaini ni wazima wa Afya Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.

Wengi katika Wanawake siku hizi wameshindwa kujua nini maana ya neno ndoa. Wanadhania ndoa ni kupika na kufua na kupanda kitandani basii na hata akiachika hapa ataenda kuolewa kule..

Kama wewe mke unayesoma hapa ni miongoni mwa wenye mawazo finyu ya aina hii, acha hizo akili za kitoto. Ushakuwa mtu mzima sasa.

Kupata mume si kitu rahisi kama wengi wanavyofikiria. Kama huamini waulize marafiki zako ambao hawajaolewa watakujuza.. Hivyo tuliza kichwa mamaaa...!!!


Hiko ni kionjo tuu...Ila dhumuni la kuandika maneno haya ni kuikemea tabia mbaya mnooo iliyokithiri kwa wengi katika wanawake wa zama hizi ambao mimi binafsi naweza kusema ni wanawake wenye akili za kitoto, wasiojielewa na wasiojua kwanini wameolewa...!!!


Tabia yenyewe ni kitendo cha mke kutoka na kueleza madhaifu ya mumewe kwa mwanaume mwengine..

Waweza kuta mke anajiachia kueleza mapungufu ya mumewe nyumbani bila kujua wewe mke unafanya jambo la hatari sana..

Aweza kuwa ni rafiki yako wa karibu (maana kuna wake za watu wengine eti wana marafiki wa kiume ukiwauliza anakujibu, "He was just my classmate..") au mume wa rafiki yako, au mume wa dada yako, shemeji yako au hata mfanyakazi mwenzako..


Utakuta mwanamke yupo busy kumchambua mumewe mbele ya mwanaume mwengine.. Kila kosa analofanya mumewe analifikisha kama lilivyo... Tabia hii ni chafu mnoo kwa mke kuwa nayo..

Nakunasihi dada yangu kipenzi, kama wewe ni miongoni mwa wenye tabia hii, komaaaa..!!!


Usijaribu hata mara moja kumsimulia mwanaume yeyote mabaya na mateso anayokupatia mumeo, jinsi anavyokukera au vitu vinavyomshinda.. Utakuta wanawake wengine wapumbavu wanashtakia hadi mambo ya kitandani, mara "oooh mume wangu anawahi kuchoka, ooohh mume wangu haniandai vizuri..." sasa unakuja kutuhadithia huku sisi tukakuandae vizurii auu..!!![emoji3479]Mpumbavu wewee..!!

Sasa habari hizo si ukae chumbani na mumeo huko umchambulie,sie yanatuhusu niniii...!!


Nikwambie basi kama hujui, kufanya hivyo inakuweka katika hatari kubwa mnooo ya kumong'onyolewa kihisia na yule unayemuhadithia kila kukicha na taratibu anapata urahisi wa kuziingiza hisia zake kwako kwa sababu kashajua unakosa nini kwa mumeo..

Na wewe mke taratibu utaanza kulainika kihisia kwa kule kujali kwake, kusikiliza shida zako nawe itakuwia vigumu kumzuia kwani hakuna apingaye kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu kwa yule anayemjali na kuthamini hisia zake awe atakavyokuwa...


Wanawake wengi waliofanya hivi, wamejikuta wakiingia katika ngono na hata hisia zao kutekwa na wanaume wengine huku mume akibakia mikono mitupu..

Bila shaka hii imepelekea ndoa nyingi kuvunjika bila kujua sababu ninii kumbe ni upumbavu tu wa mke..


Nakushauri wewe mke, usithubutu kuwa na tabia hii maana wengi imewagharimu ewe dada yangu...


Tunajua kuna baadhi ya wanawake wanajua ubaya wa tabia hii kwa sababu walifundishwa makwao...


Ila hapa tunawalenga wale wasiojua kituu na makwao walifundishwa kuvukiza chumba udi na jinsi ya kupanda kitandani tuu kana kwamba hivi ndo vinadumisha ndoa.


Jifunze kuwa msiri wewe mke kwa yale yanayojiri katika ndoa yako, ukishindwa kamueleze baba yako sie wengine hatuna haja ya kusikia habari za mumeo....


Natumai ujumbe umefika mahali husika...




IMG-20190703-WA0023.jpeg
 
Haswaa ilo ni la ndani sana utamwambia mengine jiongeze! Lakini ukinijia mm na story kama hizo lazima nikusaidie kwa vitendo
Nimekuelewa sana
Lakini kumwambia baba yangu eti mume wangu hanifikishi ni ngumu sana
 
Ko shida kubwa n privacy et hope wamekuelewa,sema uzi umekuwa mrefu kama mahubir afu point n moja
 
Ooh nmechelewa kufika kwenye kikao

Aisee vikao ni vingi sana siku hizi
IMG_20190709_112146.jpeg
 
Hakuna namna ya kutuma huu ujumbe kwenye simu za wanawake wote kama ule wa katazo la rambo toka kwa PM? [emoji4]
 
Ndio maana hutufi mapema, hatuweki mafurushi moyoni. Anatafutwa wa kuelezwa hayo mengine ni matokeo.

Sio kazi sana ni kama vile mnavyoeaelezaga tu michepuko madhaifu ya wake zenu.
 
Sawa lakini kwanini utaje udhaifu wa mmeo kwa watu Je ww yakisemwa madhaifu yako utafurahi
Ndio maana hutufi mapema, hatuweki mafurushi moyoni. Anatafutwa wa kuelezwa hayo mengine ni matokeo.

Sio kazi sana ni kama vile mnavyoeaelezaga tu michepuko madhaifu ya wake zenu.
 
Sawa lakini kwanini utaje udhaifu wa mmeo kwa watu Je ww yakisemwa madhaifu yako utafurahi
Yaani badala ya kukemea maovu ya hao wanaume ndani ya ndoa unakemea wanawake kutoa siri za ndani nje? Eti hata kama mume anachepuka au anamyanyasa mkewe mke anyamaze tu unataka hayo anayoyaweka moyoni ayatoe vipi? Wewe unaweza kuvumilia mapungufu ya mkeo mfano kama mkeo anachepuka au anakujeuria utamvumilia bila kumfanya chochote kibaya?
 
Back
Top Bottom