Ujumbe kwa wanaume wote

Ujumbe kwa wanaume wote

bishontongo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2016
Posts
239
Reaction score
223
UJUMBE MUHIMU KWA WANAUME WOTE.

1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema.

2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia "Mimi ni mume wa mtu" au ninae mtu tayari.

3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, "wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao"

4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!

5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.

6. Tafuta mwanamke ambae atakupa changamoto za maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee!

7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.

8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu!

9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba ya karume etc

10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] haya bhana
 
Mwanamke mzuri na mwema ni yule anayekushauri usikimbie jukwaa la siasa kwakuogopa kukamatwa na kukukataza kujificha huku MMU
 
UJUMBE MUHIMU KWA WANAUME WOTE.

1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema. QUOTE]

Kusali pamoja ni ibada, vile vile kufanya mapenzi kwa maana ya tendo la ndoa ni ibada pia.
 
Back
Top Bottom