Ujumbe kwako Kijana popote ulipo

Ujumbe kwako Kijana popote ulipo

Wana siasa wa Tanzania ni zawa na mabomba ya maji. Maji yapo ruaha ila yanafika na kukingwa Dar kupitia mabomba.

Hawapo hapo kutengeneza chachu bali ni kipitishio cha maagizo ya mataifa makubwa kuwapangia cha kutekeleza.

Viongozi wa kweli ni wanaume katika jamii,hao ndio wenye pawa na uwezo wa kusema nini kiwe na nini kisiwe katika jamii. Wao ndio serikali yenyewe.

Kwasasa wanaume halisi wamelala. Kuna haja ya kupiga nduru ya kiume ili katika kila kona waamke na kushika nafasi zao tuijenge upya hii jamii iliyo mahututi kabla haijafa na kuoza.

Leo wachina, wasomali, wapo mitaani mwetu wanatekeleza majukumu yetu na vijana kwasababu ya kutoandaliwa vema wamekosa power ya kufanya jambo.

Kupitia hizi forum misingi ijengwe na kuimarishwa vijana warudi katika nafasi zao ili uanaume uanze tena majukumu yake.
Wasomali na wachina huwa wanapewa mitaji na Serikali zao .

Vijana wamekuwa Kama panchi begi kila MTU anajipigia utasikia vijana hivi vijana vile .

Makosa ya Serikali ya sisiemu kushindwa kuwajibika.
 
Dah old good days ,wazee kama hawa walipotea hapa jamvini na sisi tukapoteleana .
Ahsante mzee be blessed once more .

Note:Ukiona nimeongea jambo nikaongeza na kingereza jua nimeappreciate sana hivyo taarifa kwa haters msiniquote hapa maana vita haitaishia hapa
Amina mkuu. Shukurani sana mkuu kwa kupokea ujumbe.
 
Wasomali na wachina huwa wanapewa mitaji na Serikali zao .

Vijana wamekuwa Kama panchi begi kila MTU anajipigia utasikia vijana hivi vijana vile .

Makosa ya Serikali ya sisiemu kushindwa kuwajibika.
Kabisa mzee.
 
Kwasisi vijana ambao tayari tumetoboa kwenye umri mdogo na tumeajiri vijana kadhaa na bado tunakaza inatuhusu pia?
 
KIchina zaidi au sio mzee ngoja nikusalimie kichina usikimbie.

兄弟,继续做得更好,胜利是你一生的徽章。
Mkuu xiexie🙏 hizo character tumegombana sana na mchina class alikuwa anakaguwa had notes sio powaa
 
Kwasisi vijana ambao tayari tumetoboa kwenye umri mdogo na tumeajiri vijana kadhaa na bado tunakaza inatuhusu pia?
Wewe sasa ndio utakuwa mfano wa hiki nilichokisema. Umetendea haki uwepo wako kwenye jamii kwa kuwa makini na majukumu yako ya asili.
 
Back
Top Bottom