Ujumbe mahususi kwa CHADEMA/ UKAWA kuhusu NEC

Fanfa

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2009
Posts
2,390
Reaction score
3,722
Nianze kwa kuwapongeza UKAWA kwa ujumla kwa mbinu na mikakati yao ambayo imeonyesha dhahiri kuipa wakati mgumu CCM. Hata hivyo jitihada zaidi zinahitajika kama mnataka kushinda uchaguzi huu la sivyo mtaisoma namba kama Rais kikwete alivyosema. Hakuishia hivo tu bali alienda mbali zaidi na kusema wanajua mbinu za kushinda na kwamba wana maarifa zaidi.

Moja ya mbinu na maarifa ya CCM ni hili hapa.

Napenda kuwakumbusha tu kuwa, Pamoja na mikakati yenu mizuri, ni wakati muafaka kwa CHADEMA/UKAWA kushinikiza utaratibu wa utangazwaji wa matokeo ya Urais katika ngazi ya vituo vya kuhesabia kura, ngazi ya kata na ngazi ya jimbo, yakatangazwa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi husika.

Sisemi kuwa watatangaza mshindi katika ngazi hiyo bali wasema idadi ya kura alizopata kila mgombea wa Urais ngazi ya kituo, kata na Jimbo mbele ya wapiga kura badala ya kubandika tu kwenye kituo. Hii itaondoa kwa kiwango malalamiko/mivutano isiyokuwa ya lazima na kuzuia uchakachuaji wa matokeo ngazi ya Jimbo na taifa kwenye majumuisho ya matokeo. Hili ni eneo muhimu sana ambalo CCM wataweza kupiga bao la mkono kama utaratibu hautabadilishwa.

Tukumbuke kuwa tume ikishatangaza matokeo ya urais ngazi ya Taifa hakuna kuhoji. Hilo nalo ni bao la pili la mkono.

Kupiga kampeni peke yako hakutoshi bila kudhibiti kwenye mchakatowa upigaji kura.

Kumbukeni kuwa kuiba kura sio rahisi ila kuchakachua kwenye majumuisho ni rahisi sana.

Yangu ni hayo tu kwa leo.
 
Samahani kamanda labda nina mawazo tofauti,kwani kwa kutumia BVR si kwamba matokeo yatakua yanaonekana mojamoja NEC hata kama hiyo kura imepigiwa huku kwetu Kishimundu? Tafadhali anayejua anaweza kunielewesha.
 
Mkuu ni kwamba hatutatumia upigaji kura kwa njia ya electronic bali upigaji kura utakuwa kama ambavyo siku zote tunafanya, yaani kura zinahesabiwa kwa mkono na kujumlishwa kwa mkono. Itachukua zaidi ya miaka 20 kuingia kwenye utaratibu wa Electronic vote, hii ni kwa mujibu wa tume ya uchaguzi

Kadi ya kura uliyonayo BVR inatumika tu kukupa uhalali wa wewe kuwa mpiga kura lakini upigaji kura na kuhesabu ni kama miaka iliyopita.

Sina uhakika.
 
Waulize CCM kwenye kura za maoni watakujibu swali lako kama huwa haziibiwa au la. Wana majibu mazuri sana kwa experience waliyopata

hivi kwani kura huwa zinaibiwa??
 
Waulize CCM kwenye kura za maoni watakujibu swali lako kama huwa haziibiwa au la. Wana majibu mazuri sana kwa experience waliyopata

nachokifahamu kura zingekuwa zinaibiwa au c.c.m wangekuwa wanaiba kura basi pale bungeni pasingekuwa na mbunge hata mmoja wa upinzani... ukiona mtu kashinda ujue kashinda kihalali
 
Nianze kwa kuwapongeza UKAWA kwa ujumla kwa mbinu na mikakati yao ambayo imeonyesha dhahiri kuipa wakati mgumu CCM. Hata hivyo jitihada zaidi zinahitajika kama mnataka kushinda uchaguzi huu la sivyo mtaisoma namba kama Rais kikwete alivyosema. Hakuishia hivo tu bali alienda mbali zaidi na kusema wanajua mbinu za kushinda na kwamba wana maarifa zaidi.

Moja ya mbinu na maarifa ya CCM ni hili hapa.

Napenda kuwakumbusha tu kuwa, Pamoja na mikakati yenu mizuri, ni wakati muafaka kwa CHADEMA/UKAWA kushinikiza utaratibu wa utangazwaji wa matokeo ya Urais katika ngazi ya vituo vya kuhesabia kura, ngazi ya kata na ngazi ya jimbo, yakatangazwa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi husika.

Sisemi kuwa watatangaza mshindi katika ngazi hiyo bali wasema idadi ya kura alizopata kila mgombea wa Urais ngazi ya kituo, kata na Jimbo mbele ya wapiga kura badala ya kubandika tu kwenye kituo. Hii itaondoa kwa kiwango malalamiko/mivutano isiyokuwa ya lazima na kuzuia uchakachuaji wa matokeo ngazi ya Jimbo na taifa kwenye majumuisho ya matokeo. Hili ni eneo muhimu sana ambalo CCM wataweza kupiga bao la mkono kama utaratibu hautabadilishwa.

Tukumbuke kuwa tume ikishatangaza matokeo ya urais ngazi ya Taifa hakuna kuhoji. Hilo nalo ni bao la pili la mkono.

Kupiga kampeni peke yako hakutoshi bila kudhibiti kwenye mchakatowa upigaji kura.

Kumbukeni kuwa kuiba kura sio rahisi ila kuchakachua kwenye majumuisho ni rahisi sana.

Yangu ni hayo tu kwa leo.
Hilo umenena,na idadi ya wapiga kura kila kituo ijulikane.Ukishapiga kura usiondoke kituoni mpaka upate matokeo
 
Hata nyumbani kwako kama hakutakuwa na ulinzi wa mali zako utaibiwa. Unapoona wapinzani wameshinda maana yake walithibiti sana uibaji wa kura na kuchakachua. Kumbuka kuwa kuna kuiba kura na kuna kuchakachua hayo ni mambo mawili tufauti

nachokifahamu kura zingekuwa zinaibiwa au c.c.m wangekuwa wanaiba kura basi pale bungeni pasingekuwa na mbunge hata mmoja wa upinzani... ukiona mtu kashinda ujue kashinda kihalali
 
Idadi ya wapiga kura huwa inajulikana, majina hubandikwa ukutani kabla ya kupiga kura.

Hilo umenena,na idadi ya wapiga kura kila kituo ijulikane.Ukishapiga kura usiondoke kituoni mpaka upate matokeo
 
Kadi ya kura uliyonayo BVR inatumika tu kukupa uhalali wa wewe kuwa mpiga kura lakini upigaji kura na kuhesabu ni kama miaka iliyopita.

Sina uhakika.

Duu! Kumbe kura zitakua kawaida?! Sababu ni nini? Hakuna vifaa vya kutosha au?
 
nachokifahamu kura zingekuwa zinaibiwa au c.c.m wangekuwa wanaiba kura basi pale bungeni pasingekuwa na mbunge hata mmoja wa upinzani... ukiona mtu kashinda ujue kashinda kihalali
Kaka upo dunia ipi? wale wa upinzani unaowaona pale bungeni ni wale ambao ilishindikana kuchakachua. 2010 upinzani ulishinda kuliko inavyoonekana.
 
Mkuu wakijaribu systems hiyo ya BVR kutakuwepo na zoezi la upigaji kura mwezi mzima endapo ufanyaji kazi utakuwa kama ule wakati wa kujiandikisha. Wenzetu wakenya iliwashinda uchaguzi uliopita.
 
Hilo umenena,na idadi ya wapiga kura kila kituo ijulikane.Ukishapiga kura usiondoke kituoni mpaka upate matokeo
Kwa mawazo hayo jiandae kupokea mkongoto wa nguvu wa FFU. Piga kula nenda nyumbani ukagange njaa. Acha uzembe!
 
Nianze kwa kuwapongeza UKAWA kwa ujumla kwa mbinu na mikakati yao ambayo imeonyesha dhahiri kuipa wakati mgumu CCM. Hata hivyo jitihada zaidi zinahitajika kama mnataka kushinda uchaguzi huu la sivyo mtaisoma namba kama Rais kikwete alivyosema. Hakuishia hivo tu bali alienda mbali zaidi na kusema wanajua mbinu za kushinda na kwamba wana maarifa zaidi.

Moja ya mbinu na maarifa ya CCM ni hili hapa.

Napenda kuwakumbusha tu kuwa, Pamoja na mikakati yenu mizuri, ni wakati muafaka kwa CHADEMA/UKAWA kushinikiza utaratibu wa utangazwaji wa matokeo ya Urais katika ngazi ya vituo vya kuhesabia kura, ngazi ya kata na ngazi ya jimbo, yakatangazwa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi husika.

Sisemi kuwa watatangaza mshindi katika ngazi hiyo bali wasema idadi ya kura alizopata kila mgombea wa Urais ngazi ya kituo, kata na Jimbo mbele ya wapiga kura badala ya kubandika tu kwenye kituo. Hii itaondoa kwa kiwango malalamiko/mivutano isiyokuwa ya lazima na kuzuia uchakachuaji wa matokeo ngazi ya Jimbo na taifa kwenye majumuisho ya matokeo. Hili ni eneo muhimu sana ambalo CCM wataweza kupiga bao la mkono kama utaratibu hautabadilishwa.

Tukumbuke kuwa tume ikishatangaza matokeo ya urais ngazi ya Taifa hakuna kuhoji. Hilo nalo ni bao la pili la mkono.

Kupiga kampeni peke yako hakutoshi bila kudhibiti kwenye mchakatowa upigaji kura.

Kumbukeni kuwa kuiba kura sio rahisi ila kuchakachua kwenye majumuisho ni rahisi sana.

Yangu ni hayo tu kwa leo.

Ni kweli kabisa
 
Electronic ni rahisi sana kuchakachua. hebu jikumbushe kenya. Na mwisho waliamua kuhesabu kwa mkono

Duu! Kumbe kura zitakua kawaida?! Sababu ni nini? Hakuna vifaa vya kutosha au?
 
Mkuu ni kwamba hatutatumia upigaji kura kwa njia ya electronic bali upigaji kura utakuwa kama ambavyo siku zote tunafanya, yaani kura zinahesabiwa kwa mkono na kujumlishwa kwa mkono. Itachukua zaidi ya miaka 20 kuingia kwenye utaratibu wa Electronic vote, hii ni kwa mujibu wa tume ya uchaguzi

Asante kwa ufafanuzi murua mkuu.
 
Samahani kamanda labda nina mawazo tofauti,kwani kwa kutumia BVR si kwamba matokeo yatakua yanaonekana mojamoja NEC hata kama hiyo kura imepigiwa huku kwetu Kishimundu? Tafadhali anayejua anaweza kunielewesha.
Mkuu kura zitapigwa kawaida hivyo mleta mada amesema kitu cha msingi ni vyema watu wakafahamu idadi ya kura za urais kupitia kila kituo, kata na jimbo hii itapunguza kura kugeuzwa mana matokeo ya urais yakishatangazwa hata kama yamekosewa ni shiiidaaa
 
Back
Top Bottom