ujumbe kwa wanaoishi vvu, magonjwa ya muda mrefu na wengine wote

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
neno la kuanzia mwaka. kwa wanaoishi na virusi vya ukimwi wote, usiue ndoto zako sababu ya hali yako, unaweza kutimiza ndoto zako kama kuoa,kuwa na maisha mazuri na kuwa na familia yenye furaha na amani na hata kuwa na watoto wasio waathirika. unachotakiwa kufanya ni kuikubali hali uliyo nayo na kuacha kujihukumu. wenye virusi msijifiche na msijihukumu kama mlikosea sana. Mungu huwa mara zote anajua mwanzo wetu na mwisho wetu. kinachotakiwa na kufurahia muda tunaopewa na Mungu kuishi. ili mradi uko hai basi furahia uhai huo ulionao

kwa jamii,tusishabikie magonjwa ya wenzetu na kuwanyanyasa. kila mtu anatatizo lake, sema tofauti ni kulijua tu. tuwasaidie watu wanaoishi na virusi na pia magonjwa mengine kama kisukari, kansa na magonjwa ya muda mrefu. tofauti yetu na wanyama ni kwa sababu tunaweza kuthamini utu wetu, akifanyiwa ubaya mmoja basi tuwe na uelewa kwamba ni binadamu kafanyiwa ubaya,tusiwe kama nguruwe ambaye anaweza kuona mwanaye anachinjwa na baadaye akaanza kula mabaki na nyama ya mwanaye au simba ambaye njaaa ikimuuma anatafuna watoto wake. sisi ni binadamu ni lazima tulinde utu na ubinadamu

tuache umbea uliopitilia katika magonjwa ya watu. usichukue picha ya gonjwa bila ridhaa yake na kuileta mtandaoni. tujifunze kutumia mitandao vizuri na kuheshimu usiri wa wengine. unakuta mtu anakuja na picha ya mgonjwa facebook alafu anasema type amen, sijui hawa watu uelewa wao ukoje, kwani unadhani hatujui magojwa kama hayo yapo??? lazima tuelewe nini cha kuweka kwenye mtandao, ivi unaweza kujisikiaje baba yako mwenye ulemavu fulani anawekwa kwenye mtandao alafu mtu anasema sema amen!! au mshukuru Mungu kwa kukuepusha na haya, ina maana hao ni wakosaji sana na ugonjwa wao ni adhabu? lazima tujifunze kujua ni nini cha kuleta hapa na kuweka moyoni. ukitaka kujua kuhusu magonjwa ya watu kasomee udaktali. nachukia tabia hii toka moyoni

imefikia wakati ajali ikitokea unaona watu wako bize kuchukua picha ili wapost kwenye mitandao baadala ya kusaidia majeruhi. huo ni ulimbukeni na upuuuzi na tena ukihio. tutumie vizuri mitandao na kuheshimu usiri wa watu au faragha. umbea ni mzuri kiafya lakini ukipitiliza una madhara makubwa sana na unaweza kuleta vita. pia kaziza waandishi maana wanajua maadili ya kuripoti, wapeni matukio wao watujua jinsi ya kuyaleta kwenye jamii.

pia nawakumbusha watu wote ni vyema kujua wote ni marehemu watarajiwa na tofauti ni tarehe tu. tukijua kuwa sisi wote ni wapitaji , tujifunze kuishi kwa kuheshimiana,kufadhiliana,kuto kuhesabiana mabaya, kuvumiliana, kuchukuliana mizigo maana wote tuna mapungufu na tuepuke kujilimbikizia mali kwa kuwanyonya wengine. ukiwa na mali nyingi au kidogo, kinacholeta maana kwenye maisha ni kuishi na ndio maisha hayo. usiwaumize watu na usiache dunia au mali ikuendeshe mpaka ukapoteza moyo wako

namaliazia kwa kusema pia tusisahau kucheki afya zetu na kusaidiana na kuwekea mazingira ya usalama vizazi vilivyopo na vitakavyokuja
 
Back
Top Bottom