Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,821
- 6,122
Ndani ya wiki mbili hivi simu yangu ilikuwa imepata ahueni ya kutokupokea zile message za Tuma pesa kwa namba hii..
Kiasi chake nilihisi inaeza kuwa wale jamaa waliokamatwa Dar na rununu(simu)siziso na idadi na pia walikamatwa na Ngamizi kadhaa zilizokuwa na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi kwa watu wengi ndani ya dakika moja.
Lakini kumbe bado wapo na wanabadilisha mbinu,lakini hivi sasa mbinu yao hii inaweza kuwatajirisha kuliko ile ya mwanzo maana mbinu hii imeingia kulekule kwenye ugonjwa wa watu wengi nchini (kamari).
Lakini hii inakuja kuwapotezea soko watu wenye kampuni inayotajwa hapa (BIKO)maana raia wataendelea kuona ni kampuni ya kitapeli mara mbili zaidi ya sasa.
Wao waliponitumia wakaniomba nisimwambie mtu iwe siri yangu ila mimi nimeamua kuwashirikisha ili wale wanaonidai wajue nimeshinda BIKO
Aisee hii ni hatari bado najiuliza wale watu wa kule vijijini wanakocheza BIKO wakipata hii kitu si atakopa ili akomboe hii pesa alioshinda?!