Ujumbe kwa IGP Mwema: Lini Tutaondokana na Polisi Wenye Kufanya Kazi kwa Maagizo ya Wanasiasa?

Ujumbe kwa IGP Mwema: Lini Tutaondokana na Polisi Wenye Kufanya Kazi kwa Maagizo ya Wanasiasa?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
14,176
Reaction score
25,919
Juzi hapa kulikuwa na thread iliyoandikwa kutaka Kamanda wa Polisi Morogoro, Shilogile ajiuzuru kutokana na suala la Ponda.

Nikichangia katika huo mjadala nilisema kwamba polisi wasomi kama kina Shilogile wametuangusha sana Watanzania, maana tulitarajia wasomi kama wao wangelibadilisha Jeshi la Polisi kutoka kuwa chombo kinachofanya kazi kwa maagizo ya wanasiasa na wenye uwezo wa kipesa kuwa chombo ambacho kinafanya kazi kwa kanuni za Polisi. Nilidiriki kusema Shilogile na wasomi wenzake katika Jeshi la Polisi sio polisi wenye ari ya upolisi (dedicated policemen) bali walijiunga kwa faida zao binafsi.

Kwa mfano, ikiwa Polisi wangekuwa wanaendeshwa kwa kanuni, wangeweza hata kuthubutu kumjibu Pinda kuwa Jeshi la Polisi halipo nchini kwa ajili ya kupiga wananchi, lakini hakuna hata Polisi mmoja alithubutu kukanusha kauli ya Pinda, pale alipotoa agizo wawapige wananchi.

Pia tumeshuhudia mambo mengi sana yakifanywa dhidi ya vyama vya siasa kwa kuwa Polisi waliambiwa wafanye hivyo na mwanasiasa fulani.

Leo nimesoma katika gazeti Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi akisema aliambiawa na Polisi pale Kawe yafuatayo; “Waziri aliagiza Mugishagwe akamatwe tangu Januari, nilikwenda Kituo cha Polisi Kawe, nilipowauliza kosa lake wakasema waziri ameagiza akamatwe.

Basi angalia kwamba tuna jESHI LA Polisi ambao, Waziri akisema "kamkamate yule umtie ndani" hata hawaulizi kafanya kosa gani, na wakiulizwa bila aibu wanasema "huyu bwana yuko ndani kwa sababu Waziri kasema tumkamate na kumweka ndani"

Hii Watanzania wenzangu ni aibu na kAshfa mno kwa Jeshi letu la Polisi.

Je basi, lini tutakuwa na Jeshi la Polisi ambalo Shilogile pale Mororgoro akiambiwa na mwanasiasa "kamkamate yule umtie ndani", badala ya kukimbia kama na kumkamata huyo mtu, atamjibu huyo waziri, kwa hekima tu, "mheshimiwa Waziri kama kuna kosa amefanya tuambie na sisi kama jeshi la Polisi tutachunguza na kumkamata tukiona kweli kafanya makosa".

Je IGP Mwema, karne ya uwazi na ukweli unaongoza Jeshi linakokiri hadharani kuamriwa na wanasiasa na kukimbia kutekeleza kama mchezo wa kutupa kijiti na mbwa akimbilie kukiokota na kukurudishia huku akitikisa mkia?

Ni aibu na kashfa mono Polisi kutumiwa namna hiyo na wanasiasa au watu wenye uwezo.
 
Back
Top Bottom