Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 10,651
- 22,817
Kijana huu ni ujumbe kwako ukufikie na ukukute katika hali ya kuelewa na usipoelewa soma tena vema uelewe. Wewe kama mtoto wa kiume unazaliwa na cheti na hadhi ya uongozi. Ndio maana baba yako huwa anasheherekea kimya kimya kujua kapata kidume na mama yako moyo wake huyeyuka kwa faraja na kujiumba tena kwa taswira ya uwepo wake kama mtetezi wake kutoka mbinguni. Huwezi amini mama yako anakukubali kuliko hata anavyomkubali baba yako.
Nimesema haya yote kukukumbusha thamani yako ya kiutendaji ambayo haiendi bure kila unapoionyesha kwenye jamii na kwa wale wanaokuzunguka. Wewe kama kijana kila anae kuona anakutazama kama suluhu sio kwasababu wanataka kukutumia bali ni kwasababu wewe ndie mtu pekee aliyepewa kibali na MUNGU kwa kuzaliwa nacho na kutembea nacho kifuani. Kwa kifupi wewe ni makamo kama sio waziri mkuu wa MUNGU ambaye amekuja ulimwenguni kutekeleza majukumu yake ya kujenga jamii bora yenye mwenendo wa kumpendeza MUNGU.
Najua unaweza kuwa ni yatima ama umetengwa na baba yako tokea utotoni na hii imekufanya ujihisi wewe ni tatizo ama hauna umuhimu katika jamii. Ujumbe huu ukufikie kwamba baba yako ni MUNGU huyu wa duniani ni baba wa kiulimwengu ambaye amepewa jukumu la kumuwakilisha aliye mbinguni. Ikatokea amefeli au kufariki na hivyo kushindwa kuyatekeleza majukumu yake kisawa sawa hapo sio mwisho wako kwasababu wewe bado unaripoti kwa baba yako halisi wa mbinguni.
Popote ulipo kuna majukumu yako kiasili yanakusubiri na kuna washirika wako wanakungojea uanze majukumu yako ili na wao wajoin mfumo maisha yaendelee. Popote utakapokuwepo ukiwa serious watu ndio hupata chakula, ulinzi, sehemu ya kulala, amani, utulivu, matumaini, uhakika wa kesho yao,upendo, na zaidi faraja, yote hiyo ni wewe ukiamua kuwapa kupitia jitihada zako katika kutekeleza wajibu wako wa asili uliopewa na MUNGU.
Ukilala na kujifubaza na kulemaa au kupoa na jamii yote inayokuzunguka inaharibika pia na hofu inatanda, usalama unapotea, utulivu hautakuwapo, njaa itamshika kila aliyekuzunguka, chuki na wivu vitakuwa ndio fikra ndani ya kila anayekuzunguka,hakutakuwa na usingizi mzuri,na hakutakuwa na furaha. Yote hii ni kama wewe hautaamua kushika usukani wa majukumu yako.
Najua ulimwengu wa sasa unawapiga vita ya kiroho na ya kimwili watoto wa kiume na vijana na wanaume na kuwapa nguvu watoto wa kike na mabinti na wanawake. Wadhani sababu ni nini? Sababu ni wewe kijana unaniachia mimi, na wengineo wachache kusimamia majukumu na nafasi yetu ya kiume bila msaada wako. Ni kwasababu unakubali kukaa chini na kuachia jamii ijiendeshe yenyewe bila usimamizi na utendaji wetu wa kiume.
Nina mengi ya kusema na wewe ila najua tayari umeshanielewa kuwa nataka wewe na mimi tufanye nini ili kuiimarisha jamii yetu na kuirejesha katika ubora wake. Kwahiyo popote ukisoma hili andiko langu naomba ufaje kama kusimama na kuanza kujenga upya taswira yako ya kiume kwa wanaokuzunguka. Hebu tumia rasilimali zako kidogo ulizo nazo iwe ni simu au laptop,elimu yako,suti, vitabu, hiyo elfu 50 au milioni ya akiba, kufanya jambo la tofauti ambalo sio tu litakupa heshima bali litakupa kipato halali na utakidunduliza na kujenga mfumo wako wa maisha ambao wanaostahili watakuja kupata direction ya maisha kuanzia kwako. Kaa mbali na uhalifu na tabia za hovyo za ujana ambazo zinaweza kuharibu sifa yako na kukutoa kwenye mamalaka yako.
Kumbuka, “Cheaters never win” usiishi kwa kupenda mikato ya kufanikiwa. Maisha mazuri ni matokeo ya matumizi mazuri ya muda,jitihada na bidi kwenye kufanya maisha. Maisha sio magumu ila ugumu ni matokeo ya kulazimisha mifumo isiyo sahihi ikupe matokeo unayotaka. Stress, msongo wa mawazo,na depression sio magonjwa, ni njia ya mwili kukukataza kuweka kichwani mambo yasiyokusaidia maishani na ambayo hayana faida na wewe.
Nikutakie mafanikio mema popote ulipo ujumbe wangu ukufikie na uupokee.