Ujumbe kwa wanandoa au walio kwenye mahusiano......

Ujumbe kwa wanandoa au walio kwenye mahusiano......

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
20,154
Reaction score
40,946
Habari za jumapili wapendwa....ni tumaini langu mpo salama salmini na wale wenye matatizo ya kiafya basi Mungu awafanyie wepesi....

Niende moja kwa moja kwenye mada bila ya kupoteza muda....

Hili jambo limekuwa likileta migogoro mingi kwenye mahusiano na muda mwingine kuvunja mahusiano yaliyokuwa na malengo makubwa mbele.....

Jambo lenyewe ni Dogo sana kimuonekano au linaweza kuonekna la kawaida lakini limebeba maana kubwa sana.....

Mwana ndoa au mtu yoyote aliyepo kwenye mahusiano anatakiwa kuwa makini sana namba yake ya simu na watu anaowapa namba za simu....kuna baadhi ya watu tunaowapa namba za simu lakini hawajui mipaka yao....hawajui muda na wakati gani wa kupiga au kukutumia ujumbe.....hawajui mipaka yao kwenye kutumia ujumbe....

Si jambo lenye kupendeza ukiwa umetulia na mpenzi wako alafu kuna mtu anakupigia simu mara kwa mara na kukutumia ujumbe kila muda kwa kuwa tu mnafahamiana......huwezi jua kuwa huyo mwenzako hilo jambo atalichukuliaje hata kama hataongea hasa ikiwa mtu huyo ni wa jinsia nyingine..........

Wakati mwingine tunawapa watu namba zetu za simu kwa nia nzuri alafu wao wanazitumia vibaya labda kwa kujua au kutokujua......Kwa mfano kama ni mambo ya kiofisi au kibiashara yana wakati wake....na sio mpaka usiku wa manane........haipendezi.....

Nawasilisha.....

NB;

Nimetoka kusuluhisha ugomvi wa wana ndoa kuhusiana na namba ya simu....baada ya mwanaume kuwa anapigiwa simu mara kwa mara hata wakiwa faragha na mke wake....
 
Kweli kabisa.Wanashindwa kutofautisha upi ni muda sahihi wa kupiga/kutuma sms.
 
Back
Top Bottom