Ujumbe Mahsusi kwa KMK

TrueVoter

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
2,064
1,588
Salam Dkt. Kusiluka,

Tafadhali naomba uwepo MWONGOZO wa kuwatumia wastaafu kama watu binafsi kwenye mambo ya serikali, la kama wana jambo au maoni yoyote mazuri kwa nchi washauriwe kuanzisha TAASISI zao kama alivyofanya Mzee Ludovick Utto kwa kuanzisha Taasisi ya WAJIBU.

Ili serikali au nchi ikihitaji mchango wowote kwenye eneo lolote yeye mstaafu kupitia taasisi yake wawe engaged rasmi kutoa hicho ambacho serikali inahitaji..kupitia mafunzo au namna yoyote vile itaonekana inafaa.

Haiwezekani kuwa na wastaafu wategemezi kwa kujifanya wao wana ujuzi adimu ambao wengine hawana na hivyo serikali ni kama inalazimika kuwatumia kwa kila jambo, mfano huyu Omar Issa na Balozi Ombeni Sefue ni kama wao sasa ni consultants kwa serikali, kila mahali wapo mara ni wakuu wa vyuo vikuu, kwenye sekta ya sheria wapo, kwenye sekta ya nishati (TANESCO) wapo, sasa hivi tena tume ya mipango imeundwa wapo.

Ni kitu gani hiki??? Omar Issa alianzisha BRN chini ya Kikwete, awamu ya tano ilipoingia akaondolewa yeye na BRN yake..sasa karudi tena, pamoja na kufanya kazi kwenye mashirika makubwa nje ya nchi sijawahi kuona mchango wake alipokuwa huko kwa nchi! na ni ajabu hata andiko tu moja la kitabu hawana.., unawaaminije watu wa namna hii?

Iko hatari moja hapa, nchi inaweza jikuta inafanyia kazi mawazo ya watu/wastaafu ambayo hayajawahi kujaribiwa popote hata kama ni mazuri hatimaye kuipeleka nchi kusikopaswa! Ni bora zaidi kuwa na utaratibu wa ku-engage TAASISI kwa kazi maalum kama anavyofanya Mzee Uttoh kupitia WAJIBU sababu kutakuwa na liability.

Kuliko kuwazungusha hawa wastaafu wanaojifanya wana "MADINI" yasiyoisha kwa ajili ya nchi, kumbe haja yao ni kuwa wategemezi kwa serikali na kuishi maisha ya kuwa Parasite kwa hofu ya kuwa maskini..!
Angalia mifano ya wastaafu wenye uwezo wa kuona namna nzuri kutumia uzoefu wao kwa ajili ya nchi.

Watu kama Donald Kaberuka, Frannie Leautier wana TAASISI inaitwa SOUTH BRIDGE Home | SouthBridge haya ndio wanatakiwa kufanya hawa wastaafu wetu hapa nchini na si kugeuka kuwa mzigo kwa serikali na nchi na baadae ku-mislead nchi kwa kutoa ushauri mbaya!
 
Salam Dkt. Kusiluka,

Tafadhali naomba uwepo MWONGOZO wa kuwatumia wastaafu kama watu binafsi kwenye mambo ya serikali, la kama wana jambo au maoni yoyote mazuri kwa nchi washauriwe kuanzisha TAASISI zao kama alivyofanya Mzee Ludovick Utto kwa kuanzisha Taasisi ya WAJIBU.

Ili serikali au nchi ikihitaji mchango wowote kwenye eneo lolote yeye mstaafu kupitia taasisi yake wawe engaged rasmi kutoa hicho ambacho serikali inahitaji..kupitia mafunzo au namna yoyote vile itaonekana inafaa.

Haiwezekani kuwa na wastaafu wategemezi kwa kujifanya wao wana ujuzi adimu ambao wengine hawana na hivyo serikali ni kama inalazimika kuwatumia kwa kila jambo, mfano huyu Omar Issa na Balozi Ombeni Sefue ni kama wao sasa ni consultants wa serikali, kila mahali wapo mara ni wakuu wa vyuo vikuu, kwenye sekta ya sheria wapo, kwenye sekta ya nishati (TANESCO) wapo, sasa hivi tena tume ya mipango imeundwa wapo.

Ni kitu gani hiki??? Omar Issa alianzisha BRN chini ya Kikwete, awamu ya tano ilipoingia akaondolewa yeye na BRN yake..sasa karudi tena, pamoja na kufanya kazi kwenye mashirika makubwa nje ya nchi sijawahi kuona mchango wake alipokuwa huko kwa nchi! na ni ajabu hata andiko tu moja la kitabu hawana.., unawaaminije watu wa namna hii?

Iko hatari moja hapa, nchi inaweza jikuta inafanyia kazi mawazo ya watu/wastaafu ambayo hayajawahi kujaribiwa popote hata kama ni mazuri hatimaye kuipeleka nchi kusikopaswa! Ni bora zaidi kuwa na utaratibu wa ku-engage TAASISI kwa kazi maalum kama anavyofanya Mzee Uttoh kupitia WAJIBU sababu kutakuwa na liability.

Kuliko kuwazungusha hawa wastaafu wanaojifanya wana "MADINI" yasiyoisha kwa ajili ya nchi, kumbe haja yao ni kuwa wategemezi kwa serikali na kuishi maisha ya kuwa Parasite kwa hofu ya kuwa maskini..!
Angalia mifano ya wastaafu wenye uwezo wa kuona namna nzuri kutumia uzoefu wao kwa ajili ya nchi.

Watu kama Donald Kaberuka, Frannie Leautier wana TAASISI inaitwa SOUTH BRIDGE Home | SouthBridge haya ndio wanatakiwa kufanya hawa wastaafu wetu hapa nchini na si kugeuka kuwa mzigo kwa serikali na nchi na baadae ku-mislead nchi kwa kutoa ushauri mbaya!
Makini
 
Duh.. Kwani Wewe umeathirikaje kwa Matumizi ya hayo 'Madini' Yasiyoisha..!(Nimetumia Lugha yako ulivyowaita)
Mimi mmoja naweza nisiwe naathirika, lakini tuongelee kwa level ya nchi..mfano BRN aliyoanzisha Issa iliishia njiani na tayari ilikuwa imeshatumia rasilimali za nchi..MUDA kwa mfano kutekeleza jambo ambalo badae linaishia njiani, hadi leo hakuna anayefahamu matokeo ya BRN kwa nchi kimaendeleo yalikuwa nini..hata aliyeanzisha hajawahi kusimama kutetea hicho alichokuwa anaamini, miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru bado tunafanya majaribio pasina uhakika kama hiki kinafaa au hakifai, hata anayekianzisha hana guiding material yoyote kwa hicho anachoanzisha..MKURABITA kwa mfano ipo hadi sasa, na references zipo..kuna mapungufu mengi ku-hire mtu badala ya Taasisi kutekeleza wazo lake, akifa ghafla..mnaendeleaje na hicho alianzisha? vipi rasilimali mlizotumia kwa jambo lisilokamilika inakuwaje?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom