Ujuha wa serikali ya kikwete

Jilanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
255
40
Iko haja ya kutumia nguvu ya umma pale serikali inaposhindwa kutambua wajibu wake na kuwajibika ipasavyo.
Unapokula kiapo cha kulinda maslahi ya Taifa si tena swala la kutoa majibu mepesi kwa mambo mazito ambayo yataligharim taifa kwa miaka mingi Ijayo! Nimeamua kuliwe hii mbele yenu kutokana na mwenendo mzima wa serikali yetu hususan ktk sekta ya Elimu ambayo ndo Moyo ama injini ya maendeleo ya taifa lolote duniani. Staki kuamini kwa Serikali na wizara husika hawanamajibu juu ya Wanafunzi 240903 kupata sifuri. Kuunda tume ya 4 kuchunguza kilichopelekea wanafunzi kufeli ni ni Ujuha ulokubuhi. Kwani Tume zote zilizotangulia kuanzia ya hayati Makweta, ya Juma Quara nk ni kuendelea kupoteza raslmali za watanzania kwa hamna tume ilowahi kutoa report kwa wadau husika! Watanzania tuamke kulinda maslahi ya taifa kwa kuwanyang'anya dhana wote walioshindwa kuwajibika kwani huu ni wajibu wa kila Mtanzania mzalendo. Inasikitisha sana!
 
hapo kwenye red hakuna mtu huyo hapa duniani na hajawahi kuwepo....na hapo kwenye blue ulikuwa unaharaka gani??? au unakimbizwa
 
ulitaka ifanyeje badala ya kuunda tume, acha kulalamika

Iongeze Budget katika sector ya elimu!
>Itaboresha huduma mashuleni kama vile vitabu, vifaa vya maabara, na vitendea kazi vingine!
>Shule kupatiwa waalim wa kutosha na walipe ujira stahiki!
>Serikali iandae mtaala mpya unaokithi mabadiliko ya sayansi na technology.
>Lugha ni tatizo kubwa wanafunzi wapatiwe dictionaries.
>wanafunzi wapatiwe japo mlo wa mchana!
 
hapo kwenye red hakuna mtu huyo hapa duniani na hajawahi kuwepo....na hapo kwenye blue ulikuwa unaharaka gani??? au unakimbizwa

red ni Omary Quaraa! Blue Nilimaanisha kuileta mada jukwaani, asante kwa critisize!
 
Tatizo la haya magamba hayashauriki hata ukitoa ushauri gani! Yanakuambia "ARE U A THINKING TANK OF THIS COUNTRY?
 
Iongeze Budget katika sector ya elimu!
>Itaboresha huduma mashuleni kama vile vitabu, vifaa vya maabara, na vitendea kazi vingine!
>Shule kupatiwa waalim wa kutosha na walipe ujira stahiki!
>Serikali iandae mtaala mpya unaokithi mabadiliko ya sayansi na technology.
>Lugha ni tatizo kubwa wanafunzi wapatiwe dictionaries.
>wanafunzi wapatiwe japo mlo wa mchana!

Mshkaji unastahili Nobel prize kwa kutoa suluhisho la matatizo ya elimu Tanzania.
 
Moja ya tatizo kubwa ni lugha ya kufundishia. Kubadili lugha ya kufundishia ghafla baada ya miaka saba ya mfumo wakufundisha kwa kutumia kiswahili nadhani ni kikwazo maendeleo ya mwanafunzi. Baya zaidi vitabu vote iwe hisibati sayansi ni kwa lugha ya kiswahili. Nadhani busara zaidi lugha zote mbili zitumike masomo ya awali darasa la kwanza hadi la tano na kubadilisha mfumo to full kingereza darasa la sita na saba (ie bilingual education with late exit strategy) mfumo huu umeleta mafanikio makubwa katika sekta ya elimu nchi nyingi ikiwemo USA,filipino.
 
Kuna ufahari gan kwa Government officials kutembelea gari za kifahari kulipwa milions of money wakati shule hazina vitabu! Wakati huo unataka muujiza wanafunzi kufaulu?
 
Hapo tupo pamoja sana. Kwani mm huwa najiuliza kila siku na kila dakika nashindwa kupata jibu. Inaonekana ss waafrika hatujui kwann tupo duniani. Hivi kunamaana gani baada ya miaka 100 kwamba jamaa alikuwa tajiri sana, anaishi kifalme na kuendesha magari ya bei kali au kutakuwa na maana kwamba huyu jamaa hameacha shule bora, barabara bora, viwanda bora na nchi nzima inakula matunda ya huyu jamaa.
Mm nazani vijana tusikatishwe tamaa na wachache wanaopenda kujilimbikizia mali kisa viongozi waliopita na waliopo wachache wao wanatufisadi bali tusonge mbele na mawazo yetu tutashinda siku yaja.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Tatizo la haya magamba hayashauriki hata ukitoa ushauri gani! Yanakuambia "ARE U A THINKING TANK OF THIS COUNTRY?

"WHO DOESN'T KNOW....WHO doesn't KNOW....WHO DOESN'T KNOW.......WHO DOESN'T KNOW that this country is.........."
 
Back
Top Bottom