Ujumbe kwa uvccm.the ordination.

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
Yesu sasa akawaagiza wale watu kumi na mbili ambao walikuwa wamesikiliza azimio lake kuhusu ufalme kupiga magoti kumzunguka. Akaweka mikono yake juu ya kichwa cha kila mtume,kuanzia Judas Iscariot na kuishia kwa Andrew. Baada ya kuwabariki akanyoosha mikono yake na kusali;
'' Baba yangu,sasa nawaleta kwako hawa watu[these men],taarishi wangu kutoka miongoni mwa watoto wetu duniani nimewachagua hawa kumi na mbili waende kuniwakilisha kama mimi nilivyofika kukuwakilisha. Wapende na uwe pamoja nao kama ulivyonipenda na kuwa pamoja nami. Na sasa,Baba yangu,wape hawa watu hekima ninapoweka shughuli zote za ufalme utakaokuja,mikononi mwao.Na ningependa,kama itakuwa utashi wako,nikae kidogo duniani kuwasaidia katika kazi zao za ufalme. Na tena,Baba yangu,nakushukuru kwa hawa watu,na ninawakabidhi kwakouwaweke ninapoendelea kumaliza kazi uliyonipa kufanya.''
Yesu alipomaliza kusali,mitume walibaki wameinama wote kwa dakika nyingi,na Peter ndiye aliyekuwa wa kwanza aliyethubutu kuinua macho na kumtazama Yesu. Mmoja baada ya mwingine wakamkumbatia Yesu,lakini hakuna aliyesema chochote. Kulikuwa na kimya kabisa katika sehemu hii,na viumbe wengi mbinguni walitazama chini kwa makini kinachoendelea,jinsi Yesu alipokaribia kuzikabidhi kazi za undugu wa kitakatifu ziwe chini ya uongozi wa akili za wanadamu.
Hotuba ya kusimika.
Halafu Yesu akazungumza akasema,
''Sasa ambapo ninyi ni mabalozi wa ufalme wa Baba yangu,mmekuwa kundi tofauti na watu wengine duniani. Ninyi sasa si kama watu miongoni mwa watu,ila ni watu raia walioerevuka wa nchi nyingine ya mbinguni kati ya watu wasio na ufahamu wa dunia hii yenye giza. Haitoshi kwamba muishi kama mlivyokuwa mnaishi kabla ya saa hii,bali kuanzia sasa mnapaswa kuishi kama wale ambao mmeonja utukufu wa maisha bora,na mmerudishwa duniani kama mabalozi wa Kiongozi wa ile dunia mpya na nzuri zaidi. Kutoka kwa mwalimu zaidi inategemewa kuliko kutoka kwa mwanafunzi. Kutoka kwa raia wa ufalme wa mbinguni zaidi inategemewa kuliko kutoka kwa raia wa utawala wa duniani.Baadhi ya mambo ambayo sasa hivi nitawaambia yataelekea kuwa magumu kwenu,lakini mmechagua kuniwakilisha katika dunia kama ambavyo mimi sasa namwakilisha Baba,na kama maajenti wangu duniani mtalazimika kuishi kufuatana na mafundisho na ada zinazotakiwa,zinazohitajika kwa maisha ya duniani,na ninazoonyesha katika maisha yangu ya dunia ya kufunua Baba aliye mbinguni.
'' Nawatuma kutangaza uhuru kwa watumwa wa kiroho,furaha kwa wale ambao wapo katika minyororo ya woga;na kuwatibu wagonjwa kufuatana na utashi wa Baba yangu mbinguni. Mkiwakuta watoto wako katika adha,zungumzeni kuwapa moyo,na kuwaambia;
''Heri walio maskini wa roho,wanyenyekevu,maana utajiri wa mbinguni ni wao,
Heri wenye njaa na kiu ya haki,maana watashibishwa,
Heri wanyofu,maana watairithi dunia.
Heri wenye moyo safi,maana watamuona Mungu.
''Na hivyo hivyo zungumzeni kwa watoto wangu maneno haya zaidi ya kuwafariji kiroho na kuwaahidi.
Heri wenye huzuni,maana watafarijiwa.
Heri wanaolia,maana watapokea roho ya furaha na kusherehekea.
Heri wenye huruma,maana watahurumiwa.
Heri wenye kuleta amani,maana wataitwa watoto wa Mungu.
Heri wanaoteswa kwa kufanya anavyotaka Mungu,maana ufalme wa Mungu ni wao.
Heri wale wanaotukanwa na kuteswa na kusemwa uongo mambo ya uovu ya kila aina. Furahini na kushangilia,maana zawadi yenu mbinguni ni kubwa.
''Ndugu zangu,ninapowatuma,ninyi ni chumvi ya dunia,chumvi yenye ladha ya kuokoa. Lakini kama chumvi ikipoteza ladha yake,itakolezwa na nini?Haifai kwa chochote isipokuwa kutupwa tu na kukanyagwa na watu.
Ninyi ni mwangaza wa dunia. Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika,wala watu hawawashi mshumaa na kuufunika kwa debe,ili huuweka juu ya kinara uwaangazie watu wote walio nyumbani. Hivyo hivyo,mwanga wenu uangaze mbele ya watu ili wayaone matendo yenu mema wamsifu Baba yenu aliye mbinguni.
Nawapeleka ninyi katika dunia kuniwakilisha na kuwa kama mabalozi wa ufalme wa Baba,na mnapokwenda kutangaza habari njema,wekeni imani katika Baba ambaye ninyi ni taarishi wake. Msipinge udhalimu kwa kutumia nguvu,usitumainie nguvu ya mkono wako. Jirani yako akikupiga shavu la kulia,mgeuzie lingine pia. Muwe radhi kuvumilia udhalimu miongoni mwenu, kuliko kwenda kwenye vyombo vya sheria, . Kwa upole na huruma wasaidie wote wenye matatizo na wenye shida.
Nawaambia wapendeni adui zenu,watendeeni wema wanaowachukia,wabarikini wanaowalaani,waombeeni wale wanaowatendea ubaya. Na lolote unaloamini mimi nitawafanyia watu,wewe watendee hilo hilo.
'' Baba yangu aliye mbinguni anaangaza jua kwa waovu na wema,pia analeta mvua kwa watenda haki na wasiotenda haki,ninyi ni watoto wa Mungu,na zaidi,ni mabalozi wa ufalme wa Baba yangu. Muwe na huruma,kama ambavyo Mungu ana huruma,na katika siku zijazo katika ufalme mtakuwa wakamilifu milele,kama ambavyo Baba yenu wa mbinguni ni mkamilifu.
''Mmepewa kamisheni kuokoa watu,siyo kuwahukumu. Mwisho wa maisha yenu ya dunia wote mtategemea huruma;kwa hiyo nawataka wakati wa uhai wenu,muonyeshe huruma kwa ndugu zenu. Msifanye kosa la kutaka kuondoa kibanzi kutoka kwenye jicho la mwingine wakati kuna gogo katika jicho lako. Kwanza ondoa gogo kutoka kwenye jicho lako halafu utaona vizuri na kuweza kuondoa kibanzi kutoka kwenye jicho la mwingine.
''Uelewe ukweli vizuri,ishi maisha ya haki bila woga,na hivyo mtakuwa mitume wangu na mabalozi wa Baba yangu. Mmesikia ikisemwa,'Kama vipofu wakiongozana,wote watatumbukia ndani ya shimo.' Kama unataka kuwaongoza wengine waingie katika ufalme,wewe mwenyewe lazima uonyeshe hukumu ya haki na hekima nzuri. Usiwape mbwa vitu vitakatifu,na lulu zako usiwatupie nguruwe,au watazikanyaga na kugeuka kukurarua.
''Nakuonya kuhusu nabii wa uongo ambao watakuja kwako na vazi la kondoo,wakati ndani ni mbwa mwitu wakali. Mtawajua kwa matunda yao. Je watu huchuma zabibu kutoka kwenye miti yenye miba au tini kutoka kwenye mbigili?Hivyo hivyo kila mti mzuri huzaa matunda mazuri,mti mbaya huzaa matunda mabaya. Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya,mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri.Kila mti ambao hauzai matunda mazuri hatimaye utakatwa na kutupwa katika moto. Ili uweze kuingia katika ufalme wa mbinguni ni nia ndio inahesabiwa. Baba yangu anatazama katika mioyo ya watu na kuwahukumu kutokana na nia na malengo yao.
''Katika ile siku kubwa ya hukumu ya ufalme,wengine wataniambia,'Tulitangaza ujumbe kwa jina lako,kwa jina lako tulifanya kazi nyingi njema'Lakini nitalazimika kuwaambia;'Ondokeni hapa ninyi walimu wa uongo' Lakini yule ambaye anasikiliza haya maagizo na kwa dhati anatimiza kamisheni aliyopewa kuniwakilisha kwa watu kama ambavyo mimi nilivyomwakilisha Baba yangu kwenu,atakaribishwa kwenye utumishi wangu na katika ufalme wa Baba yangu mbinguni.''
Mitume walikuwa hawajawahi kumsikia Yesu anaongea namna hii,kwa vile alikuwa anaongea kama vile alikuwa na mamlaka yoye. Walishuka kutoka mlimani,karibu na saa ya machweo,lakini hakuna aliyemuuliza Yesu swali.
 
Mkuu Ganesh huwa napata taabu kweli kuainisha yale unayoyaandika na yale unayotaka kuyasema. Kama hapa nimejaribu kufikiria umetaka kuwaambia nini UVCCM nimeishia hewani.
 
Ujumbe wangu kwa UV-CCM hapo,ujumbe mkubwa ni pale ninaposema wasitumainie nguvu za mikono yao,kama wanafanya kazi halali,watasaidiwa na vyombo vya sheria,ambao naona ni ujumbe mzuri,wakati huu ambapo wanajitayarisha kufanya kampeni za Uchguzi Mkuu.
 
Mkuu Ganesh,nimeiona,huwa nasoma ujumbe kutoka kwako,tafadhali nitaisoma kisha nitafakari alafu nitakuuliza swali ama maswali kama nitakuwa nayo.:angry:
 
Please, achana nafasi between paragraphs ili iwe rahisi kusoma! tunapata tabu kusoma makala ndefu katika hali kama hiyo! It's not a user friendly article!

Naomba uweke injili au mapokeo uliyotumia katika articles zako ili tukishindwa kusoma hapa tufuate huko yalipo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom