Ujumbe kwa wanawake

Ujumbe kwa wanawake

Umepata bwana, umempenda kweli kweli na umemlalamikia sana eti kwanini hakupeleki kwa wazazi wake kukutambulisha, jamaa akagoma sana mwishowe akaona isiwe kesi akakupeleka.

Wewe badala hata utake hiyo advantage umefika tu siku ya kwanza umeshinda unachati, siku ya pili umeshinda unachati tena ndio unajisifia kwenye groups upo ukweni kumbe wao wanakutazama tu na kukupimia wala hawakwambii kitu.

Siku ya tatu wanakwambia leo ni zamu yako kupika, unaingia jikoni unaona kila kitu kigeni vya huku unaweka kule, vya kule unaweka huku (yaani hujui kupika chochote)

Sufuria unashika kama umeshika power bank, unapika na lipstick, mdomo mwekunduuu utafikiri mtoto wa jini katoka kufundishwa kunyonya damu tena huku umevaa saa, umevaa culture zimejaa nusu ya mkono, umevaa mini skirt kama wafanyakazi wa emirates.

Msosi wa wakwe huwezi kupika. Ukiambiwa hufai kuolewa unavuta mdomo utafikiri umenyimwa USB cable ubust smartphone yako.

Unaanza kulalamika wakwe hawakupendi, unalalamika weee, unashindwa kuelewa kuwa wewe ndo tatizo.

Usitake kuolewa ukidhani mumeo atakula chips na wewe utakuwa utakula pizza kila siku, jifunze hata kuchemsha chai basi au unadhani google wataleta Application ambayo unaweka USB kwenye simu yako alafu unaielekezea kwenye sahani inaproduce msosi.

#jipange dada usidhani ndoa ni kama kupiga selfie

Hahahahaaaa....
Mkuu huu ujumbe umekua maumivu kwa kina dada we angalia mda ulioupost halafu angalia na wachangiaji avilingani ingekuwa mambo mengine ungekuta kurasa zaid ya mia sasa lakini kwa kuwa ni mambo ya maana ki uhalisia lakini wao wanaona si yamaana lakini najua wachangiaji tu ndio hawachangii lakini wanaisoma ki100 ki100 😱😱😱😱😱
 
Mnachukua madada powa wanaoshindia chapati za mama ntilie na soda watajulia wapi kupika?
Mpk unampeleka kwenu hata humjui, unadhani anaaibika peke yake? Na wewe unayepeleka mwanamke wa hivyo kwenu unapata aibu tena unaonekana unaendeshwa nae ndugu hawatamsema huyo dada tu na wewe utang'ong'wa sana, "yaani ujanja wake wote kakamatwa na mwanamke hajui hata kupika mvivu n.k ". Kama unampenda muelekeze, aibu ni kwenu wote wawili hata ukimwacha baada ya hiyo introduction.
 
Na wewe mwanaume unamchukua msichana mpk ukamtambulishe kwenu hujamjua tu kuwa yupo hivyo? Hamjui kuchagua wake...mmekalia kuangalia sura na makalio. Wife materials wapo...tatizo akili ya kichwa kidogo imezidi ya kichwa kikubwa. Thats y mnapata matakataka ya namna hiyo. Kafundishweni kujua mwanamke yupi anafaa na yupi hafai.
Unalazimishwa kuoa na wewe unaingia kichwakichwa. Tatizo si huyo bidada ila ni la kwako.
Bils shaka una vinasaba na wahindi...!
 
Jamaa nakumbuka alimwacha msichana.mzuri sana kwa sababu hajui hata kupika chai
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom